Ummy Mwalimu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Diwani Mwinjanga na wote wanaohusika saidieni hawa vijana

Mama Mwana

JF-Expert Member
Jun 6, 2023
1,233
3,936
kuna vijana walichaguliwa kujifunza kilimo cha kisasa,wakiwa chini ya halmashauri ya jiji la Tanga na washirika wao Botna na SUGECO.

Saidieni hao vijana wapate stahiki zao wana akiba ya kiasi cha Tsh. million nane benki, wameachiwa mradi wauendeshe ajabu wanachosemea wameomba kutoa pesa walizotumia jasho lao kuendeleza mradi wamekataliwa na pesa zimekua na masharti kibao, mara zina watu wengi, mara mkataba haukusema watalipwa.

Kibaya zaidi afisa kilimo mkoa akawajibu kashtakini popote siogopi yoyote. Hongera diwani wa geza, anawahangaikia lakini mkurugenzi wa jiji hapokei simu za vijana kiasi wanahisi anahusika katika hujuma hio.

Waliahidiwa kupewa eneo pande lakini hakuna mrejesho wanaoupata, huu mradi upo sehem kunaitwa Nema - Tumbirini.
 
Back
Top Bottom