Mzungu ang'ata sikio la mhamiaji mjini Glasgow nchini Scotland wakisubiri chips na kuku KFC.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Mtu mmoja ambae inasemwa kuwa ana asili ya kigeni ameng'atwa sikio na kijana wa kizungu wakti wakisubiri chips na kuku ndani ya mgahawa maarufu uitwao KFC uliopo kwenye mtaa wa Renfield mjini Glasgow nchini Scotland.

Mtu huyo ambae inasemwa ana miaka 28 alikuwa akisubiri order yake na ndipo kijana huyo wa kizungu alipoingia mgahawani humo akiongozana na kijana mwenzie na msichana.Walipoingia kama kawaida wakaona kuna mtu wa kumchokoza na wakamwona mtu huyo kuwa ndio waanzishe zogo nae.

Mtu wa watu alipoona kwamba hawezi mambo ya zogo ikabidi atoke aende zake bila kuchukua chips na kuku ambazo alikwishaagiza.Kijana huyo wa kizungu alipoona hivyo aliamua kumfuata mtu huyo na kumshambulia na hatimae kufanikiwa kung'ata sikio lake karibu lote na kumsababishia jeraha kubwa mtu huyo.

Mtu huyo bado yupo hospitalini iitwayo Glasgow Royal Infirmary ambapo amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji.

296330-part-of-mans-ear-bitten-off-in-particularly-violent-glasgow-attack-410x230.jpg


Tukio hilo limetokea hapa.

Polisi wa kutoka kituo kikuu cha polisi cha Strathclyde wanafanya uchunguzi wao.Haya mambo ya chuki sijui yataisha lini.
 
huyo alieng'atwa sikio alikua ni mweusi? mana kama mweusi hapachelewi kusikilikana Black Live Matter
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom