Mzungu afukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau Waafrika!

tulikuwa tunakula vyakula nachurale....sio hivi vyenu vyenye madawa lukuki.....sato walikuwa wanavuliwa na nyavu....sio hawa wenu mpaka wavuliwe na baruti...sijui sumu.....ukimkuta sato pale chakula barafu ni mkubwa anakulingana.......


Da kweli mamam mkubwa maana cku hizi hii milo ya kisasa inahribu kila kitu,any way Mungu mwema ntafika tu huko na hii miaka yangu ya sasa
 
Wewe librarian au? Umeenda kwenye archives ukasoma! Unawezaje kutunza kopi ya gazeti kwa karibu miaka 50? Ikawa iko intact? Na utatunza Kopi ngapi? Haujazeeka kama wanavyotaka tuamini! Nyway....Topic yenyewe iko makini.
 
RC Walwa alikuwa na jeuri ya kumfukuza mzungu kwakuwa kiongozi mkuu wa nchi alikuwa na msimamo usioyumba katika masuala ya maslahi ya wananchi wake.
Jeshi la polisi lilikuwa na jeuri ya kutekeleza wajibu wao bila kusita kwakuwa lilikuwa linatambua wajibu wake na dhamana yake kwa wananchi. Jeshi la polisi lilikuwa halijachakachuliwa na kuwa vibaraka.

Sasahivi mkuu wa nchi kila siku kiguu na njia kutembeza bakuli kwa hao wazungu, hawezi kuthubutu hata kuwakemea achilia mbali kuwafukuza.

Wazungu wanalindwa na polisi wetu wenyewe na kuwatumia kuwanyanyasa wananchi na hata kufikia hatua ya kuua.

Wazungu wanabaka dada zetu kwenye balozi, migodini, mahotelini na kwingineko lakini viongozi wa serikali, si raisi, mkuu wa jeshi la polisi, RC ama DC anayethubutu kuchukua hatua.

Swali la kujiuliza hapa, kama enzi za mwalimu yeye na viongozi wenzake waliweza, hawa wa sasa wamepungukiwa na nini hadi wazungu wanatamba watakavyo?
Hivi kweli MWITA jibu la swali hilo hunalo??????? najua hii vunga tu!!!!!!
 
Angalizo: Tokeo hili lilichapishwa kwenye gazeti la Mwafrika 1962. Swali je hivi leo, ambapo viongozi wetu wanawakumbatia wawekezaji, kuna yeyote kati yao anayeweza kufikia maamuzi kama haya?

Mwafrika, Jumatatu Oktoba 29, 1962


MZUNGU mwingine ambae ni Meneja wa kampuni ya kuuza dawa, Arusha Bw. R. Bawley ameamriwa aihame Tanganyika, Mzungu huyo amepewa saa 48 tu kufanya hivyo.

Ripoti iliyopokelewa jana na gazeti hili ni kwamba Bwana Bawley alionekana akiondoka na matokaa kuelekea Kenya.

Sababu za kufukuzwa Mzungu huyo ni ufedhuli na kuwadharau Waafrika.

Mwandishi wetu akizungumza na na Regional Commissiner wa Jimbo la Kaskazini, Bwana P. Walwa jana alijulishwa kwamba jambo hilo alilihakikisha yeye mwenyewe alipofukuzwa na Meneja huyo.

Bwana Walwa alipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu ufedhuli wa meneja huyo. Watu wengine walisema kwamba huwafukuza watu dukani kwake au kuwatupia fedha wakinunua vitu.

Bwana Walwa alikwenda katika duka hilo ili ahakikishe mwenyewe kabla ya kuchukua hatua na kwenda kufika Bawley akamwambia 'nenda zako'.

Hapo Bwana Walwa alitoka na kutoa habari hizi kwa polisi.

Radhi yakataliwa:

Asubuhi yake Meneja huyo alikwenda kuomba radhi akisema hakujua kuwa yule aliyemfukuza alikuwa Regional Commssioner.

Bwana Walwa alikataa kumsamehe kwa sababu, alisema 'dharau ile ilifanyiwa Waafrika wote'.

Bwana Walwa alimwambia mwandishi wetu hiyo jana kwamba yeye alitembelea jimbo lote akiwaonya watu waheshimiane. Aliona si haki
wengine waachiwe kufanya dharau.

Bawley sasa ni Mzungu wa sita kuondolewa kwa visa kama hivyo tangu nchi hii ipate uhuru wake.

asante kwa taarifa za enzi hizooooo.leta na nyingine...
 
Mnaongelea ya zamani hivyo?
Hivi miaka ya juzi kati - mwanzoni mwa miaka ya 2000,
Mzungu wa KADCO alimkatalia waziri kutumia VIP Lounge KIA!
LOL....JEURI WANAYO HAWA WATU



Hata Mh. Ahmed Hassan Diria (rip) akiwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (awamu ya 2), aliwahi kupekuliwa kwa nguvu pale JNIA na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa kwa shirika lile la ndege.

 
Hongera mamaa wa Kericho kwa kuuteka mjadala wa mzungu na kuhamia kwako na umri wako binti mkongwe!

Nadhani kwakuwa umezaliwa na kukulia yaeda chini mnapokula vitu nachurale ndo maana unaendelea kudunda pamoja na kuwa na umri mkubwa kuliko Tanganyika huru.

Lakini siku hizi waarabu wamechukua eneo lenu la asili na mmetulia kama vile hamna kumbukumbu ya RC Walwa!
 
Back
Top Bottom