mzumbe university utata pesa za chakula second year

fatakifataki

Senior Member
Nov 2, 2009
134
60
ni jambo la kushangaza kuona, kuguswa ama kusikia kuwa hadi sasa wanafunzi wa mwaka wa pili hwajapatiwa pesa za chakula na bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
lakini uongozi wa chuo hicho umekuwa ukiona ni jambo la kawaida kabisa huku ukiwa umepanga tarehe ya kufungua chuo kuwa tarehe 19.10.2009 na wanafunzi hao wawe wameripoti chuoni kwa awamu nyingine ya masomo yaani new semester, jambo la kusikitisha ni kwamba wakati wanafunzi hao wakiripoti chuoni masomo yameanza motomoto huku kukiwa hakuna enforce yoyote ile ktk kuwapatia fedha za matumizi ya chakula. ila tunaambiwa kuwa kuna menejiment chuoni hapa, hii inawezekanaje? tunaweza kusema kuwa pengine njia za utatuaji matatizo ya wanafunzi vyuo vikuu ni nguvu ya hoja na sio kuendesha migomo kama ilivyopata kutokea siku za nyuma, lakini hapa mzumbe wanasifiwa si kwa dhati kwamba wao ni wana amani bali ni watu waliojawa na uchovu, chuki, na waliopoteza matumaini na utendaji mbovu wa taasisi ya mikopo ya elimu ya juu au hata pengine menejimenti ambayo ndio inayopaswa kuwajibika kwao kama mlezi. pengine sasa ni utamaduni wa miaka nenda rudi kuwa suluhu ya hoja na masuala ya msingi chuoni pale pengine kuchukuwa muda mrefu.
kilichobaki haijulikanai ni lini hawa vijana hali ya kuwa wazazi wanajua watoto wako chuoni wanaandaliwa kuwa kuwa watawala bora, jamani image ya chuo kikuu mzumbe iko wapi hapa? hebu waungwana tusaidieni maana hata mtawala akishindwa sijui mwalimi na madaktari na mainjinia watafanya nini ili wasigome.......
 
Back
Top Bottom