Mzee wa Upako: Rais Samia na viongozi wengine wa juu wa Serikali, acheni chokochoko kwa wananchi

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,197
Moja kati ya viongozi matata wa madhehebu ya Kikristo anayeitwa Mzee wa upako aliwahi kuyasema haya mwaka mmoja uliopita.

Viongozi wetu ambao wako kwenye nafasi ya kutuamulia "kesho yetu", wanapaswa kufuata ushauri wa Mchungaji Mzee wa upako.

Wasifanye maamuzi kwa kuongozwa na utashi wao tu, bali kwa kufuata ushauri wa wale wanaowaongoza kwa sababu hata hivyo wako pale kwa niaba yetu wananchi. Kwa maneno mengine, wananchi ndo wanapaswa kuwa na sauti ya mwisho ya maamuzi kwa sababu ndo waajiri wa viongozi hao.

Vinginevyo, viongozi wakiendelea kuwapuuza wananchi kwa kufanya maamuzi ambayo mengi ni ya kuwakandamiza na kuwaumiza, hufikia hatua watu wanaichoka serikali yao na kuamua kufanya kila linalowezekana kuiondoa madarakani kwa namna yoyote.

Ni wazi huu mkataba kati ya serikali na DP World, wananchi wengi wameonesha kuwa na mashaka na kutokukubaliana nao. Hivyo ni busara kwa serikali kuachana nao na kutafuta mwekezaji/wawekezaji wengine, tena ikipendeza wale wa ndani wapewe kipaumbele. Mbona tunao wafanyabiashara wakubwa wengi tu hapa kwetu, kama vile Mohamed Dewji, Said Bakhresa, Rostam Aziz n.k.?!

Tangazeni tenda kwa wazawa kwanza, wakishindwa ndo tutafute huko nje.

Jengine, kama kuna ma-mikataba mengine yenye masharti kandamizi kama hili li-mkataba la DP World, basi fanyeni kuyaficha hivyo hivyo ili yasije kuzua taharuki na kutuingiza kwenye machafuko.

 
Back
Top Bottom