M-bongotz
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,734
- 405
Nimeangalia kupitia channel ten mkutano wa Bw. Antony Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako akiongea na waandishi wa habari juu ya mgomo wa madaktari, jamaa anaonekana kuitetea sana serikali na kuita Madaktari ni wauaji na kila aina ya majina machafu.,anapinga uanaharakati akidai ni uchanga wa fikra eti nchi haiwezi kuendeshwa na kelele za wanaharakati.,anasema kwamba madai ya Madaktari hayana tofauti na madai ya nyongeza ya posho za wabunge.,eti mbona wananchi hawapazi sauti zao kutaka madaktari wasiongezwe mishahara lakini wanagomea posho za wabunge.,akamalizia kwa kusema anaomba Mungu asiugue maana hataki kutibiwa na "wauaji" ambao hawana tofauti na wauaji wa Albino.
Mimi nadhani huyu jamaa aidha anatafuta cheap popularity au anatumiwa na Magamba au anajipendekeza kwa watawala...Ni mtazamo yangu tu.
Mimi nadhani huyu jamaa aidha anatafuta cheap popularity au anatumiwa na Magamba au anajipendekeza kwa watawala...Ni mtazamo yangu tu.