Mzee wa miaka 70 ashikiliwa na Polisi akituhumiwa kufanya utapeli na Maafisa wa NSSF

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii [NSSF] linamshikilia mtuhumiwa Pius Komba [70] mkazi wa Itigi Jijini Mbeya kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya utapeli na kughushi nyaraka mbalimbali.

Mtuhumiwa alikamatwa Januari 25, 2024 eneo la Retco Jijini katika msako wa pamoja uliofanywa na Jeshi la Polisi na Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii na kufanikiwa kumtia mbaroni kinara wa kuandaa nyaraka na mihuri bandia na kuwapa wanachama wa NSSF ili wapate mafao kinyume na sheria inayosimamia ulipwaji wa mafao.

Mtuhumiwa amekuwa akishirikiana na wanachama wa mfuko na baadhi ya maafisa rasilimali watu wa makampuni wanayofanyia kazi kufanya udanganyifu wa taarifa zinazohitajika ili kulipa mafao kwa mujibi wa sheria ya NSSF sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018 kifungu 72 (1) (a) (b)

Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vishoka/matapeli ambao wamekuwa wakiandaa nyaraka (barua za kuachishwa kazi) za kughushi ambazo hutengeneza na kuwapa wanachama wa mfuko kwenda kufungua madai kinyume na taratibu ambazo ziko wazi kuwa ili mwanachama apate mafao ni lazima awe ameachishwa kazi na anakidhi vigezo vilivyopo kwa mujibi wa sheria.
 
Mzee kaona vijana wa 30's wanashangaa kaamua aingie kambani mwenyewe.
Bila shaka huwa anachukua fungu la 10 mambo yakitiki.
 
Back
Top Bottom