Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameshindwa kutetea kiti chake cha uenyekiti ambapo amepata kura 28 za ndio na 48 za hapana kati ya kura zote katika uchaguzi uliofanyika leo Kibaha mkoani Pwani.

Hii ndiyo inaitwa "From Hero To Zero"

Siasa za mchangani ni aibu kubwa!
 
Kutoka kuwa PM mpaka kupigania mwenyekiti Wa kanda? Niko aibu sana ngoja aendelee kuaibika?
 
Ana tamaa sana huyu mzee. Chama kikampa heshima ya kumpitisha peke yake kugombea uenyekiti wa kanda ya pwani, bado akaona tamaa kuchukua form ya ku compete na mwenyekiti. kapata stahiki yake. Sasa akatulie katesh
 
Mbona hujamalizia kati ya kura zote 73 zilizopigwa!?
IMG_20191129_082640.jpeg
 
Habari .

Jana uchaguzi wa mwenyekiti chadema kanda ya Pwani umemalizika kwa kuacha simanzi na vilio kwa kigogo wa siasa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka 10 mfululizo Frederick Sumaye kubwagwa! Hii ni ajabu kubwa kwa sababu Sumaye alikuwa hana mpinzani lakini ameambulia kura nyingi za HAPANA!

Lakini ikumbukwe siku moja kabla ya uchaguzi wa kanda ya Pwani ,gazeti linalomilikiwa na Mbowe la Tanzania daima liliandika habari front page iliyosomeka SUMAYE KUMVAA MBOWE, habari ilikuwa na maana gani? ,wachambuzi wa siasa wanasema habari hii ilikuwa ni moja ya mbinu za Mbowe kuwashughulikia wale wote wanaotaka kuchukua uenyekiti wa chadema taifa, ndiyo maana imepelekea Sumaye kushindwa vibaya!!.

Ikumbukwe Mara baada ya matokeo ,Sumaye aliposimama kushukuru wanachama alisema wazi kuwa baada ya kuona habari ile kwenye gazeti alitabiri matokeo ya kushindwa kwake na akasema hizo figisu siyo afya kwa chama cha chadema.

Screenshot_20191129-093114.jpeg
 
Wewe huna akili timamu kichwani, yani ccm wana mgombea wao, halafu Chadema wana mgombea wao then wawaache wagombea wao wakupigiw kura wewe? Hivi watu wa Kigoma mbona mna tambo za kipuuzi sana? Who hell are you?
 
CCM ni vizuri muache unafiki, asingechukua fomu Sumaye mngesema hakuna demokrasia CHADEMA.

Sumaye angeshinda mngesema kapita bila kupingwa hivyo hakuna demokrasia.

Sasa ameshindwa badala msifie kuwa ndio demokrasia kuwa pamoja na umaarufu wake hakuchaguliwa ndio kwanza mnaanza kulalamika kuhusu Mbowe.

Alafu ambacho husemi ni kuwa hata makamu mwenyekiti Meya Isaya Mwita aliangushwa licha ya umaarufu wake. Hilo hamsemi ila Sumaye kisa kumvaa mbowe???

Tuacheni demokrasia ifanye kazi yake. Kama CCM hamjazoea watu kuchukua fomu za uenyekiti kumchallenge magufuli then mjifunze kwa CHADEMA.
 
Wewe huna akili timamu kichwani, yani ccm wana mgombea wao, halafu Chadema wana mgombea wao then wawaache wagombea wao wakupigiw kura wewe? Hivi watu wa Kigoma mbona mna tambo za kipuuzi sana? Who hell are you?
Unajuwa huwa wakirudi kwao wanasifiwa sana kuongea basi hata huku mjini wanadhani wote ni waha.
Niliambiwa sifa moja ya Muha wa Kigoma ni ubishi.
Anaweza kubishana na watu waliojaa behewa zima LA 3rd class toka Tabora had I Kigoma wote wakachoka yeye yupo tuu na hata maji ya kunywa hajaomba!
 
Sumaye amesema form ya uenyekiti anayo ingawa bado ajaijaza. Anafikiria akaichanechane au namna gani. Mi namshauri aijaze na airudishe. Aikiichana itakua 0 plus 0.
 
Naomba usemacho kiwe kweli. Siafiki kabisa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm na sitamsupport kwenye nafasi hiyo, ila siko tayari kuona nafasi hiyo inaangukia kwa mwanaccm yoyote. Maana inaeleweka fika Sumaye sio mwanaCHADEMA, bali ni mwanaccm aliyeko likizo huko CHADEMA.
Mi naona unaongozwa na chuki binafsi katika hili.
Ukiangalia kwa kina, chama chenyewe, utagundua wazi kua Cdm bila mh. Mbowe haijiwezi.

Mbowe ndiye ameijenga CDM, na kuweka rekodi kuliko binadamu yoyote yule.

Wewe unawakataa wana CCM lakini hapohapo Unaiunga mkono CCM katika kumkataa Mbowe asiwe mwenyekiti. Na CCM wanajua kua Mh.Mbowe ndiye Mwiba mkali kwa CCM. Mchungaji akipigwa Kondoo watatawanyika. Utaelewa tu. Muda ni Mwalimu Mzuri.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Wewe huna akili timamu kichwani, yani ccm wana mgombea wao, halafu Chadema wana mgombea wao then wawaache wagombea wao wakupigiw kura wewe? Hivi watu wa Kigoma mbona mna tambo za kipuuzi sana? Who hell are you?
Huyu Dogo tayari ni project ijayo. Wanaangalia namna ya kumtenfenezea Chama ili we kama akina Dovutwa
 
ukawa2020,
Kwakweli hapa CHADEMA wamekosea sana. Kama mgombea alikuwa peke yake kulikuwa na haja gani ya kupiga kura?? Alikuwa peke yake hakuwa na upinzani hivyo alipata bila kupingwa. Kama mnafanya hivi, mtaaminika VP kwa wananchi kuwa chama inafuata demokrasia?? Mngemwacha Sumaye awe mwenyekiti na angeendelea kugombea nafasi ya uenyekiti sanduku la kura ingeamua. Nafikiri kuna watu wamelupwa kufanya yote haya ili chama ionekane haifuati demokrasia. mmekosea sana na hakuna njia ya kuirekebisha. Mmeigawa chama
 
Back
Top Bottom