Mzee Morris Nyunyusa; Historia itamkumbuka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
1477103844089.jpg

Kwa miaka mingi tulikuwa tunasikia midundo ya ngoma kuashiria kuanza kwa taarifa ya habari kwenye redio ya Taifa/serikali RTD na baadae TBC! ilikuwa ni midundo maarufu sana na yeyote aliyeisikia hata kwa mbali alijua wazi huu ni wakati wa taarifa ya habari....kwa majonzi makubwa midundo hii haipo tena huko TBC

Midundo hii ni ufundi wa Mzee Morris Nyunyusa mlemavu wa macho aliyekuwa na kipaji cha ajabu cha kupiga ngoma 17 kwa wakati mmoja, na midundo hii ilihusisha ngoma zote hizi

Umahiri wake huu ulimfanya ajulikane ndani na nje ya nchi huku akipata mialiko mingi tu...! Mzee huyu alikuwa ni tunu ya Taifa kwenye sanaa. Ni miaka mingi imepita hakumbukwi popote hata pengine kwenye vyuo vyetu vya sanaa

INAUMA SANA lakini historia itamkumbuka celebrity huyu wa kipindi hicho Mzee Morris Nyunyusa na pengine kuna siku kazi zake zitatakumbukwa na kutengenezewa hakimiliki ili wale aliowaacha wafaidike nako
1477104491476.jpg
 
Vitu vinavyo relate na ngono ndiyo vinathaminiwa na KUPEWA kipaumbele tz

OVA
Angekuwa mwanasiasa angetunukiwa tuzo hata kama ametangulia mbele za haki. R. M. Kawawa alipewa kadigree kwenye mahafali ya kwanza ya UDOM kwa mchango wake wa ujenzi wa ukumbi wa Chimwaga ambapo chuo kilianza. Watu kama hawa hawakumbukwi kabisa.
Haaaaa Kabisa.
 
Mkuu Mshana vipi unaweza kuweka audio ya midundo yake. Tusiwe tunajaza nyimbo za wenzetu na kusahau tunu zetu.
 
Bad enough ndugu mshana jr michango yetu kwenye jamii inathaminiwa tu kwenye kusherehesha mikutano nashughuli za kisiasa na hukoma punde tu wale wanaotutumia wanapokamilisha malengo yao ama zama zao kupita. Umenena vyema kwamba watu hawa wenye michango yao kukuza sanaa wangekuwa nembo ya taifa na funzo kwa kizazi cha leo!
Leo hii kuna mtoto wa kileo anayemjua Basket Mouth,Klint da drank, Kansiime na kina Eric Omond kuliko hata mchekeshaji maarufu kutoka mtaa wanamoishi!
 
Shida ni kwamba Watunga sheria/Wapitisha hoja wa Tanzania (Wabunge) hata hamjui wala hwana kumbukumbu zozote juu yake Nyunyusa.
Kama mh. Mbunge anasema:
TANGANYIKA+ZIMBABWE=TANZANIA??!!!!!!!!!
 
Bad enough ndugu mshana jr michango yetu kwenye jamii inathaminiwa tu kwenye kusherehesha mikutano nashughuli za kisiasa na hukoma punde tu wale wanaotutumia wanapokamilisha malengo yao ama zama zao kupita. Umenena vyema kwamba watu hawa wenye michango yao kukuza sanaa wangekuwa nembo ya taifa na funzo kwa kizazi cha leo!
Leo hii kuna mtoto wa kileo anayemjua Basket Mouth,Klint da drank, Kansiime na kina Eric Omond kuliko hata mchekeshaji maarufu kutoka mtaa wanamoishi!
Pathetic
 
Back
Top Bottom