Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
MUULIZAJI KAULIZA KWA NINI SYKES WANAREJEWA NA KUREJEWA?
''Nauliza hakuna familia nyengine ila ya akina sykes ilo shiriki?
Kugomboa tanganyika naona kila mara tunawarejea hao hao?''
Namjibu:
NYARAKA ZA SYKES KATIKA HISTORIA YA TANGANYIKA
Siku nilipofunguliwa sefu iliyokuwa na nyaraka za Sykes nilipata mshtuko mkubwa usio na kifani.
Historia ya mimi kufikia hapo ni ndefu atakae kuijua inabidi asome kitabu cha Abdul Sykes.
Kwa ufupi nyaraka na kumbukumbu nyingine zinarudi nyuma hadi 1890s.
Ilikuwa kama vile narudi kinyumenyume katika historia.
Nikapewa taarifa kuwa nyaraka hizi zilikataliwa kuwa sehemu ya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika mwaka 1962.
Matokeo yake ikawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ikawa inasomeshwa bila ya mchango wa akina Sykes.
Baada ya miaka mingi historia hii ikapotea.
1998 nikaandika kitabu kilichochapwa London.
Kitabu hiki kilipindua historia iliyokuwapo.
Kitabu kikatiwa katika Cambridge Journal of African History.
Hapa nyumbani kitabu kikasababisha taharuki kubwa.
Waliosoma kitabu wakauliza iweje mipango ya ukombozi iwe toka 1929 na iliasisiwa na Kleist Sykes na kundi la vijana wa mjini akina Mzee bin Sudi lakini historia imewafuta?
Waliposoma historia ya Abdul Sykes hali ikawa mbaya zaidi.
Prof. Haroub Othman akamkabili Mwalimu na hoja kuwa lazima na yeye Mwalimu aeleze historia yake kwa kuwa tayari historia ya Tanganyika imepata mashujaa wengine.
Bahati mbaya Waislam ndiyo wakawa wametawala historia ya ukombozi wa Tanganyika.
Mjadala huu umetawala mitandao ya kijamii na kila FM Station, Online TV na AZAM TV, TBC 1 wamenihoji si mara moja.
Pandora's Box imefunguka.
Hakika ni historia ya kipekee ukisoma mswada alioacha Kleist Sykes kabla hajafa 1949 anavyoeleza uhusiano wa jeshi la Wazulu lililoingia Tanganyika likiongozwa na Hermann von Wissmann.
Mswada huu uko Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam toka 1968.
Vita na Abushiri na Mkwawa.
WW I watoto wa hawa Wazulu wanapigana na Waingereza chini ya von Lettow Vorbeck 1914 - 1918.
Wajukuu wanapigana na Wajerumani WW II KAR Burma Infantry 1939 - 1945.
1950 Abdul Sykes na Kenyatta Nairobi mipango ya kupambana na Waingereza.
Yote haya kwa ushahidi wa nyaraka nyingine kutoka Rhodes House Oxford.
1953 Abdul Sykes anamuweka Nyerere madarakani.
1954 wanaunda TANU.
1955 Nyerere anaacha kazi anakwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes.
Tanganyika hii hakuna ukoo wenye historia kama hii.
Kila siku mimi ni kuulizwa maswali kuhusu historia hii.
Na kila siku napata wanafunzi wapya.
Kitabu kinakwenda sasa toleo la 5.
Mwaka wa 2011 nilimzungumza Abdul Sykes Northwestern University, Evanston, Chicago, Illinois katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.
Hiki ndicho chuo kinaongoza ulimwengu mzima katika African History.
Mhadhara wa kwanza ulikuwa University of Iowa, Iowa City.
Baada ya hapo nikamzungumza Abdul Sykes Zentrum Moderner Orient, Berlin.
Hii ni taasisi kubwa Ujerumani katika utafiti wa historia.
Nilitoa paper: "Tanzania A Nation Without Heroes."
Namshukuru Allah.
Nakushukuru sana ndugu yangu kwa swali hili kwani bila ya kupata changamoto ubongo una kawaida ya kusinzia.
Nitatumia hizi ''notes'' hapa In Shaa Allah kuwasomesha wanafunzi wangu wapya.
Historia ya Kleist Sykes ipo katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, New York 2011.
HIstoria ya Kleist Sykes ipo katika kitabu hicho hapo chini ''Modern Tanzainians,'' East African Publishing House, 1973.