Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Mtu mzima akikosa usingizi,utulivu na umakini na kutumia muda na gharama kubwa sana kushughulika na mtu anayeamini ni mpumbavu na lofa tena kwa jazba basi ujue mtu huyo ndiye Mpumbavu na lofa namba moja duniani.

Mzee anazeeka vibaya huyo! Nafikiri ameonja viroba msikilizeni vizuri. MABADILIKO ni lazima yaje. KUNAKUCHA uwike na hata usipowika, asubuhi ipo karibu, MUNGU ni Mkuu!
 
Pole kwa Watanzania kuelewa isivyo kauli "upumbavu na ulofa". Nami mwanzo nilielewa kama maneno hayo ni matus. Lakini maana halisi ya "mpumbavu" ni mtu asiyetumia busara katika maamuzi yake. Mara nyingi ni watu ambao hufuata upepo. Kwa mfano katika hali ambayo mtu anapita kuomba udhamini wa kutaka uongozi, watu badala ya kuendelea na shughuli zao za maisha wanakesha kumsubiri na hata kudiriki kuingia uwanja wa ndege au kupiga deki barabara, hakuna jina linalowafaa hawa watu zaidi ya "upumbavu". Mbaya zaidi ya aina hii ya watu kwa kufanya matendo kama hayo ni katika hali inayoonyesha si tu ufinyu wa fikra ila ni dalili tosha wamefirisika kimawazo. Neno sahihi ni "ulofa". Tujitahidi kutunza heshima na utu wa kibinadamu kwa fikara kutawala matendo.

Umemaanisha hata waliokuwa jangwani Jana ni wapumbavu malofa plus,kweli tuna haja ya kuondoa ccm fasta.
 
Rafiki yangu mmoja akasema "Mkuu wa Malofa ni Lodi Lofa". Basi kama huyu jamaa aliyewaita Watanzania "Malofa" alishakuwa rais wa hao Malofa, yeye mwenyewe ndiye Lodi Lofa, a.k.a. "LordLofa". Kwa wale mlowahi kusoma gazeti la Sani, basi mnazielewa tabia za Lodi Lofa. Hilo la "Wapumbavu" mtalitafuta wenyewe. Sina mengi ya kusema

Wenu Lofa mdogo
 
Wahenga walisema "ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo!" Katika siasa za kistaarabu na kiungwana sikutegemea Mh. Mkapa (Rais mstaafu wa awamu ya tatu) kuporomosha matusi ya kejeli kwa vyama vya upinzani kama alivyofanya jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi! Matusi aliyoyatoa mh. mkapa yanamdhalilisha yeye mwenyewe kama kiongozi wa ngazi za juu mstaafu, yanadhalilisha utu na yanavunja haki ya msingi ya mtanzania kuchagua chama anachokiamini kuwa kinaweza kumletea maendeleo ktk nchii ya Tanzania. Ina maana kwamba vyama vyenye mawazo mbadala pamoja na wafuasi wake ni wapumbavu na malofa! Hiyo ni kweli na haki?

Naomba wana jamvi mnisaidie pengine huyu mheshimiwa alikasirishwa na:

1. Kuhama kwa watu muhimu (mh. Lowasa, Mh. Sumaye n.k) toka CCM na kwenda ukawa,
2. Vyama vya upinzani kuimarika kutokana na umoja wa UKAWA na hivyo kuwa tishio kwa mgombea urais wa CCM,
3. Alikuwa kaweka whisk kiana akasosa control ya kuongea?

Na kama ndivyo hiyo solution ya kupunguza nguvu ya upinzani? Tuanze kufikiria kuandoa kinga ya kutokushitakiwa ya hawa marais wstaafu maana wanaitumia vibaya!
 
Mkapa anamuogopa na anamchukia sana Edward
Lowasa kwani baada ya kuwa waziri
mkuu alianza kupitia upya mikataba ya
madini iliyosainiwa na serikali ya Mkapa na alirudisha mgodi wa kiwira
kwenye serikali.
Mgodi huo mkapa alijiuzia tsh milioni
moja tu alipokuwa raisi na alishindwa kuuendeleza
kabisa.
Pia mkapa na magufuli walijiuzia
nyumba za serikali kwa bei powa na
mchakato uliogubikwa rushwa na usiri
mkubwa.
Baada ya Rowasa kuanza kufatilia
maswala hayo Kikwete ilifikia hatua ya
kumtetea mkapa kwa kusema
"MWACHENI MZEE WA WATU
APUMZIKE".
NA baadae wakafanikiwa kumtoa
madarakani lowasa kwa kumpakazia
skendo ya richmond.
Ikumbukwe baada ya Lowassa
kutolewa madarakani aliingizwa waziri
mkuu Mizengo pinda Ambaye alifanya
kazi muda mrefu na mkapa na Mkapa
ndiye aliyemshawishi Pinda aingie
kwenye siasa na kumpendekeza kuwa
awe waziri mkuu.
Pia waliingizwa maswaiba wengi wa
mkapa CCM kama mangula.
Tofauti na lowassa aliyeondolewa kwa kasfa moja, Mizengo Pinda alipitia
kadhia nyingi sana kama;
1. Hongo kwa wabunge ya wizara ya
nisharti na madini ili wapitishe bajeti iliyomuondoa ktibu wa wizara hiyo.
2. Operation Tokomeza
3 Ubadhilifu na matumizi mabaya ya
fedha kutokana na mkaguzi mkuu wa
serikali.
4. Kashfa kubwa zaidi ya Wizi wa fedha za Escrow Ac.
lakini kikwete alimkingia kifua asiguswe au kuondolewa
**(mada hii haihusiani na hotuba ya jana ya mkapa ambayo sikuisikiliza)**
 
Daaah umati ule ulimdanganya mara zote unapokuwa kwenye umati wa watu wengi neno lolote linalokuja mbele yako unatamka tu madhala yake utayaona baadaye UKAWA Watakapotumia Gia ya kwamba Mkapa aliwatukana lakini adhabu yake muadhibuni kwenye kizimba cha kupigia kura. Sasa hapo ndio utaona impact ya kauli za ajabuajabu.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Kauli ya jana aliyoitoa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa kuwa wanaosema kuwa wanataka kuikomboa Tanzania ni malofa na wapumbavu inaendelea kuleta mijadala kwenye mitandao ya kijamii. Wapo wanaosema kuwa Mkapa amewatukana wapinzani wote kwa kudai kuwa wanataka kuikomboa Tanzania.

Binafsi nimesoma michango ya wadau wengi kwenye mitandao ya kijamii. Hakika nimebaini mambo mawili.

1. Baadhi ya wafuasi wa UKAWA hawakuelewa nini Mkapa alimaanisha. Hii ni kwa sababu wafuasi hao wanalishwa tu maneno kuwa Tanzania nahitajimkukombolewa lakini hawajui ni ukombozi wa aina gani. Mkapa alikuwa specific. Kwamba, Tanzania ilishakombolewa na TANU na ASP na ukombozi huo umekuja kuboreshwa na CCM. Hata nchi za kusini mwa Afrika zinajua kuwa Chama cha Ukombozi Tanzania ni CCM. Hii ni kusema kuwa chama chenye nembo (brand) ya Ukombozi Tanzania ni CCM.

Hivyo kama UKAWA wana hoja ya kuthibitisha kuwa wao ni wakombozi waziweke bayana badala ya kusema jumla jumla kuwa wanataka kuwakomboa Watanzania ilhali Tanzania ilishakombolewa kutoka kwenye makucha ya adui Mkoloni na sasa inaendelea kukumbolewa na CCM kutokana na maadui watatu ambao ni Maradhi, Ujinga na Umaskini maadui ambao walitangazwa na Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

2. Kauli ya Mkapa wnataka kuitumia UKAWA kupata huruma ya Wananchi. Ijapokuwa Mkapa alikuwa specific kwa wale tu wanaosema kuwa wanataka kuikomboa nchi, UKAWA wamedandia hoja hiyo ili tu wahurumiwe na wananchi. Sasa wanasambaza propaganda kuwa Mkapa kawatukana wananchi wote kitu ambacho si sahihi. Hizi zinaitwa siasa nyepesi.

Ninachokiona hapa ni kwamba UKAWA wamepanic kutokana na ile Tsunami ya jana na umahiri wa Magufuli kunadi sera za CCM. UKAWA hawana pa kuponea. Mgombea wao hana uwezo wa kuongea hata kwa muda wa nusu saa na mpaka sasa hawana hoja za kuomba kura kwa wananchi. Hivyo wanataka kutumia kauli ya Mkapa kama ndo sera yao ya kuomba kura kwa wananchi.

Nimalizie kwa kusema kuwa Watanzania wanajua kizuri na kibaya. Magufuli ndiye chaguo lao kwa vile amepata baraka na Mungu. Huyo anayeendelea kumwaga fedha kwa lengo tu awe Rais hakika amekataliwa na ataendelea kukataliwa. Uchongaishi wenu kwa mkapa hautawasaidia. Pia mtambue kuwa mgombea si Mkapa wala Kikwete bali ni John Pombe Magufuli. Kama mna hoja za kupambana naye tumieni majukwaa haya kumnadi mgombea wenu badala ya kuendelea kulalamika kwa kuambiwa ukweli.
 
Kama jana kulikuwa na matusi, basi JF sasa hivi imesheeni matusi kuliko ya upumbavu na ulofa! Oktoba mbali wabaki ma GT kama zamani!
 
Back
Top Bottom