Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

nchi hii ilishakombolewa na wazee wetu wakiongozwa na mw. nyerere miaka dahali iliopita sasa anakuja mtu anasema anataka kutukomboa ni ukosefu wa akili tena narudia mpumbavu mkubwa
ukawa ni wafinyu wa uelewa wote ni kama waumwa parkinsons aliyeambiwa mpumbavu jana alikuwa sumaye kwa sababu mkapa alimuamini kwa miaka kumi kama waziri mkuu.

na sumaye mwenyewe wakati akitamka kutia nia ya kuutaka urais kupitia ccm alisema wakimpitisha fisadi lowasa yeye atahama ccm sasa kulikoni kala matapishi yake kama sio upumbavu?
 
Rafiki yangu mmoja akasema "Mkuu wa Malofa ni Lodi Lofa". Basi kama huyu jamaa aliyewaita Watanzania "Malofa" alishakuwa rais wa hao Malofa, yeye mwenyewe ndiye Lodi Lofa, a.k.a. "LordLofa". Kwa wale mlowahi kusoma gazeti la Sani, basi mnazielewa tabia za Lodi Lofa. Hilo la "Wapumbavu" mtalitafuta wenyewe. Sina mengi ya kusema

Wenu Lofa mdogo

Aliposema neno malofa ikaja ile picha ya Lodi lofa nikamwona lofa mkuu alivyofanana na lofa wa gazeti la sani,tofauti ilikuwa kofia tu! Hakika nyani haoni kundule!!
 
lazima tuwe malofa na wapumbavu tulimuweka juu yetu na kumheshimu kwa woga kwa miaka 10,hizi ndio fikra za viongozi na taasisi ya ccm kuwa nawanchi ni wajinga,miaka 50 ni mingi sana kuwa madarakani lazima uone watu ni wapumbvu tu na kiukweli hasa ni ushabiki wa kipumbavu kuendelea kuipiga kura ccm,tusifananishe ushabiki wa mpira(yanga na simba) na ushabiki wa siasa,siasa zinaathiri maisha yetu moja kwa moja,hapa wapumbavu na malofa ni watanzania wote walio ccm na wapinzani,wanaccm hawatakiwi kufurahia kauli hii wanatakiwa kuzishinda nafsi zao na kuweka hawa nje kwa kipindi ili kutoa somo na kuimarisha tz
 
Aliposema neno malofa ikaja ile picha ya Lodi lofa nikamwona lofa mkuu alivyofanana na lofa wa gazeti la sani,tofauti ilikuwa kofia tu! Hakika nyani haoni kundule!!

Ila siku zinaenda jamani,mkapa amezeeka!
Yani kama sio kufoka matusi,wala huwezi kumtambua!
Utajua labda mtu kakosea sehemu ya kukaa
 
Wataalamu wa Sheria na Ustawi wa Jamii naomba mwongozo.Jana nilikuwa naangalia mkutano wa CCM na Binti yangu wa miaka 5. Katika malezi yake yake huwa tunamwongoza asitumie lugha ya matusi ,kejeli kuwa ni dhambi .Na wanaotumia lugha hiyo ni watu wa shetani ! Sasa jana wakati Rais Mstaafu akitokwa na povu na ile mitusi binti yangu alimpata vizuri sana .Huyu binti anawajua wanasiasa wa Tanzania Kuanzia Nyerere ,Mkapa na JK ,na sasa Pombe(ndivyo anavyopenda kumuita) na Lowasa ...amabaye kwake ni kila kitu! Na anawachukulia kama role modal wake ! Jana amefadhaishwa sana na Kkitendo cha Mkapa kutukana hadharani ! Na ameniambaia kuwa kwa kuwa Mkapa amelitumia neno hilo basi ni neno halalai na yeye ataanza kulitumia. Sasa sijui atatnza lini/
Kabla hajaanza naomba niombe Mwongozo wa Wataalmu je nina weza kumshtaki Rais Mstaafu kuwa ameniharibia bINTI YANGU KWA KUTUMIA LUGHA YA MATUSI ? SHERIA YA MTOTO INASEMAJE KATIAK KADHIA HII!
 
Kwa kuwa wanaotaka mabadiliko nu wapumbavu na malofa hivyo hakuna mabadiliko yanayoweza kuletwa.

Mh.mkapa hajui hata historia ya nchi yetu.

Anasema"Ukienda kote kusini mqa Afrika ukauliza chama cha ukombozi Tanzania utaambiwa ccm"
Je nchi yetu iliyopata uhuru ni Tanzania au Tanganyika?
Je chama cha ukombozi kilikuwa ni Tanu au Ccm?

Yawezekana kutojua historia yetu ndiko kulikopelekea ashindwe kutuongoza vizuri maana alikuwa hata hajui anaongoza nchi gani?
 
Hii nchi imesha kombolewa tayari na TANU na ASP hawa wakombozi wa saivi wanakomboa nini..NI WAPUMBAVU tena MALOFA
 
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!

hakuna kitu nachokiogopa kama uzee manake unakuja na mambo mengi kweli ambayo wakati mwingine yanakufanya uonekane kituko mbele za jamii.ukiangalia kwenye red,mtu huyo huyo anasema nchi ilishakombolewa na mtu huyo huyo anasema kuna ukombozi unaendelea.

kweli lowasa kawachanganyia watu madawa,kiasi kwamba hata hawajitambui
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu mzee alikuwa rais????.
Tume ya taifa ya uchaguzi isipo muonya hadharani nita kuwa na wasiwasinayo sana.
Kauli hizi za matusi ndio zinasababisha jazba kwa watu wasio jua kupuuzia mambo na zinaweza kuleta madhara.

Namshauri asipanic atulize akiliyake anapokuwa anaongea iliabaki na heshima yake kama rais mstaafu.
 
Wataalamu wa Sheria na Ustawi wa Jamii naomba mwongozo.Jana nilikuwa naangalia mkutano wa CCM na Binti yangu wa miaka 5. Katika malezi yake yake huwa tunamwongoza asitumie lugha ya matusi ,kejeli kuwa ni dhambi .Na wanaotumia lugha hiyo ni watu wa shetani ! Sasa jana wakati Rais Mstaafu akitokwa na povu na ile mitusi binti yangu alimpata vizuri sana .Huyu binti anawajua wanasiasa wa Tanzania Kuanzia Nyerere ,Mkapa na JK ,na sasa Pombe(ndivyo anavyopenda kumuita) na Lowasa ...amabaye kwake ni kila kitu! Na anawachukulia kama role modal wake ! Jana amefadhaishwa sana na Kkitendo cha Mkapa kutukana hadharani ! Na ameniambaia kuwa kwa kuwa Mkapa amelitumia neno hilo basi ni neno halalai na yeye ataanza kulitumia. Sasa sijui atatnza lini/
Kabla hajaanza naomba niombe Mwongozo wa Wataalmu je nina weza kumshtaki Rais Mstaafu kuwa ameniharibia bINTI YANGU KWA KUTUMIA LUGHA YA MATUSI ? SHERIA YA MTOTO INASEMAJE KATIAK KADHIA HII!

mkuu hiyo picha kwenye avatar yako ndio malezi mazuri? sio kuwa nawewe unamdhalilisha huyo binti hapo, sioni tofauti yako na mkapa, na huenda wewe ndo
 
Mpumbavu maana yake ni mtu mwenye uelewa mdogo kuhusu jambo Fulani.Kabla ya kukurupuka na kupost malalamiko kuhusu usichokijua ni bora ungejibidisha kwa kutumia smartphone yako kutafuta maana ya "Neno Mpumbavu".......kama alivyosema mkapa inawezekana tupo wengi sana mitaani...
 
bINTI YANGU HAJAPITIWA NA HAYA MAGONJWA YA MITANDAO ...NAMDHALILISHA VIPI...HATA MAMA YAKE HANIJUI KAMA NIPO HIVI KWA JAMII FORUM
mkuu hiyo picha kwenye avatar yako ndio malezi mazuri? sio kuwa nawewe unamdhalilisha huyo binti hapo, sioni tofauti yako na mkapa, na huenda wewe ndo
 
Sasa nahisi na wewe ni mpumbavu ...hiyo tafsiri umeitoa kwenye lugha gani .acha kukurupuka kumbuka tunamwongelea mtoto ! We nawe ....
mpumbavu maana yake ni mtu mwenye uelewa mdogo kuhusu jambo fulani.kabla ya kukurupuka na kupost malalamiko kuhusu usichokijua ni bora ungejibidisha kwa kutumia smartphone yako kutafuta maana ya "neno mpumbavu".......kama alivyosema mkapa inawezekana tupo wengi sana mitaani...
 
ukawa ni wafinyu wa uelewa wote ni kama waumwa parkinsons aliyeambiwa mpumbavu jana alikuwa sumaye kwa sababu mkapa alimuamini kwa miaka kumi kama waziri mkuu.

na sumaye mwenyewe wakati akitamka kutia nia ya kuutaka urais kupitia ccm alisema wakimpitisha fisadi lowasa yeye atahama ccm sasa kulikoni kala matapishi yake kama sio upumbavu?

Si heri na parkinsons kuliko wale wanaoingizwa mipira na mabomba njia za kutolea makapi ya chakula. Mie mzungu hawezi nigusa sehemu hizo aisee.
 
Jamani sisi “wapumbavu/fu malofa” tuwaulize Mkapa na CCM yao watupe majibu yafuatayo ili ikiwezekana tubainishe mpumbavu na lofa ni nani:-

Maana na uhalisia wa mpumbavu/fu ni asiyefundishika, asiye na busara

1. Mwalimu J. K. Nyerere aliondokea uwanja wa ndege akitembea kwa miguu yake bila msaada wa mkongojo kwa ajili ya kupima afya yake uingereza(kwa busara za Mkapa). Karudi kwenye sanduku tukamzika.
2. Wiki mbili baada ya mazishi ya Mwl NBC ikabinafsishwa
3. Ubinafishaji ukakumba mashirika ya umma vikiwepo viwandanzadi ya 400. Ubinafishaji ulihusisha mali zisizohamishika kama ndiyo hatua ya kwanza. Nyumba za shirika la posta tuwaulize familia ya Mkapa na akina Lukuwi kujiuzia hapo kuna busara.
4. Nyumba za serikali zikauzwa na serikali ya Mkapa chini ya usimamizi yaw a Magufuli. Naomba msomaji jiridhishe mwenyewe kuwa vile viwawanja vya nyumba zile hivi sasa wako kina nani pamoja na sheria kutaka visibadilishwe matumizi mpaka baada ya miaka 25. Watumishi wa serikali wakiwepo mawaziri wanapanga mahotelini kwa zaidi ya gharama za kukarabati hizo nyumba hata kujenga nyumba mpya kwenye viwanja hivyo. Hayo tunaambiwa ni maamuzi ya busara.

Maana ya neon lofa ni mtu zaidi ya masikini ambaye hata ukimpa mtaji mkubwa wa namna yo yote hataweza kuufanyia cho chote. Kifupi ni masikini wa mali na akili. Nawakumbusha huyu huyu Mkapa alipoanzisha msamiati wa wivu wa kike. Alikuwa na wazee wenzie na mawaziri wake wanakandia watu kupigia kelele wizi na ufisadi unaowatajirisha Mkapa na wale wateule wa CCM kuwa watu hawana akiuli na uwezo wa kutajirika wanabakia na wivu wa kike. Kumbe sababu ni kukosa mitaji na maarifa ndiyo inayo sababisha wao wateule wameatamia fursa zote za ujasiliamali. Huo nao ni ulofa wa kufikiri kama vile kuishi kwenye nyumba ya vioo katikati ya Uswazi.
Kifupi kuna yafuatayo

Awamu ya pili walihakikisha wanaua kabisa mfumo wa utendaji wa serikali na kuifanya serikali kuwa tawi la CCM. Hupewi uongozi wa namna yo yote kwa sifa za kitaalamu bali sifa ya CCM. Mtakumbuka siasa ilpoanza kuwa dili kupita uprofesa.

Awamu ya tatu ilikuja na mageuzi ya kiuchumi Mkapa na CCM watumia mageuzi ya uchumi kitaifa kuwa yao binafsi. Huo ndio ubinafsishaji.

Awamu ya nne ilikuja kwa kauli za kitaarabu elimu na huduma za kijamii ikaporomka uchumi wa mtu binafsi ndani ya wateule ukapaa uchumi wa mapumbavu/fu na malofa ukawa afadhali ya jana siku zilivyosaonga. Mikataba ya siri, kuuawa tembo na wanamageuzi hasa waandishi.

Bahati upinzani ukawa unajikongoja ukakurupusha hadidu za rejea za katiba na utendaji wa serikali. Wateule wakatunisha misuli hakuna cha katiba mpya wala utekelezaji wa maazimio ya bunge. Hizo nazo ni busara.

CCM wamekwenda kwenye kura za watia nia kumpata Magufuli mtendaji mzuri anatekeleza maamuzi ya wateule (Usisau uuzwaji wa nyumba ndio utendaji mzuri wa Magufuli lakini alitumia akili au akili yake alishikiliwa na wateule).
Wanaingia kwenye uchaguzi huu kwa ahadi siyo kwa sera kwa maana halisi ya sera, na sera ya kutukana wasiokubaliana nao.

Mahitaji ya baadhi yetu watanzania.

1. Ni uongozi unaoweza kutoa maamuzi na kuyasimamia. Si utendaji unaotekeleza maamuzi yenye ukakasi.
2. Maono ya miaka 50 ya Tanzania inayowakumbatia wananchi wake wakinufaika sawa na reasilimali na fursa za uchumi na kijamii.
3. Watanzania wenye kujitambua kwa kuwa na elimu ya kuchabua mambo na majasiri wa kuhoji uongozi mbovu. Hii ni pamoja na kuilewa katiba ya nchi ambayo inakidhi na kutokana na maoni yao.

Kwa kuitwa wapumbavu na malofa tumetngwa na kubaguliwa maana ni jumla jumla. Kwa hali hiyo wateule wamejitenga nasi hatuna namna yo yote ya kujinasibu nao. TUMIA KURA YAKO KWA BUSARA UACHANE NA UPUMBAFU NA ULOFA
 
Mimi naona tusipoteze muda na Mkapa,tuendelee uwasiliana na ndugu zetu vijijini na kuwaeleimisha kuhusu kutunza shahada ya kupiga kura na kulinda kura.Na pia kuwasilisha matokeo kwenye kata zao mara wakitoa matoke.PIGA SIMU SASA HIVI KWA KAKA YAKO,BABA YAKO,MAMA YAKO,MJOMBA WAKO.NA WAO WAWAELEZE MARAFIKI ZAO.Hatuta bahatisha sasa hivi.Ukiweza kutuma text msg 100 kwa week.Utakuwa umefanya vizuri sana
 
Kwani mini maana at kukomboa ina wezekana hats mkapa hajui maana yake amekurupuka si unajua tena
 
mimi mpumbavu na lofa kwa sababu nahitaji ukombozi wa kweli?!!!Mungu nisaidie niione october25 nikiwa na afya njema ili nami nionyeshe upumbavu wangu kwa hiki chama cha CCM.kweli ccm mnatuita sisi malofa wakati nyie ndo mmesababisha tuwe malofa kwa miaka zaidi ya 54?sawa mim lofa...
 
Back
Top Bottom