Mzee Kawawa afariki dunia!

Tribute to Kawawa, ambaye hukuwa kama hawa,
wanaofanya vitu bila kufuata usawa,

they say the good die young,
but you lived long to teach the old and the young,
to imancipate themselves from doing wrong,
today we sing you a song.

RIP our lion, our icon, our inspiration, our companion!
 
Kikawaida kulingana na maandiko umri wa binadamu kuishi ni miaka 70, kwa huyu Mzee wetu nadhani amefariki akiwa na 83, sio mbaya tumshukuru Mungu kwa kumuweka hadi leo hii, yeye ndiye mtoaji na ndiye anayetoa pale anapoamua. Sisi ni mavumbi tu

RIP
 
R.I.P Simba wa Vita na Muasisi/Mwanaharakati wa uhuru wa Tanganyika Rashid Mfaume Kawawa.Daima tutakukumbuka kwa utumishi uliotukuka kwa Taifa letu ukiwa Waziri mkuu,Makamu wa pili wa Rais,Waziri wa Ulinzi na JKT,Makamu mwenyekiti na Katibu mkuu wa CCM..Hakika tutakukumbuka baba yetu mpendwa..Umeondoka katika kipindi ambacho Taifa letu linahitaji sana Hekima na busara zako,tulikutegemea sana kwa ushauri mara tunapokwama(kama Taifa)..Salamu kwa Baba wa Taifa na mama yetu Sophia..Raha ya milele umpe e bwana,na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa AMANI
 
Kumaliza mwaka ni jambo ZITO sana. MUNGU ashukuriwe, maana ndiye mwenye uwezo wa kupanga na kupangua. Sote tuombe Mungu.. Mengine zaidi baadaye... INASIKITISHA

Muasisi wa chama cha TANU, Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, Simba wa Vita na mchapa kazi.

Kalale pema peponi.....KAMANDA - I SALUTE YOU COMREAD.
 
RIP RASHIDI!.

Halisi/Mode, kwa kuanzia kama JF initial Tribute ya Mzee Kawawa, nashauri ile profile ya Mzee Mwanakijiji kuhusu iwekwe chini ya tangazo la Halisi, kama inawezekana Halisi aiweke mwenyewe, ama mode ili kila atakalog kutoa pole apate zaidi kidogo.

Asante Halisi kwa hii ya ukweli sasa. Asante Invicible kwa angalizo la jana kuhusu afya yake na asante Mzee Mwanakijiji kwa profile yake, young generation wasiojua haya ni wengi kuliko sisi old guards.

He was the most humble in times of Mwalimu.

Pole sana Zamaradi na familia nzima ya Mzee Wetu, Shujaa Wetu, Kipenzi Chetu na Mwenzetu Simba wa Vita.

RIP RASHIDI!.
 
Wakuu habari za kusikitisha zilizothibitishwa punde tu ni kuwa mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa Amefariki dunia leo,mwenye data kamili atuhabarishe zaidi.
 
Sio jana tu walikuwa wanakanusha? Tanzania bado kuna vijitu vijinga sana.

RIP aka Wakawaka.
 
Mungu amlaze pema Rashid Mfaume Kawawa!

Mzee Rashid ameaga dunia akiwa mwadilifu hakuwa FISADI amefariki akiwa hajajilimbikizia mali pamoja na kushika nyadhifa kubwa!
Sidahani kama kuna kiongozi wa wakati huu ataweza kufikia uadilifu wa Mzee Kawawa .
 
R.I.P Simba wa Vita na Muasisi/Mwanaharakati wa uhuru wa Tanganyika Rashid Mfaume Kawawa.Daima tutakukumbuka kwa utumishi uliotukuka kwa Taifa letu ukiwa Waziri mkuu,Makamu wa pili wa Rais,Waziri wa Ulinzi na JKT,Makamu mwenyekiti na Katibu mkuu wa CCM..Hakika tutakukumbuka baba yetu mpendwa..Umeondoka katika kipindi ambacho Taifa letu linahitaji sana Hekima na busara zako,tulikutegemea sana kwa ushauri mara tunapokwama(kama Taifa)..Salamu kwa Baba wa Taifa na mama yetu Sophia..Raha ya milele umpe e bwana,na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa AMANI

Mkuu pia umesahau afikishe salaam zetu wa Waziri wetu Mkuu na kipenzi cha wantanzania - Hayati Edward Moringe Sokoine - Daima tunawakumbua Makamanda wetu.
 
Muasisi wa chama cha TANU, Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, Simba wa Vita na mchapa kazi.

Kalale pema peponi.....KAMANDA - I SALUTE YOU COMREAD.

Mzee sahihisho kidogo,

Waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru ni marehemu Mwalimu JKN. Kawawa (RIP) ni wa pili!!!!
 
Rashid Mfaume Kawawa alikuwa kiongozi shupavu, mwaminifu kwa chama chake na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa wananchi wa Tanzania. Kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere kwa Rashid Kawawa juu ya kuta za nyoyo zao yaliandikwa maneno "TAIFA KWANZA". Naam, Taifa limepoteza mwanamapinduzi, shujaa na mzalendo wa hali ya juu.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Mzee Wetu Rashid Mfaume Kawawa mahali pema peponi, Amen.
 
Muasisi wa chama cha TANU, Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, Simba wa Vita na mchapa kazi.

Kalale pema peponi.....KAMANDA - I SALUTE YOU COMREAD.

Kwakweli huyu Mzee tutamkumbuka sana, mchango wake ktk ujenzi wa Taifa ni mkubwa sana.

Hata hivyo ni Waziri Mkuu wa pili (siyo wa kwanza). Waziri Mkuu wa kwanza ni Mwl. J. K. Nyerere (1961 - 1962). Hatukuwa na Rais kabla ya kuwa Jamhuri, kiongozi Mkuu alikuwa Waziri Mkuu Nyerere.
 
Back
Top Bottom