Mzee Farijala wa CCM Amshambulia Dkt. Charles Kitima

Huyo mzee ni kilaza sana, mara zote akili ndogo hujadili watu badala ya kujadili masuala.Kwani Andrew Chenge,Daudi Ballali na hawa kina Lowassa Lowassa wamesomeshwa na nani kama siyo kodi zetu na kuishia kwenye kashfa za ufisadi? Sasa si bora anayetuonesha tunakwama wapi? Kwanza hajielewi, Dr.Kitima hakusomeshwa kwa fedha za CCM ila kodi za wananchi wote hivyo hakuna ulazima wa kuitumikia CCM iliyojaa ufisadi na rushwa kwa kuisifia kila mara!
 
Mkuu Mwita Maranya
Mimi huwa na mjibu tu mama toto yeye anataka sana kuingia kwenye anga zangu mimi kwa kuwa ni muungwana huwa namkwepa siku zote.
Mimi sijaliona kosa la mzee Farjalla alichoongea ni sahihi sana ni sehemu ya siasa; hii ni kumkumbusha anakotoka kama amesahau; hivi wewe hushangai kwa nini slaa haitupi kadi ya CCM wakati huwa anachoma za wenzake? Anakumbuka fadhila akitoka kwenye majukwaa kuishitumua CCM usiku kabla ya kulala huwa anaswali na kuibusu kadi ya CCM; hivi bila ya CCM ungemjua slaa??
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Msomi wa chuo kikuu?! Kwa taarifa yako huko vikuu ndio kuna wasomi wanao tumika kuliko unavyofikiri! Hivi unajua mbunifu wa kauli mbiu "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya?", unamjua mbunifu wa kauli mbiu "Maisha bora kwa kila mtanzania?" Ni mtu mahiri aliye chuo kikuu! Ukiulizwa kauli mbiu zake zimefanyaje kazi kupitia mtu aliye muandikia utashangaa! Au hujui kuwa hata aliye sema "We will mafucture teachers" naye ni msomi wa chuo kikuu cha dsm?! Au hujui kuwa hata aliyesema kuwa "Sijui sababu za wananchi wangu kuwa maskini?" Naye ni mshika shahada wa chuo kikuu bora Afrika

Muambie huyo msomi wako wapenda vya bure ni wale wanao hongwa chumvi, kofia, t shirt na khanga ili wachaguliwe.

Tumia akili usitumike tu bila kushirikishaa ubongo wako.
Prof.MUKANDALA nae eti UWT
 
Yule kitima ni janga kuu la taifa, mtokwa povu tu. Njaa inamsumbua

Hahaaaaaa njaa inamsumbua Kitima? Njaa ipi? Katika ma VC wote waliowahi kupita SAUT hakuna VC mwenye mafanikio makubwa kama kitima kaingia kukiwa na chuo kikuu Mwanza peke yake ila katanua branches kibao,Bugando,Bukoba,Tabora,Moshi,Mtwara,Iringa na hata Dar huko kote kafungua matawi ya SAUT.

Pili anatumika ki vipi huyu jamaa kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi kitu ambacho sie waafrika hatupendi kwa Mfano alishawahi kumkataza Tundu Lissu kutoa mhadhara katika kongamano SAUT kwa kusema wazi wazi hakuna alichokifanya Tundu Lissu jimboni kwake so hawezi mruhusu aje kuongea kwani sio mfano wa kuigwa.
Usipende kupanua panua mdomo kwa vitu usivyovijua kwa ushabiki wa ki chama
 
Mwasisi wa Taifa hili aliwahi kuonya kwamba hatopendezwa kama chuo kikuu cha DSM kitatoa wasomi akina ndio bwana(yes sir) kwa kila jambo.Elimu lazima ikuweke huru vinginevyo inakuwa hakuna tofauti ya wasomi na mambumbumbu.Kinachoiua CCM ni kuendekeza makada waliojichokea kama Farijala,hawana fikra mpya za kwenda na wakati tulionao.Nadhani hawa ndio washauri wa akina Pinda ndio maana wanawashauri kuropoka tu bila umakini kwa kauli wanazozitoa.
 
Salam Wana JF,

Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.

Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.

Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.

Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.

kwani huyo Farijala anahis km sio ccm Kitima asingesoma kbs? Angeweza ht kuuza mayai akajisomesha km alkua na nia bt sio mjisingzie kua ni ccm ndo imemfikisha hapo. Kama kaniki pengne ht ww ulivaa
 
FARIJALA, eti nae anajadiliwa humu ! YULE MZEE ANAMFADHAIKO WA MAISHA MAGUMU, akili zake si timamu, hata kuna kipindi niliwahi kumuona Radio Free Afrika , na siku hiyo aliibuka na matusi dhidi ya Mengi hadi ikafikia hatua ya RFA kuomba radhi.
Nilichogundua, ni Nape Nnauye ndio yuko nyuma ya yule mzee, huwa wanamuombea vipindi TV mbalimbali.
 
Ni msomi gani huyo mwehu? Yuko chuoni au chooni? sijaelewa vizuri,maana iko wazi sana wanachama wa CCM ndio wanaobebwa kwenye mafuso kwenda kupiga kelele kwenye mikutano baada ya hapo wanarudishwa na vizawadi vya kitoto wakati huo wanachama maskini wa CDM wanachangia chama! CCM ni chama cha matajiri kinachangiwa na wahindi then vijisent vinaletwa mikutanoni kwa walala hoi wananunliwa,Kama msomi ameshindwa kuona hili basi Farijala ana haki ya kubwata aliyobwata.Aibu!
 
Hii inadhihirisha mtaji wa CCM ni umaskini na ujinga, kwa sababu tu mtu ametoka familia duni basi awe mfuasi wa CCM?Kwani wote waliofanikiwa wametoka kwenye familia zenye uwezo?Na nikitoka familia duni siruhusiwi kuwa mfuasi wa chama cha upinzani?Na je ni tangu lini CCM imemlipia mtu masomo?
 
DR Kitima hana njaa kwani mtu ukijielez mtazamo wako kuna ubaya gani hata watoto tunawazaa na kuwasomesha lakini wanatukosoa wazazi.sasa hiyo ccm inayokwenda halijojo ukiisema imekua una njaa?
 
Mwita ni kweli namie nimemuona na kumsikiliza hadi nikaona kama Wazee waliobaki CCM ndiyo hao basi CCM hakuna Wazee. Mf. Ameulizwa na mtangazaji kuhusu Tanzania imefikia wapi kwenye malengo ya milenia yanayokamilika 2015, mzee yeye kaenda kwenye mabomu ya Arusha, mtangazaji amejitahidi sana kumweka kwenye mstari waapi! Hivi huyo Mzee Farjalla ndiyo yule fisadi wa EPA?

Namshangaa MUNGU kwa nini mizee kama hiyo bado ingali inaishi hapa duniani na hasa Tanganyika?
 
There are currently 1040 users browsing this thread. (33 members and 1007 guests)

Karibuni ndugu wageni msichungulie kupitia dirishani, ingieni ndani ili mtuletee maoni yenu kwani naamini hamko kwenye thread hii kwa bahati mbaya.
 
Salam Wana JF,

Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.

Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.

Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.

Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.

Juzi jumapili mwenyekiti wa UVCCM alikuwa akiongea na wanafunzi wa elimu ya juu pale Moshi mjini..

Tena walikuwa wanalipwa pesa nzuri tuu ili wahudhurie kile kikao cha jamaa,
Wengi walikimbia baada ya kugundua waandishi wa habari walikuwepo,

CCM inatoa Pesa ili hao wanafunzi wafanye siasa..
 
Back
Top Bottom