My CCM, NEVER do that again!

kabindi

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
333
120
Msingi wa kwanza wa uimara wa chama ni wanachama wake. CCM tunajivunia kuwa na idadi kubwa yawanachama wapatao takribani milioni 9. Ingawa sidhani kama takwimu hizi zipo "updated" kwa maana kwamba sina hakika kama CCM tunayo kanzi data ya wanachama wetu na kama ipo basi siyo "active". Nasema hivyo kwa maana kipindi hiki kilikuwa cha viongozi wa CCM kutambua thamani ya wanachama wake. Mtaji huu wa wanachama usingesababisha CCM kutumia gharama na nguvu kubwa kiasi cha kutisha kama inavyojidhihirisha katika uchaguzi huu.

Matharani, ikiwa katika idadi hiyo ya wanachama milioni 9, wanachama milioni 4 wamehama,au kufariki, n.k, na hivyo kubaki na wanachama milioni 5, kwa hesabu ya haraka hao wanachama waliobaki kila mmoja akiweza kushawishi mpiga kura mmoja tu, idadi ya kura za uhakika inakuwa milioni 10 na hivyo kuwa na uhakika wa ushindi wa mapema. Ikizingatiwa kwamba kuna wapiga kura wengine wasio kuwa wanachama wataipigia kura CCM bila kushawishiwa na hivyo kura kuongezeka hadi kufikia milioni 10+. Nina imani idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura haiwezi kuzidi milioni 19.

Bahati mbaya
nahisi kama viongozi wa CCM hawakuwapatia thamani ya kutosha wanachama wake ya kutambua uwepo wao kama vile kuwashirikisha vya kutosha katika mikakati ya kukijenga chama na kutengeneza ushindi mapema, na hivyo wanachama wengi kuto-feel uanachama wao na kuonekana kama vile wapiga kura wengine wa kawaida wasiokuwa wanachama. Hii imejidhihirisha ambapo imeonekana kama nguvu nyingi kupelekwa kwa wasanii ii walete ushawishi na kutumia nguvu za ziada kudhoofisha viongozi wa upinzani. Nakubaliana na hizo "strategies" lakini pengine zisingekuwa kipaumbele "from day one". Raslimali zilizotumika wakati huu zingekuwa zimewekezwa kwa wanachama mapema, hapana shaka chama kisingetumia nguvu kiasi hiki.


Ni vizuri kwa wakati ujao kuimarisha kanzi data ya wanachama ikionyesha mahali wanachama walipo, kazi zao, professional zao na mambo mengine ambayo tutayaona ni yaMsingi. Pia pawepo na mfumo mzuri wa vikao kwa wanachama wote kwa vikundi pale walipo ili kujadiliana na kupeana mikakati ya kukijenga chama. Mfano mzuri tunaoweza kujifunza ni mfumo wa kanisa Katoliki wa kuwa na jumuiya ndogo ndogo ambazo zinasaidia sana kuimarisha Kanisa hilo. Hivyo si vibaya tukakopa kutoka huko au mifumo mingine inayofanana na hiyo. Pengine
mawazo yangu yangeweza kuwa "postmoterm" baada ya uchaguzi, lakini si vibaya pia kuyatoa kwa wakati huu ambapo afya na uhai wangu unaniruhusu.

Mwisho,tuzingatie maslahi ya Chama na Taifa kwanza na siyo UBINAFSI tulioushuhudia kwa kipindi kirefu. Ninayo Imani kwamba CCM tutashinda ingawa Lowassa anatutoa Jasho kwelikweli.
 
Huo ni muono wako c mbaya lkn watu wamechoka ufisad was wazwazi unaofanyika huku serikali yetu ya ccm ikiwa inachekelea.
 
Back
Top Bottom