My best gospel song ever

Kuna hawa jamaa ni wakongo wapo canada wanaitwa krystaal wazuri mnoooo
Yes nawasoma wale jama
Nina kaka yangu anawaoenda sana. Kuna kibao wameimba "eeh yahwe" version yao kali sana

Kaka zangu wanapenda sana gospel songz kwa kweli
 
Lauren Daigle anakuja juu kwenye worship and praise, katoa mpya mbili kali sana, sikiliza mojawapo inaitwa FIRST....inakuambia before I bring my need I will my heart...before I lift my cares, I will my arms....endelea.
 
"Shine the light let the whole world see 'we are singing' for the Glory of the Risen King..Jesus...."
Na ile solo guitar inavyoita na kupokewa na drums kisha vyombo vyote wakati nyimbo inaanza,dah!jamaa ni wazuri mno kwenye music arrangement.
Huku kwetu Africa labda wasouth ndio wako vizuri eneo hilo.Kuna ngoma mbili za dada Rebecca,moja inaitwa Look at me Lord (humo kuna wanaume wa shoka wanaharmonize kwa sauti za bass ni shida yaani) na nyingine inaitwa Uyingcwele,hii naipenda ile namna yake ya mapigo ya kitamaduni,muafrika ni muafrika tu,kuna mapigo ukiyasikia unaona mwili unaanza kumtukuza Muumba wake wenyewe:D,ndio hapo wasouth wametushika,wana fuse muziki wa kisasa na ngoma zao za asili.
 
Upendo Nkone & Christina Shushu ndio kiboko yangu
hata waimbe nini,sichoki kuwasikiliza
Mimi hizi za nyumbani kuna vile vikwaya vya zamaniii,basi nikisikiliza zile roho inatulia kwa Yesu.
Kuna kwaya inaitwa Kilimanjaro revival na ile nyimbo yao ya Upendo wa Mungu(Agape).
Kuna wale jamaa wa Kijitonyama na ule wimbo "Kama si wewe ningekuwa wapi".
Kuna nyimbo ya kwaya moja ya Kurasini catholic mt.Maurus nadhani chorus inanukuu maneno fulani ya Mungu kwenye biblia akisema " mawazo ninayowawazia ninyi ni mawazo ya amani,wala si ya mabaya,asema bwana".
Kuna ule wimbo wa Lulu.
Kuna huyu mdada anasema "napenda kufanana nawe",sijui anaitwaje yule?
Kuna wale wa kkkt Kimara wanaimba "Ulimwengu nilimo ni wa mateso"
Ng'ang'ania baraka wa AIC Shinyanga
Kuna ule wa "sipati picha" wa Tabata,n.k zipo nyingi sana nzuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom