Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Jamani, nahisi sifa moja kubwa ya kuwa mwanasiasa Tanzania ni uwezo uliopitiliza wa kuwa mnafiki. Sishangai serikali ikimgeuka Mengi. Ila katiba si inaruhusu mtu kutoa maoni yake na kama inaonekana kuna waliokosewa wampeleke mahakamani. Serikali kuwatetea hawa wafanyabiashara ambao wengi tunajua wanatudhulumu, ndio watakuwa wamechemsha
Serikali yetu inashangaza; Waziri Simba na Mkuchika wameiabisha serikali sana katika sakata hili kwa wanaonekana kuwasemea na kuwatetea Watuhumiwa.
Kinachoshangaza ni jinsi wanavyomchulia Mengi, labda sikufuatilia vizuri lakini ni vema Mawaziri hao wajiulize Mengi alitoa tuhuma hizo kwa kuvialika vyombo vyake pekee au alialika vyombo vyote vya habari (vikiwamo vya Rostam)? Kama Mengi alizungumza na vyombo vyote vya habari na vyombo vyote viliripoti habari hii, iweje leo Mawaziri wetu waseme ati Mengi anatumia vyombo vyake vya habari vibaya? Hao T/Daima, Mtanzania, Majira nk walioripoti habari hiyo nao watachukuliwa hatua gani? Nijuavyo mimi Mengi aliongea na Waandishi na Vyombo malimbali vya Habari na si vyombo vya IPP!
Waziri wa Utawala Bora Sofia Simba ni vema angesea kuwa Serikali itafuatailia na kuchunguza tuhuma dhidi ya "raia wema" (Watuhimiwa wa Ufisadi) kuliko kumshukia Mengi moja kwa moja, hii inaonyesha kuwa ama wameshegemea upande mmoja au wana chuki binafsi na Mengi.
Mawaziri wetu wanachemsha! They don't qualify kuwa Mawaziri, WAJIUZULU!