Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

I can't argue with you mkuu because you make a good point. I am against discrimination in any shape, form or manner be it racism, sexism, tribalism, religionism etc. but don't you think we should at least hear that evidence that Mengi claims to have? The mannerism in which he used in this case is wrong but since the cat is out of the bag why don't we just hear what he claims to know? Instead ya kujigawa kati ya wanaozani Mengi mzalendo halisi na wanaoona Mengi ana agenda zake kwa nini tusidai atoe huo ushahidi wake tujue moja? Akisha toa huo ushahidi ndiyo tutajua nia haswa ya Mengi. Mengi is not above the law but neither are the mentioned people. If he really has the evidence let the authorities ask him to give it & deal with the matter according to the laws of the country. I am tryin to be unbiase the best I can here so mimi naona ili kujibu maswali yote haya Mengi atoe ushahidi anaodai kuwa nao halafu sheria ichukue mkondo wake. Maana kama kuwataja hao watu ambao ni innocent untill proven guilty kashawataja kwa hiyo hamna maana kubishana kama njia aliyo tumia ni sahihi au la. kilicho baki atoe ushahidi wake kama una basis sheria ifuate kama mzee mzima aliji ropokea tu basi na sheria uchukue mkondo wake. Jamani wana JF mnaonaje? I think thats fair but its only my opinion.

Ninakubaliana na wewe kabisa.

Ukiangalia malalamiko mengi juu ya chaguzi kuu wachangiaji wengi hueleza kuwa wananchi hupewa kanga na pilau then wanachagua mtu. Maana yake ni kuwa wananchi wanakuwa influence na hali hiyo na kuwaondolea haki zao msingi za kufikiri na kufanya maamuzi.
Katika hili la Mengi nilieleza katika thread moja wapo ya mwanzo kabisa kuwa kabla ya kumsifia Mengi kwa hiyo press conference yake ni vema tumbane afikishe ushahidi na vielelezo katika vyombo vya sheria. Kwa kufanya hivyo sisi kama watanzania tungekuwa tumetimiza wajibu wetu na kujiondoa katika kuegemea upande mmoja. Lakini kama unavyojua tena hii forum ina watu wengi na mitizamo tofauti na vilevile motives mbalimbali. Hali hii inafanya kujadili hoja bila ya kuangalia uhalisia as a results hoja inakufa bila ya kuleta tija au impact yeyote.
Kwa vile Mengi ni Chairman wa makampuni makubwa na ni mhasibu ni imani yangu kuwa anaendesha biashara kwa kuzingatia miiko mbalimbali (ethics), kwa vile Mengi si mwanasiasa basi ni vema akatoa ushahidi na vielelezo. Vinginevyo awe muungwana awaombe radhi kwani sitegemei kuwa Mengi anaendesha makampuni yake bila kuzingatia miiko mbalimbali na hafanyi maamuzi ya kibiashara kwa kuzingatia siasa.
 
Sophia Simba alipokuwa akimponda Mengi leo asubuhi ktk mahojiano na Marin Hassan alionyesha kusahau alichokariri.

Nilishangaa sana kumuona Mheshimiwa anaongea kama vile yuko katika mipasho ya Kitchen Party!

Sasa tunajiuliza, JK anatumia kigezo gani kuwateua hawa Mawaziri wetu??? Tena waziri wa Utawala bora anayemhukumu Mengi kuwa "kawahukumu mafisadi" wakati yeye hapohapo anamhukumu Mengi! Mh. Simba kuwa waziri wa Utawala bora ndio anakuwa UNIVERSAL BAROMETER hapa TZ.

I get my fingers CROSSED!

Amesema nini yeye mwenyewe? Tuwekee direct speech.

Hiyo ni reported speech, tafsiri yako wewe Midas Touch, mawazo yako wewe, ulivyomuelewa wewe; na kila mtu ana mawazo yake, na mjadala unaweza ukaishia hapo hapo katika kuheshimu mawazo yako.

Kama unataka na wengine wachangie kwa mapana zaidi basi tuwekee hata sentensi moja ya alichokisema ili tuone huko kuchemka kwake tushawishike na ulichosema wewe.

Huwezi ukaruka tu kuja kusema "...Simba kachemka TBC1 kamponda Mengi leo asubuhi..." na lile na hili na kile. Baadhi yetu tunataka kusikia alichosema yeye mwenyewe Simba, sio wewe ulivyotafsiri.
 
Ninakubaliana na wewe kabisa.

Ukiangalia malalamiko mengi juu ya chaguzi kuu wachangiaji wengi hueleza kuwa wananchi hupewa kanga na pilau then wanachagua mtu. Maana yake ni kuwa wananchi wanakuwa influence na hali hiyo na kuwaondolea haki zao msingi za kufikiri na kufanya maamuzi.
Katika hili la Mengi nilieleza katika thread moja wapo ya mwanzo kabisa kuwa kabla ya kumsifia Mengi kwa hiyo press conference yake ni vema tumbane afishe ushahidi na vielelezo katika vyombo vya sheria. Kwa kufanya hivyo sisi kama watanzania tungekuwatumetimiza wajibu wetu na kujiondoa katika kuegemea upande mmoja. Lakini kama unavyojua tena hii forum ina watu wengi na mitizamo tofauti na vilevile motives tofauti. Hali hii inafanya kujadili hoja bila ya kuangalia uhalisia as a results hoja inakufa bila ya kuleta tija au impact yeyote.
Kwa vile Mengi ni Chairman wa makampuni makubwa na ni mhasibu ni imani yangu kuwa anaendesha biashara kwa kuzingatia miiko mbalimbali (ethics), kwa vile Mengi mwanasiasa basi ni vema akatoa ushahidi na vielelezo. Vinginevyo awe muungwana awaombe radhi kwani sitegemei kuwa Mengi anaendesha makampuni yake bila kuzingatia miiko mbalimbali na hafanyi maamuzi ya kibiashara kwa kuzingatia siasa.

kwanini usiulize kama Polisi wana mpango wa kwenda kuuliza ushahidi alionao au waliotajwa kwenda mahakamani ili ushahidi utolewe mahakamani. Ndio maana tuna mahakama. Mimi nikiibiwa na kusema fulani kaniibia ni Polisi ndio wanakuja kunichukua mimi, na mtuhumiwa wangu na ushahidi na kupeleka mahakamani na mimi nikaitwa nielezee upande wangu, na mtuhumiwa ataitwa ajitetee halafu na ushahidi utaangaliwa.

So, kumtaka Mengi ajitolee kupeleka ushahidi siyo sawa hata kidogo; Ni polisi au waendesha mashtaka ndio wanatakiwa kufanya kazi hiyo. Lakini hawawezi kufanya hivyo bila mtu kulalamika. So, watake Manji, Patel, Rostam, na wengine waende Polisi kushtaki. Hapo ndipo utawala wa sheria unapotakiwa. Lakini so far, hata majina yao hutaki kuyagusa umeng'ang'ania Mengi aende..

Kwanini hawa jamaa wasiende Polisi kushtaki kuwa wamekashfiwa au kudhalilishwa?
 
Sophia Simba alipokuwa akimponda Mengi leo asubuhi ktk mahojiano na Marin Hassan alionyesha kusahau alichokariri.

Nilishangaa sana kumuona Mheshimiwa anaongea kama vile yuko katika mipasho ya Kitchen Party!

Sasa tunajiuliza, JK anatumia kigezo gani kuwateua hawa Mawaziri wetu??? Tena waziri wa Utawala bora anayemhukumu Mengi kuwa "kawahukumu mafisadi" wakati yeye hapohapo anamhukumu Mengi! Mh. Simba kuwa waziri wa Utawala bora ndio anakuwa UNIVERSAL BAROMETER hapa TZ.

I get my fingers CROSSED!

Mi mwenyewe nilistuka nilipoona vile vidole kaviweka juu kama vile alikua anamzodoana kumsuta Marin Hasani, nadhani baadaye alijishtukia mwenyewe akaviweka chini.
Mpaka sasa najiuliza iwapo Mh Rais atampongeza Mengi kwa ushujaa aliouonyesha katika hotuba ya mwisho wa mwezi huu, je huyu waziri atakua tayari kujiuzulu??
 
Kwa nini Serikali inawajibia mafisadi?

Hata mimi nashindwa kuelewa nini kinawasibu mawaziri wetu na kinachowakera sana ni nini. Wameambiwa wasipofanya vile hakuna mgawo? Kwanini wajiingize kwenye mambo haya? Why? Kuna nguvu ya ziada inayowalazimisha wafanye hivi vinginevyo...?!?
 
Ninakubaliana na wewe kabisa.

Ukiangalia malalamiko mengi juu ya chaguzi kuu wachangiaji wengi hueleza kuwa wananchi hupewa kanga na pilau then wanachagua mtu. Maana yake ni kuwa wananchi wanakuwa influence na hali hiyo na kuwaondolea haki zao msingi za kufikiri na kufanya maamuzi.
Katika hili la Mengi nilieleza katika thread moja wapo ya mwanzo kabisa kuwa kabla ya kumsifia Mengi kwa hiyo press conference yake ni vema tumbane afishe ushahidi na vielelezo katika vyombo vya sheria. Kwa kufanya hivyo sisi kama watanzania tungekuwatumetimiza wajibu wetu na kujiondoa katika kuegemea upande mmoja. Lakini kama unavyojua tena hii forum ina watu wengi na mitizamo tofauti na vilevile motives tofauti. Hali hii inafanya kujadili hoja bila ya kuangalia uhalisia as a results hoja inakufa bila ya kuleta tija au impact yeyote.
Kwa vile Mengi ni Chairman wa makampuni makubwa na ni mhasibu ni imani yangu kuwa anaendesha biashara kwa kuzingatia miiko mbalimbali (ethics), kwa vile Mengi mwanasiasa basi ni vema akatoa ushahidi na vielelezo. Vinginevyo awe muungwana awaombe radhi kwani sitegemei kuwa Mengi anaendesha makampuni yake bila kuzingatia miiko mbalimbali na hafanyi maamuzi ya kibiashara kwa kuzingatia siasa.

mara nyingi hatupendi ukweli, ushabiki una mipaka, na pia mashujaa hutukuzwa kwa lile jema,

Point za Sofia Simba si za kuzipuuza na ni za kisheria zaidi hata kama tutaamua kupinga na kupiga kelele, lazima tutofautishe mipasho na sheria. Mengi katika hili amebanwa hata kama tutamtukana Sofia Simba, na ndio mara nyingi tunasema japo wengine wanabisha, maneno matupu hayatusaidii, watanzania sidhani kama alilosema MeNGI JUZI NI LA AJABU SANA, linajulikana na kila mtu!

The best way ni kuwa kupeleka hawa watu mahakamani! kama ushahidi upo, basi ni huko mahakamani, Mengi fedha anazo na amejitoa mhanga, hatima ya haya yawe mahakamani, SOFIA ANGEKUWA KIMYA SO AS MKUCHIKA!

TUwe wakweli jamani, kutaja mfisadi hadharani ni vizuri kwa hali yetu hii! lakini haina tofauti na kuchoma vibaka pale wanapopigiwa kelele za mwizi! if they are accused let mahakama iamue,! Mengi amefanya mengi amesaidia mengi, na inapofikia kuongea hili kama mimi, kuna maswali mengi, sana je amesaidia nini katika hili? kujua kuwa hawa jamaa ni mafisadi?? mbona inajulikana mpaka kwa watoto wadogo?

Twende mahakamani, tuko nyuma yake, kuwsema huku bado wakiwa na fedha zetu haisaidii this truth hurt
 
Kukaa kimya kwao ina maana ni ukweli, na kama si kwelil wamshtaki maana shutuma hizo ni kubwa. Nadhani Mengi ana ushahidi kwa aliowasema na kama ulivyosema, '' ni wafanyabiashara wakubwa na wengine ni mahasimu wake siku nyingi''. Anawajua vizuri.

Tom,

Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:

Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?
 
Hawa viongozi wanaotoa kauli za kumshutumu Mengi nashidwa kuwaelewa kama watajwa wanaona ya kua wametendewa haki wana haki ya kutafuta haki zao kupitia mahakamani kwa kumshitaki Mengi.Hapa naona kitu kimoja hawa viongozi wanowatetea watajwa wana sababu zao.Kwanza sio siri ya kua CCM na viongozi wengi serikalini akiwemo Mh.Rais wamewekwa au kuingia madarakani kwa msaada wa hao mafisadi cha kusikitisha kwa pesa walizoziiba kwa walala hoi.Pili hao viongozi wanafikiri ya kua kuwakingia mafisadi kifua ni kumsaidia Rais Kikwete au wanajipendekeza kwani kuwanyooshea mafisadi kidole kama nilvyosema katika sababu ya kwanza ni kwanyooshea vidole Mh.Kikwete na viongozi wengi wa serikali MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mara nyingine hao viongozi hawafikirii na kuona huo ujumbe unaenda kwa akina nani.

Ujumbe wa Mengi ulikuwa clear nasi ni wafuasi wake. Alichoongea huyo mama aliyesoma chini ya mwembe na kujipatia vyeo kirushwa rushwa ....kingonongono......ni upupu mtupu .Waamuzi ni sisi. Mengi aluta continua Mzee? mapambano bado yanaendelea.
 
Tom,

Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:

Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?

Au unamchoma moto??

Thanks fella
 
Tom,

Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:

Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?

mfano wako mzuri although misleading; Mengi hajaibiwa na kina Manji na Rostam bali anadai Taifa.. so nani anatakiwa kwenda mahakamani si aliyeibiwa? Mengi kasema (na wengine tumekisema kabla yake) kuwa wanaohusika na ufisadi mkubwa nchini ni hawa na ushahidi ni huu sasa kama Taifa linaona tunawadanganya basi watupuuzie au wachukue hatua lakini kama wanaona kuna hoja wafuatilie na waende mahakamani.

Kama Mengi ndiyo angekuwa ameibiwa personally na kusimama kuwatuhumu hawa hadharani basi hata mimi ningesema kwanini hakwenda mahakamani (kwenye mfano wako). Tatizo hajaibiwa personally ni Taifa. Alichofanya siyo tofauti na alichofanya Dr. Slaa pale Mwembe Yanga! Si walisema anawaonea na wakamwambia aende mahakamani, leo ni nani aliyewafungulia wengine mashtaka Dr. Slaa?

Si serikali? So why not take alichosema Mengi wakifanyie kazi na wakufikishwa mahakamani wafikishwe?
 
Tom,

Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:

Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?

Mshikaji fikiria nje ya BOX. Aliyeibiwa nguo ni wananchi wa Tanzania. hao wananchi wanakuwa represented na POLISI (au kwa upana SERIKALI).

Sio kazi ya mwananchi kumfungulia mwananchi mwingine kosa la JINAI. Ni Polisi au ofisi ya DPP ndo ina mamlaka hayo.

Mengi hana mamlaka ya kuwapeleka mahakamani hao mafisadi kwa CRIMINAL CASE.

Jamani muwe mnauliza kwanza!
 
Mbona TV yake hiyo hiyo ilipoibua rushwa kwa matrafiki, (Ripoti Maalum ya Jerry Muro) serikali ilichukua hatua na pia kumpongeza Jeri kwa kitendo cha kishujaa????
 
Mshikaji fikiria nje ya BOX. Aliyeibiwa nguo ni wananchi wa Tanzania. hao wananchi wanakuwa represented na POLISI (au kwa upana SERIKALI).

Sio kazi ya mwananchi kumfungulia mwananchi mwingine kosa la JINAI. Ni Polisi au ofisi ya DPP ndo ina mamlaka hayo.

Mengi hana mamlaka ya kuwapeleka mahakamani hao mafisadi kwa CRIMINAL CASE.

Jamani muwe mnauliza kwanza!

tatizo ndugu zetu hapa wanaliangalia kwenye personality.. kwamba aliyesema ni Mengi. It has nothing to do with the nature of the accusations. Jamani, Dr. Slaa ameyasema hayo na hivi majuzii wabunge wenzie wamemtuhumuu wizi Bungeni na hakuna aliyekwenda mahakamani kumfungulia mashtaka.. lakini hili la Mengi watu wanataka kuonekana wanadai utawala wa sheria.. Really?
 
Ndugu hii sera na maoni yako yataweza tukifanilkiwa hapa tulipo. Wewe jiulize kagoda ipo wapi? Meremeta je?

Acha mambo haya, we are tired. Huu utawala bora umetushinda na wewe ndo unaupalilia. Dr. Slaa amewaambia yeye ndo anamiliki nyaraka za siri, nani mwenye moral support kumkamata? we are tired. Kama wewe unafaidika na utawala bora ni wewe na jitahidi katika hilo, mimi sitaki utawala bora.

AMANI WAKATI HAKUNA UTULIVU?

Ndugu yangu inaonekana kuwa umekata tamaa na huenda hali hiyo imesababishwa na kukosa mikakati thabiti ya kujadili hoja mbalimbali ili zilete manufaa. Wajibu wa kupamba au kuleta mabadiliko si wajibu wa mtu mmoja katika jamii, hata huyu Dkt Slaa itafika wakati kama binadamu atachoka tu. Kitu cha msingi ilikufikia mabadiliko kwanza nikujiuliza wewe mwenyewe kama uko tayarii kubadilika. Pili, jiulize are you doing the right things, either nyumbani kwako, kazini, shule nk. Endapo utakosa kujiuliza mambo kama hayo hutaweza kuwa na mikakati ya kweli ya msingi kabisa ya kuweza kuleta mabadiliko...matokeo yake utakuwa vulnerable na influences...2010 utaweza kushawishika kupiga kura kwa upande wa khanga na pilau.
Maana yangu ni kwamba tusipofanya mambo kwa kuzingatia utaratibu basi hatutaweza ku-influence changes at all, tusahau, tutakuwa wapiga kelele tu!
 
Sophia Simba alipokuwa akimponda Mengi leo asubuhi ktk mahojiano na Marin Hassan alionyesha kusahau alichokariri.

Nilishangaa sana kumuona Mheshimiwa anaongea kama vile yuko katika mipasho ya Kitchen Party!

Sasa tunajiuliza, JK anatumia kigezo gani kuwateua hawa Mawaziri wetu??? Tena waziri wa Utawala bora anayemhukumu Mengi kuwa "kawahukumu mafisadi" wakati yeye hapohapo anamhukumu Mengi! Mh. Simba kuwa waziri wa Utawala bora ndio anakuwa UNIVERSAL BAROMETER hapa TZ.

I get my fingers CROSSED!
Nami pia nimeiona hiyo. Amejikanyagakanyaga sana. Kwanza aliulizwa maana ya utawala bora. Kilichoelezwa ni upupu. Akapewa swali la mtego kuhusu watu wanaolalamika juu ya ukosefu wa maadili (Marin hakuweka bayana, nadhani kwa makusudi). SS akachemka, akaenda moja kwa moja kwa kumtaja Mengi na ishu ya mafisadi. Maelezo aliyoyatoa ni marudio ya mara kwa mara ya kauli yake "....ni kosa la jinai kumtaja mtu kupitia vyombo vyako vya habari....." Nilitamani Marin aulize, Je angetumia vyombo vingine (visivyokuwa vyake) ingekuwa halali?
Nadhani nia yake SS ilikuwa ni kujisafisha kwa wananchi, lakini alichofanya ni kujichafua zaidi.
Kama viongozi wetu ndio hao, basi bado tuna safari ndefu sana! Tujipe pole.
 
Kuna watu ambao huwa nawaona hawastahili kabisa kuwa viongozi ni huyu Sophia Simba, hawezi hata kujenga hoja za msingi kama vile hajaenda shule kabisa. Sijui mkuu wa kaya alitumia kigezo gani kumpa uwaziri huyu mama. Maana bado anaonekana ana mawazo ya mtaani. Serikali inafikiria kumchukulia hatua? ama kweli sasa hii serikali inabidi kuisaidia, kwa sababu inafuatilia mambo yasiyo na tija kwa watanzania wasio na uwezo hata wa kununua chumvi na panadol ya sh 100. Bado inaendelea kuwatesa hawa watu wasio na hatia, je walifanya makosa kuzaliwa Tanzania? mpaka hawa wezi na sirikali isiyo jali hawa watanzania. Kama hawa mawaziri walikosa vitu vya kuongea na waandishi wa habari wangekaa kimya kwa sababu wanaendelea kutupa taka kwenye dampo lao la CCM. Na sasa taka zinakaribia kujaa na zinatoa harufu mbaya na ni hatari kwa maisha ya watanzania. Ikiwezekana inabidi watanzania tuamue kulifunga hili dambo la sivyo tutaendelea kupata madhara ya kiafya na kiuchumi.

Jibu ni hili:
Ni vizuri tukaanza kugudua kundi la mtandao ambalo limetufikisha hapa tulipo.
Sofia na wenzake wanamwandama Mengi kwa kuwa amegusa mtandao wao.
lakini hakuna mapana yasiyokuwa na mwisho,Serikali yetu isitumie rungu ambalo limepewa na wananchi kunyamanzisha watu.je mkuchika na Sofia ndo wasemaji wa wahusika? mbona hawajawa msitari wa mbele kutusaidia kuelimisha umma kuhusu KAGODA kama walivyojitokeza katika hili.
 
Tumeshachoka kungojea 2010 ilikuachia mafisadi wote baada ya JK kupita;... desperate times call 4 desparate measures; we are heading to 2010 now and so far in the last 5 yrs nobody (not even a single person) has been held accountable. How can we take this process seriously anymore....Tanzanians are not Stupid and what Mengi is doing is proving that.

Besides Mengi has made allegations not judgements on these ppl, why doesnt the governnment do what it does best and form a comitee 2 investigate these allegations??

The true question here is how long is JK & CCM going to continue harbouring these ppl who are slowly and painfully destroying TZ and expect to remain the Darling of Tanzanians????
 
Binafsi inaniuma sana. Wakati mwingine najihisi kama ni mgeni hapa nchini kwangu. Hivi Nyie wakuu wetu kwani hayo aliyoyazungumza Mengi ni Mageni masikioni mwetu? NAni asiyeijua Kagoda? na wamiliki wake? Kwani mngenyamaza kimya ingekuaje? Hivi hamjui wananchi wana hasira na serikali yao? Tafadhalini mnaivuruga amani yetu. Mnasema Mengi kakosea yeye si msemaji wa hizo issues sasa nyie ndio wasemaji wakuu? Kwani Jeshi la Polisi halikutoa Msimamo kuhusu hilo la Mengi siku ya pili yake? Hivi Mkuu wa Kaya (Mjomba) unayaona haya? Ujue wanakuharibia chukua hatua......... Inauma, Inauma sana
 
Huyu Sophia Simba, hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora kwani hajui kabisa anatakiwa asimamie nini. Anasahau, au hajui kuwa serikali ndiyo mvunjaji mkuu wa utawala bora kwa hiyo jukumu lake ni kusimamia serikali isiwe inafanya hivyo -- yaani kukiuka kanuni za utawala bora.

"Utawala bora" haumaananishi kuangalia watu binafsi wanakashifiana, kama vile Mengi kuwataja mafisadi hadharani. Suala kama hili silo lake kwani lina utaratibu wake -- yaani wale waliojisikia kukashifiwa wafanye nini kutafuta ahueni. Waende mahakamani kumshitaki kwa kuwakashifu. Hili yeye mwenyewe Mengi aliliweka wazi, lakini Simba hataki kuliona au kulikubali.

Leo ni siku 5 lakini hatujasikia kwamba waliokashifuiwa na Mengi wanapanga kwenda mahakamani -- na wala kwa umoja wao, au mmoja mmoja ameitisha press conference kumjibu Mengi -- kwa hoja zozote zile -- yaani hata zile za kushambulia private family yake, hoja ambazo ndizo hasa wanaona imara kuliko zile za ndani ya subject yenyewe.

Sophia analiingiliaje suala hili? Jee amepewa kitu kidogo na hao ili awasemee ktk vyombo vya habari? Picha inayopatikana ni hiyo.
 
Back
Top Bottom