Hapo kwenye red mhusika hakufanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyilo, baada ya kupigwa chini wakati wa mchakato kwa kura za maoni kulelekea uchaguzi mkuu.Mawaziri waliotemwa,kwenda kukaa beki bencha bungeni hawa....
Prof.Juma Kapuye
Prof.David Mwakyusa
Prof.Peter Msolla
Mh.Chiligati
Mh.Summari
Mh.Seif Khatibu
Mh.J.Wanjancha
Mh.H Chibulunje.....
Kama kuna aliyesaulika ongezea....
katoka wapi huyu? au mzenji?
Mawaziri 29 na manaibu 21. Tisa kujumlisha moja ni kumi, unaandika sifuri unakwenda na moja. Mbili kuongeza mbili, nne na ile moja tano. Hivyo, 29+21 =50.
Njoo tuisheni mdogo wangu.
Kwani kulikuwa na makubaliano ya kupunguza baraza? Mbona mnataka kuingilia kazi ya Rais? Ni uamuzi wake na chama chake kupanga safu kwa jinsi wanavyoona ni bora na kwa manufaa ya nchi.
Hii ni Serikali yake, Anatekeleza ilani ya chama chake, hamwezi ku-influence chochote katika uundwaji wake.
Tulio wengi tumeridhika sana na hili baraza. Ni kazi nzuri.
najaribu kujiuliza ni kitu gani kilichokuwa kigumu katika hili baraza jipya hadi likamchukuwa JK pamoja na wasaidizi wake wote zaidi ya wiki mbili kuliunda? Kama imemchukua muda mrefu namna hii kuunda baraza la mawaziri je watendaji wake wakichelewa kutekeleza majukumu yake watalaumiwa?
Prof. Msola yumo. Fuatilia vizuri vyanzo vyako! Angalia wizara ya Kilimo
Mawaziri 29 na manaibu 21. Tisa kujumlisha moja ni kumi, unaandika sifuri unakwenda na moja. Mbili kuongeza mbili, nne na ile moja tano. Hivyo, 29+21 =50.
Njoo tuisheni mdogo wangu.
Usishangae ndugu. Hesabu ya Mkwere inamaanisha kuwa kazi aliyokuwa naifanya Shukuru Kawamba ni sawa na Mawaziri wawili na Naibu wawili?!!!!!!!!!!!!!!!!! Ahahahahahahahaha Hesabu ya Mkwere hiyo.Hili baraza ingawa kweli lina wachapakazi lakini ni kubwa sana.
KWA MFANO hakuna umuhimu wa kuwa na wizara mbili zinazoshughulikia usafirishaji. Rais amevunja ile wizara ya maendeleo ya miundombinu (Infrastructure devpt) na kutengeneza mbili: Wizara ya Ujenzi (Works) na Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi (transport). Haiingii akilini anawaza nini hapa. Tunahitaji wizara moja itakayounganisha vyombo vyote vya usafiri kwani vinategemeana. Hapa ndio anatengeneza barriers kwa watendaji wake. Kwa mfano uakiangalia sera ya usafiri wa tanzania (Transport Policy) inahusu nyanja zote za usafiri. Ntaendelea kuwalaumu washauri wake kwani wanamshauri Rais vibaya. Tunahitaji wizara moja tu ya usafirishaji tena iongozwe na Magufuli. Labda angeweka manaibu wawili ningemwelewa kidogo. Lakini aaaagr, kuna tatizo hapo. Jamani sio kila mtu awe waziri.....na hawezi kumfurahisha kila mbunge kwa kumzawadia uwaziri.
HILI BARAZA KULINGANA NA HOTUBA YA BUNGENI MBONA KUBWA SANA INA MAANA HALINA TOFAUTI NA LA MWAKA 2005, KAMA MAWAZIRI 29 NAIBU 29 INAMAANA TOTAL 58, Je wale 60 KUNA TOFAUTI KWELI, HII TANZANIA KWELI. HAWA WOTE GARI MPYA, NYUMBA, BUDGET ZAO TU, UJE MAKATIBU WA WIZARA 29 ZINGINE NI MPYA HII YA UJENZI HAIKUWEPO.
KWELIIIIIIIIIIIIIIIIII, TZ TUTAUMIA SANA.
Jamani mi simuelewa naitaji kuelimishwa, Waziri wa maji kazi yake nini?
Msola hana ishu SUA palimshinda ataweza wizara.
Kapuya abaki kuendesha bendi yake ya AKUDO tu uongozi wake wa jaziba na amemuingiza JK kwenye matatizo kumbuka ishu ya mgomo wa wafanyakazi.
Meghji ni haki yake yeye ni mama wa mipasho tu bungeni uongozi labda aende bendi ya taarabu awe rais wao.
- Idara ya Umwagiliaji tumeiunganisha na Kilimo ambako ndipo ilipokuwa zamani.
- Imeonekana upangaji wa maendeleo ya kilimo unakuwa hauna hakika bila ya umwagiliaji kuwa sehemu ya kilimo. Tuliihamishia maji kurahisisha pia upangaji na hasa kwa vile maji ndiyo wanaotoa haki ya matumizi ya maji.
- Kwa kuwa tatizo la uhaba wa maji ya binadamu ni kubwa sana na tunataka tuongeze kasi ya kukabiliana na tatizo hilo tumeona tuiondolee wizara hii mzigo wa umwagiliaji ili ibaki na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama mita 400 kutoka wanapoishi.