Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

Katika hali inayotia matumaini ,mkuu wa serikali kwa mujibu wa NEC, Jk ametangaza serikali mpya ambapo J.P.Magufuli amerudi ofisi yake ya zamani iliyompa umaarufu. Magufuli amerudi wizara ya Ujenzi iliyoundwa baada ya kuua Wizara ya Miundombinu. Naibu waziri Harisson Mwakyembe,naisi katibu mkuu ni Patric Rutabanzibwa. Kweli hii ni "solid ministry" Dr.Magufuli karudi penyewe,ama kweli 'kichaa kapewa rungu' sina maana nyingine ila ni kwamba kakabidhiwa "rungu" analojua kutumia kwa umahiri mkubwa. Pia prof.ANA Kajumlo Tibaijuka kapewa makazi,ni dalili nzuri. Kwa aya tu wananchi wanaona kuwa kikwete katumia familia yake ktk kampeni ili akwepe mafisadi kwenye nafasi za uwaziri,kwa ili amejitahidi, Jk sasa atakuwa peke yake kwenye serikali kuu kati ya list ya mafisadi "list of shame" ni maendeleo mazuri. Kwa wizara zingine sina neno kwa sasa maana ni sura mpya ila kama kawaida jk anaweza kuunda tena baraza jipya baada ya miaka2 kama kawaida yake. Mzee sita kapewa Afrika mashariki ,kapozwa ila mama 6 kawekwa pembeni. Binafsi simkubali JK ila kwa baraza ili Nampongeza. Na mwisho namshauri amuondoe makongoro Mahanga maana wananchi hatuna imani naye. JK mkoa wa dsm sasa uweke mkuu wa mkoa msomi,mpaka sasa ilikuwa ikipokezana kutoka kwa darasa la7 mpaka fomu4. Weka msomi apange mji huu. Ni ayo tu,tunasubiri katiba mpya na tume huru!

Magufuli Magufuli Mhh!
hivi mnajua mambo ambayo huyu jamaa anafanya kudhoofisha maendeleo ya jimbo jirani yake la Biharamulo magharibi, ambalo mwaka 1990 lilikuwa moja pamoja na chato (biharamulo mashariki)?
Fuatilieni, fanyeni uchunguzi mtaona/mtagundua alafu muamue kwa niaba ya wote.
 
Back
Top Bottom