Mwisho wa siku tuambizane gharama za mwenge na thamani za miradi iliyofunguliwa kwa kila wilaya

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Ifike mahala tupeane mchanganuo wa gharama za mbio za mwenge wa uhuru na thamani ya miradi iliyofunguliwa kwa kila wilaya. Hii itasaidia kukokotoa kufaulu au kutokufaulu kwa mbio hizo katika eneo husika.Bila kufanya hivyo, tutajikuta tunatumia Shilingi 5 kukirimu mbio za mwenge huku tukifungua miradi yenye thamani ya sh 2. EEE serikali ya Tanzania, funua fikra za viongozi hawa.
 
Utaambiwa ni fedha za wafadhili, hazina mwenyewe, haiulizwi, mambo chungu nzima full ubabaishaji!! Utasikia walimu wanachangia mwenge kumbe ni dili za wakuu wa wilaya na mikoa.
 
ifike mahala tupeane mchanganuo wa gharama za mbio za mwenge wa uhuru na thamani ya miradi iliyofunguliwa kwa kila wilaya. Hii itasaidia kukokotoa kufaulu au kutokufaulu kwa mbio hizo katika eneo husika.bila kufanya hivyo, tutajikuta tunatumia shilingi 5 kukirimu mbio za mwenge huku tukifungua miradi yenye thamani ya sh 2. Eee serikali ya tanzania, funua fikra za viongozi hawa.


ukishajua ndio utafanyaje sasa?mwenge ni sera ya vyama vyote na iko kwenye sheria mama ya nchi unatumulikia wote.
 
ukishajua ndio utafanyaje sasa?mwenge ni sera ya vyama vyote na iko kwenye sheria mama ya nchi unatumulikia wote.

Ikiwa mwenge ulutoka C.C.M Ikawa sera ya vyama vyote:

1. Viwanja vya mipira vilivyokuwa chini ya umiliki wa C.C.M ambavyo bado wanavimiliki navyo viwe chini ya vyama vyote.

2. Radio ya C.C.M iondoe kiashiria chake cha taarifa ya habari kwani ule ni wimbo wa mwenge
 
Mwenge ni upotezaji wa rasilimali za Taifa tu. Hauna tija kwa zama hizi, Watanzania tumeshaunganishwa vya kutosha.
Kama ni mfuatiliaji utagundua kila mwenge unapolala ni lazima asubuhi ziokotwe condoms zilizotumika (kuna sehemu zilifikia ndoo nzima). Sasa tafakari hao ni waliotumia tu, je, ambao hawajatumia? Ni chanzo cha uzinzi!
Hiyo miradi inayozungumziwa haikugharamiwa na fedha za mwenge, kinachofanyika ni uzinduzi tu, ndio maana saa nyingine wanazindua darasa moja la shule, mara hiki mara kile ili mradi wajumlishe na kuwadanganya Watanzania kwamba miradi ya thamani flani imezinduliwa. Hata mwenge usingekuwepo hiyo miradi ingekuwepo.
Kama mnaona mwenge ni nembo ya Taifa basi iendelee kuwa hivyo ila usitembezwe nchini.
My personal take: Mwenge ni moja ya vitu vya kuviondoa kwa kupitia katiba mpya.
 
Mimi nilidhani mwenge huwa unafungua miradi ya wananchi katika ujumla wao kama shule, maji nk kumbe hata miradi ya watu binafsi. Mfano nilikuwa kijiji cha MLANGALI wilayani Ludewa, nilipokuwa nachunguza nyumba ya wageni niliyofikia iitwayo KIZOTA kati ya mbili pale kijijini nilikuta jiwe la msingi lililosomeka "Nyumba hii ya kulala wageni imefunguliwa na kiongozi wa mbio ...." Baadae usiku katika mazungumzo na wenyeji nilionyeshwa mmiliki wa nyumba hiyo.
 
Back
Top Bottom