Nawashauri Viongozi wapya wa CCM kufuatilia kwa kina miradi inayotekelezwa na Serikali katika kuzuia Ufisadi na Rushwa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu Ikumbukwe kuwa CCM ndio iliyounda serikali na siyo serikali iliyo unda CCM, CCM ndio iliyotangulia ndio ikafuata serikali, CCM ndio iliyoomba kura kwa wananchi na ndio iliyosimama katika majukwaa ya kisiasa kuwapigia magoti wananchi kuomba kura,ndio inayofahamu uchungu wa kupata kura moja kutoka kwa mtu,ndio inayofahamu adha na uchungu wa kampeni,Ndio inayokutana na dhoruba zote wakati wa mchakato wa uchaguzi. Hivyo CCM Ni kubwa kuliko serikali na ndio yenye uchungu Na wananchi.

Ndio sababu serikali ikiharibu inalaumiwa CCM,inatukanwa CCM,inazomewa CCM,inasimangwa CCM, inavuliwa sare CCM na inanyooshewa kidole Cha lawama ccm. Na ikifanya vizuri inapongezwa na kusifiwa CCM. Ndio maana inapofanya vizuri Mimi Kama mwanachama Nina wajibu wa kuipongeza serikali yangu kwa kutekeleza vyema majukumu yake katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Hivyo Ni lazima CCM iwe kali,jasiri,Hodari,shupavu na madhubuti katika kufuatilia utekelezaji wa ilani take dhidi ya watendaji wa serikali wanaokwenda kinyume na maadili ya kiutumishi au wanao onyesha ufisadi na ubadhirifu wa Mali za umma,CCM Haipaswi kumwonea haya mtumishi yoyote wa umma na Wala Haipaswi kuwa na unyonge mbele ya mtumishi wa umma au kiongozi yeyote wa serikali. Wala CCM Haipaswi kutishiwa na Mtumishi yoyote wa umma Bali mtumishi wa umma ndio anapaswa kuiogopa na kuiheshimu CCM iliyopewa Dhamana na wananchi kuunda serikali.

CCM inapaswa kuwa Kama mbogo kwa yeyote atakayechezea pesa za umma kwa kutambua kuwa mtu huyu anaichongasha na wapiga kura wake na kuhatarisha usalama wake madarakani,CCM Ni lazima imkemee na kumwonya yeyote atakayemwonea mwananchi wake na itoe maagizo ya kumwajibisha haraka Sana kwa mamlaka yake ya uteuzi au Nidhamu kwa kutambua kuwa atakaye chukiwa Ni CCM endapo hatua hazitachukiliwa haraka,Ni lazima viongozi wa CCm wakifika mahali kila mtu afahamu kuwa wenye Mali wamefika na yeyote aliyegusa Mali zao kwa maslahi yake binafsi hatabaki salama,Ni lazima atasombwa na kimbunga Cha uwajibikaji.

Ndio maana nawashauri viongozi wangu wapya kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inavyotekelezwa na serikali yake katika maeneo yao, kuhakikisha thamani ya Fedha inaendana na mradi Husika na ubora wa mradi, kuhakikisha hakuna ufisadi na ufujaji wa fedha za umma. kuwa na watu wa kiuchunguzi katika kufanya tathimini ya miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na serikali zinatumika Kama ilivyo kusudiwa. Inakuwa Ni aibu fedha za umma zinatafunwa na wao wapo au wanasubiri mpaka mbio za mwenge zianze na kupita katika maeneo yao na kubaini ufisadi wakati wao walipaswa kuwa wa kwanza kufahamu na kuagiza hatua za kuchukuliwa kwa mamlaka. hawapaswi kuwa watu wakushangaa shangaa pale unapoibuliwa ufisadi kana kwamba hawaishi maeneo hayo Bali wanapaswa kuwa Kama Rejea juu ya hatua za kitaarifa zinazokuwa zimetolewa ili zishughilikiwe.

Wananchi wanaumia Sana wanapoona wanalipa Kodi,ushuru na tozo mbalimbali halafu wanasikia kamradi ka kawaida kamekomba mabillioni ya Fedha yasiyoendana na uhalisia au ubora wa kazi au mradi Husika. wananchi wanaumia Sana,wanachama tunaumia Sana na vijana Ndio tunaumia zaidi kwa kuwa tunakuwa tunatamani tungepewa pesa hizo Kama mitaji yetu tuendeleza hata kilimo Bora na Cha kisasa kuliko tunavyotegemea damu zetu katika kulima mashamba yetu. Wananchi wakigundua ufisadi wanahuzunika na kukatishwa Tamaa Sana ya kulipa hata tozo maana wanakuwa wanaona ni Kama wanalipa ili kuwafaidisha wachache kuneemeka na jasho letu,wananchi wanasikitika na kujenga chuki kwa chama na serikali kwa uzembe wa watu wachache. Wanakuwa wanatamani hata kukwepa Kodi,wanakuwa hawapo tayari hata kudai risti madukani kwa kuwa wanaoona mbona Ni Kama wachache waneemeka na kuishi utafikiri wapo paradiso na Dunia ya peke yao? Wanapungukiwa hata na uzalendo wa kutamani kulipa kwa hiyari yao.

CCM yangu chini ya uongozi shupavu wa mama Samia isikubali hili,isiruhusu hili,isitoe mwanya katika hili na ihakikishe wabadhirifu wote wanawajibishwa,isimbembeleze mtu yoyote fisadi Wala kumpa nafasi ya pili au kumhamishia mahala pengine kana kwamba huko ndio Shamba la Bibi au ndiko anakopaswa kwenda kula bila kunawa au ndiko ambako watu wa huko hawaumiaa kulipa Kodi au ushuru au tozo. Mtu akiharibu awajibishwe bila huruma kwa kuwa Tanzania tuna hadhina kubwa ya vijana wasomi ambao hawana kazi na wapo mitaani wakivuja jasho muda wote.

Ikumbukwe kuwa wananchi wanalipa Kodi kuijenga nchi yao kwa mikono yao wenyewe,wanalipa ili wapatiwe huduma zilizo Bora,wanalipa ili kuendesha serikali yao. Hawalipi ili wachache waneemeka na familia zao au na mahawala zao au na ndugu zao au na jamaa zao. Viongozi Ni lazima wakumbushwe wajibu wao Mara kwa Mara kazi ambayo inapaswa kufanywa na viongozi wa chama na chama waliopewa dhamana ya kuunda serikali. Ni matumaini yangu kuwa viongozi wapya watawajibika ipasavyo. Ushauri Ni ushauri na ushauri wangu siyo lazima ukachukuliwa wote maana ushauri huwa haulazimishwi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu,: 0742-676627
 
Yaliyosikika Kisarawe hayana afya kwa nchi yetu, lakini yote hayo ni sheria zetu zimtengenezwa kuwa favoour mafisadi
 
Naamini uchunguzi utafanyika na Tathimini ya kina kubaini uhalisia wa mradi na kiasi Cha pesa kilichotumika kukamilisha mradi
 
... majizi #1 duniani yafuatilie miradi kuzuia ufisadi na rushwa! Are you ok upstairs? Kama dishi limeyumba vile!
CCM na serikali yake chini ya uongozi shupavu wa mama Samia haiwezi kumfumbia macho Wala kumwacha salama yayote atakayebainika kuchezea fedha za umma kwa maslahi yake binafsi
 
Ziko tuhuma za rushwa ambazo zimesababisha baadhi ya chaguzi kufutwa naza kutumia sera ni wa dini yetu. Viongozi waliopatikana kwa staili hiyo wataweza kufanya hayo majukumu unayowataka wayafanye?
 
Huu sasa utani,yaani wezi namba Moja wafatilie jinsi wezi wenzao wanavyoiba?Hiii haiwezekani.
 
Ziko tuhuma za rushwa ambazo zimesababisha baadhi ya chaguzi kufutwa naza kutumia sera ni wa dini yetu. Viongozi waliopatikana kwa staili hiyo wataweza kufanya hayo majukumu unayowataka wayafanye?
Viongozi wote waliochaguliwa wamechaguliwa kwa sifa zao za kiuongozi na siyo Dini Wala kabila la mtu. Ndani ya CCM kinachoangaliwa Ni uwezo na sifa za mtu kiuongozi na uwezo wa mhusika kumudu majukumu katika nafasi husika
 
Kiongozi kapita kwa rushwa then unamwambia akadhibiti rushwa haya ni maajabu. Hapo unawapa dili za Rushwa wakapige pamoja na serikali
 
Hawa waliozidi wenzao kwa rushwa wakachunguze rushwa? Kuna watu mna vifuniko vya shingo eti?
Hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM na serikali,Hakuna aliye zaidi ya Sheria na katiba yetu,atakayekiuka misingi ya kikatiba na kisheria atawajibishwa
 
Viongozi wote waliochaguliwa wamechaguliwa kwa sifa zao za kiuongozi na siyo Dini Wala kabila la mtu. Ndani ya CCM kinachoangaliwa Ni uwezo na sifa za mtu kiuongozi na uwezo wa mhusika kumudu majukumu katika nafasi husika

Matokeo yanasema maneno tafauti hiki ulicho andika. Hata ukiyapitisha kwenye darubini ya ukweli haya matokeo ya ngazi mbali utakuta kuna sifa microscopic iyotumi ya ni fisafi mwenzetu.
 
Hakika uchawa unalipa nchi hii

Back
Top Bottom