Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,247
Watanzania tunapaswa kubadili mawazo na fikra zetu hasa katika kufukia fedha kwenye ujenzi. Tuna watu wengi wanakosea kujenga kwa kukosa mawazo sahihi au exposure. Tafsi ya nyumba siyo mpangilio wa tofali bali ni muunganiko wa ramani na mazingira ya nje.
Viwanja vya masaki na osterbay vinaweza kuwa kielelezo cha fikra za ujenzi zinavyotakiwa kuwa. Alichofanya mwijaku na kampuni aliyowapa kazi ni aibu kwa karne hii.
Unapoweka malengo yakujenga nyumba hasa ghorofa unapaswa kuanza kuwaza kiwanja, eneo kiwanja kilipo na majirani wanaokuzunguka.
Unapotenga bilion moja ya ujenzi tunategemea kiwanja kitengeewe si chini ya milioni mia na hamsini endapo unataka kupata kiwanja mjini. Jengo la bilioni moja kibongo bongo linapaswa kujengwa kwenye eneo la heka moja endapo utajenga kigamboni ambapo maeneo ni makubwa.
Waliomshauri na kumjengea Mwijaku ndio washauri wa NHC, ambao wanajenga nyumba Tanzania kwenye kiwanja cha Sqmt 200 au 400 kwenye jiji kama Dodoma ambalo linakuwa . Poverty mentality ya wataalam wa ardhi wa nchi imepelekea watu kujenga kwa gharama kubwa lakini hawana uwezo wakupaki magari ishirini au kuwaalika marafiki nyumbani. Unakuwa na nyumba kama ya mwijaku lakini ukialika marafiki mia kuja kwako unalazimika ukatafute ukumbi. Leo Mwijaku akitazama chini akiwa ghorofani anawachungulia majirani.
Nyumba kama ile ingejengwa kwenye eneo sahihi hata wafanyakazi wenzake wangetuonyesha garden ya nje na wangepiga picha hata mandhari ya kwenda kwa huyu mjuba.
Nakubali kwamba tunanunua viwanja tukiwa hatujui tunajenga nini ila tunapochora ramani ya nyumba kama ile tutafute kiwanja. Alishindwa nini kwenda kujenga mbweni huko au bagamoyo ?
Nampongeza na niwapongeze wote wenye maono kama yake ila tubadili fikra tuje na maeneo ya uzunguni ambapo tukitaka kutembelea tunakuta miundombinu hata ya usalama ipo sawa.
Povu lazima