Hizi Hapa Ni Hatua Ya Kuomba Na Kupata Kibali Cha Ujenzi Jijini Tanga, Tanzania

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Miundombinu Inayopatikana Wilaya Ya Tanga Jiji.

✓ Bandari inayounganisha nchi ya Uganda na Tanzania. Bandari zipo mbili. Bandari husaidia kwenye usafiri wa Mkonge, kahawa, Pamba na chai.

✓ Reli kutokea Tanga kwenda/kurudi Moshi.

✓ Uwanja wa ndege wa Tanga (Tanga Airport). Ndege kutoka Dar Es Salaam, Pemba, Zanzibar kwenda Tanga.

✓ Vivutio vya utalii. Vivutio ni kama vile Fukwe za Bahari ya Hindi, Galanos hotsprings, Saadani International Parks, URITHI Tanga Museum, Makaburi ya Sakarani, Kisiwa cha Ulenge, Magofu ya Tongoni, Mapango ya Amboni, na Kisiwa cha Toteni.

(d) Hatua Za Kupata Kibali Cha Ujenzi Katika Wilaya Ya Tanga Jiji.

Kibali Cha Ujenzi (Building Permit).

Kibali cha ujenzi ni njia mojawapo ya kupata tathmini ya ongezeko la thamani ya ardhi katika miaka ijayo. Wilaya ambayo vibali vya ujenzi hutolewa kwa urahisi, hupelekea wengi kujenga nyumba zao za kuishi katika eneo hilo.

Hivyo, kiasi cha kodi katika siku husika hushuka kwa sababu ya uwepo wa nyumba toshelevu kulingana idadi ya wakazi kwenye wilaya husika.

Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya:-

Moja.

Kuandaa na kutuma maombi kwa mamlaka ya mji.

Mbili.

Kuandaa na kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika.

Tatu.

Kufuatilia na kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Building Permit (Kibali cha ujenzi) ”.

Kibala Cha Awali (Planning consent).

Tunashauri kupata kwanza kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outland plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.

Sababu za kutangulia kuomba kibali cha awali ni:-

✓ Kuokoa muda wa kurekebisha michoro kwenye hatua za mwisho endapo itaonekana haijafuata mahitaji ya kitaalamu.

✓ Kuokoa gharama za kuandaa upya michezo endapo itaonekana ina kasoro kwenye hatua za mwisho ya uandaaji wa michoro ya kuombea kibali cha ujenzi.

✓ Kufahamu mahitaji ya michoro husika kabla ya kuiandaa.

Jinsi Ya Kuwasilisha Maombi Yako Ya Kibali Cha Ujenzi.

Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe kwa namna hii:-

Moja.

Seti tatu (3) za michoro ya jengo (Archectural drawing).

Mbili.

Seti mbili (2) za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya majengo aina ya ghorofa.

Michoro Yako Inatakiwa Kuonyesha Vitu Hivi.

Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-

Moja.

Namna jengo litakavyokuwa (plans, sections, elevations, foundation and roof plan).

Mbili.

Namba na eneo la kiwanja kilipo.

Tatu.

Jina la mmilikaji ardhi inayohusika.

Nne.

Jina la mchoraji, ujuzi wake na anwani ya mchoraji wa mchoro husika.

Tano.

Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba.

Sita.

Ujazo wa kiwanja (Plot coverage).

Saba.

Uwiano (Plot ratio).

Nane.

Matumizi yanayokusudiwa kwa jengo litakolo jengwa.

Tisa.

Idadi ya maegesho ya vyombo vya moto yatakayokuwepo.

Kumi.

Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) husika.

Kumi na moja.

Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo.

Viambatanisho Vya Maombi Ya Kibali Cha Ujenzi.

Moja.

Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi.

Mbili.

Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo.

Tatu.

Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano, n.k

Nne.

Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo kwa miaka yote.

Tano.

Mabadiliko ya matumizi ya ardhi endapo yapo.

Hatua Za Kufuata Kwenye Mchakato Wa Kupata Kibali Cha Ujenzi.

Hizi ni hatua za kufuata wakati wa kuchunguza michoro ya kuombea kibali cha ujenzi:-

Moja.

Uhakiki wa miliki halali wa kiwanja husika.

Mbili.

Kukaguliwa usanifu wa michoro uliyowasilisha.

Tatu.

Kukagua kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa katika wilaya husika.

Nne.

Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano wa kiwanja (plot ratio).

Tano.

Uchunguzi wa maofisa wa afya.

Sita.

Uchunguzi wa mipango ya utolewaji wa maji taka kutoka katika kiwanja ambacho jengo litajengwa.

Saba.

Uchunguzi wa tahadhali za moto.

Nane.

Uchunguzi wa uimara wa jengo litakalojengwa.

Tisa.

Kuwasilishwa kwenye kikao cha Mipangomiji na Mazingira baada ya kukamilisha taratibu zote.

Kumi.

Ni uandishi na utoaji wa kibali cha ujenzi.

Taratibu Za Kufuata Baada Ya Kupata Kibali Cha Ujenzi.

Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi mijini, ujenzi wowote ambao umepata kibali unapaswa kukaguliwa kwa kila hatua ya ujenzi. Baada ya kupata kibali cha ujenzi mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika:-

Moja.

Kutoa notisi ya masaa 48 kabla ya kuanza ujenzi. Fomu ya notisi hii utapatiwa unapokabidhiwa kibali cha ujenzi.

Mbili.

Kujaza fomu ya ukaguzi na kuwasilisha kwenye ofisi ya ujenzi ili hatua hiyo ya ujenzi unayotaka kufanya ikaguliwe.

Tatu.

Utapatiwa “Certificate of Occupation” baada ya ujenzi wako kukamilika iwapo tu hatua muhimu za ujenzi zimekaguliwa.

Faida Za Kujenga Kwa Kutumia Kibali Cha Ujenzi.

Moja.

Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama.

Mbili.

Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa.

Tatu.

Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa pamoja na kushitakiwa mahakamani, kuvunjiwa jengo na kulipa gharama za uvunjaji.

Kwa ufupi hii ni programu ya leo iitwayo TANGA JIJI REAL ESTATE WORKSHOP. Ninashukuru sana kwa ushirikiano wako. Je unapenda tufanye workshop katika mkoa au wilaya yako?. Toa taarifa kila au kabla ya Jumatatu.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

MUHIMU; Jiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Nitumie ujumbe usemao "WORKSHOP"...

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Hiyo inavyopaswa kuwa ila Kwa ground sasa ukishapeleka michoro yako tu na kulipia, Kwa hizi nyumba zetu za kawaida wanakuambia unaweza ukaendelea wakati kibali kipo kwenye process maana lazima watapitisha kama ilivyo maana wanachojua wao ni wale wataalam kusaini nyuma ya ramani na kugonga muhuri na kupita Kila siku kuchora ukuta X na maneno wasilisha kibali Kwa wale ambao hawana vibali. Mengine kama kukagua Kila hatua Wana skip

Otherwise, uzi mzuri tujitahidi kufuata taratibu za ujenzi
 
Mchakato wa kupata HATI jijini Tanga ni mrefu sana, Ofisi ya Mipango Miji wanajibu simple tu File lako hatulioni njoo Ijumaa ijayo as if wanakupatia Nauli na hata ukirudi wanakuzungusha na hupati msaada wowote
 
Back
Top Bottom