Mwigulu ni almasi ya Tanzania

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Anaandika Chigaitan kutoka KivuDRC.

Leo nitaongea UKWELI Ifike mahali Watanzania tuiamini serikali yetu, tuthamini "Cabinet Ministry ya Taifa letu Kutekeleza SHERIA za taifa letu.

Ifike mahali tuweke imani kubwa kwa MWIGULU.

"Nimewasikiliza kwa makini wafanyabiashara wa Tanzania, wanaodai ni wafanyabiashara wa Kariakoo lakini mkusanyiko ule ulikuwa na taswira ya wafanyabiashara kila kona ya Tanzania.

Shida kubwa ya Tatizo la Tanzania ni Watanzania kuheshimu SHERIA.

Tanzania ni taifa pekee Afrika na nchi zinazoendelea lenye SHERIA bora na rafiki kwa Raia wake.

Utajiri wa SHERIA Tanzania ndiyo Taswira ya mapinduzi makubwa ya kiuchumi Tanzania.

Huwezi kuwa na taifa imara bila kuheshimu SHERIA.

Hakuna mfanyakazi yeyote Tanzania anaiomba "RUSHWA" kwa mifumo bora ya sheria ya Tanzania.

Wafanyabiashara WANAWABEMBELEZA watumishi wa serikali wapewe wa Tanzania wapokee RUSHWA SHAHIDI zipo.

Shida kubwa sana, Shida kubwa sana Watanzania ndiyo viumbe pekee Afrika Mashariki wanaopenda kutoa RUSHWA

Wafanyabiashara wa Tanzania kutoa rushwa ni utamaduni kufanikisha mambo yao .SHAHIDI zipo.

Hakuna na hayupo mtendaji wa serikali Tanzania anaependa kupokea Rushwa. SHAHIDI zipo.

Tanzania ndiyo taifa pekee Afrika linawatumishi wenye weledi na uadilifu wa hali ya juu sana .SHAHIDI zipo.

Matajiri wengi wa wenye asili ya kibantu Tanzania wamepata utajiri kwa njia ya magendo na Rushwa. SHAHIDI ZIPO.

Tafiti nyingi za zinaonesha wafanyabiashara wenye asili ya kibantu Tanzania (na Afrika) wanaongoza kwa:-

(i) Biashara za magendo
(ii) Ukwepaji kodi
(iii) Kutotunza rekodi za kibiashara
(iv) Kuficha takwimu za kibiashara
(v) Udanganyifu uliopindukia

Tafiti zinaonesha biashara za watu wenye asili ya Asia Tanzania ndiyo zinaongoza kwa ulipaji kodi kwa usahihi na uthabiti .SHAHIDI zipo.

Malalamiko ya wafanyabiashara ni mwendelezo wa tabia ya watanzania kutotii SHERIA za taifa lao kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mwigulu ni mzalendo anatekeleza SHERIA kwa maslahi ya taifa lake Tanzania.

Mtu yeyote Tanzania akifanya maamuzi ya kutekeleza sheria nukta kwa nukta anageuka kuwa Audui wa Watanzania.

Mwigulu atachukiwa na hata kulipa gharama kubwa kwa uzalendo wa kusimamia SHERIA .

Tunawajibu wa kuthamini watanzania wachache waliojitolea maisha yao kusimamia SHERIA za taifa letu,

Tusiwavunje moyo tuwape nguvu za kusimamia SHERIA kwa maendeleo ya taifa letu.

Ukimchukua Mwigulu na kumleta hapa CONGO DRC Mwigulu ni Almas kubwa sana kwa Tanzania. Mpeni nafasi awajibike kwa ajili ya taifa lake kusimamia SHERIA.

Kuikosoa makala hii unapasa kwanza uwe mzalendo wa Tanzania, pia uwe na facts za kutosha.

Chigaitan Mapinduzi vijijini

0757900020/0628300020.

copy and share
---------
Lipia sh.20000 upate copy ya kitabu tutekeleze Sheria za Taifa letu kwa kulipa kodi.

Kulipa kodi ni Uzalendo.

Sent from my SM-N950U using JamiiForums mobile app
 
IMG_5244.jpg
 
Hapa Kuna kikao Cha Wataalamu harafu ikiwa ndivyo sivyo atalaumiwa January 😁😁

Ndivyo ilovyotokea Kwa Mwigulu
 
Uwongo mbaya.

Mwigulu kamsaidia sana mama Samia kwenye wakati mgumu sana alipochukua hii nchi.

Ubunifu wake kwenye vyanzo vya mapato na kodi na kulipa madeni kumemsaidia sana Samia kuendesha hii nchi.

Kama Samia angeingia madarakani akaweka waziri mbumbumbu wa Fedha hii nchi ingemshinda hata kulipa mishahara.

Kwa hiyo pamoja na hasira nilizonazo kwa Tozo, bei ya vifurushi kuwa juu, Lakini kimoyomoyo ninasema kuwa Li Mwigulu limemsaidia sana Samia kustay afloat kiuchumi.

Mama asifuate mihemko ya watu, aendelee kumwamini Mwigulu na ampe fursa ya kuonyesha uwezo wake!.
Mwigulu ana akili, yuko smart kichwani Lakini aliniudhi na habari za kutwambia tuhamie Burundi, hiyo haikuwa sawa.

Sasa basi ipo haja ya kuongeza vyanzo vya mapato ili kuepuka kuwatoza watu walewale kodi mara mbilimbili.
Nchi hii inahitaji kuongeza uwekezaji, utalii, mikataba bora ya madini, kuwezesha vijana kuwa enterpreneurs, kufanya overhaul ya mifumo na sheria kandamizi za kikodi na kuziba mianya ya rushwa kwa kupunguza mtu wa kati kwa kufanya computerization ya mifumo ya huduma na manunuzi.

Mwigulu linaweza, liko vizuri
Tuache mihemko ya kisiasa
 
Back
Top Bottom