Mwigulu: Marufuku Wafanyakazi wa Serikali Kushabikia Vyama vya Upinzani!

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Naibu katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi amesema kwamba CCM haitamvumilia Mfanyakazi yeyote wa Serikali atakaueonekana kushabikia vyama vya Siasa hasa Upinzani.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaonya wafanyakazi wa Serikali wanaoshabikia vyama vya siasa kikiwataka kuacha kufanya hivyo.

Kauli hiyo ya CCM imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara), Mwigulu Nchemba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kibaha, mkoani Pwani.

Kiongozi huyo wa CCM alieleza kuwa wapo watumishi wa Serikali, ambao wanawafahamu hawatekelezi Ilani ya CCM inayowataka kuwatumikia wananchi, badala yake hutumia muda wa kazi kushabikia siasa, hasa vyama vya upinzani na kukwamisha nia njema ya CCM na Serikali yake.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Nchemba alisema kwamba watumishi hao walio katika kada mbalimbali wanarudisha nyuma maendeleo.

Alisema kuwa mtumishi wa umma lazima awe anayejali miiko na maadili ya kazi na kwamba kinyume na hivyo, anapaswa kujiondoa mwenyewe kazini.

"Umefika wakati wa kuchagua moja kama chama ni chama na kazi ni kazi. Kuanzia leo akionekana mtumishi wa umma, awe mwalimu au daktari hatavumiliwa," alisema Nchemba akionya.

Aidha, Nchemba alisema pia kwamba CCM kinayumba kutokana na kuwa na makundi ya watu, ambayo yameweka masilahi binafsi mbele.

Alifafanua kuwa ubinafsi huo unakiweka chama hicho katika wakati mgumu huku akiwataka watu wanaotanguliza masiahi binafsi mbele kuacha tabia hiyo, badala yake watangulize masilahi ya chama mbele.

Akizungumzia michango mbalimbali inayotozwa na Serikali katika maeneo ya huduma, alisema kuwa michango hiyo ipo kisheria ili kuwezesha huduma husika kuwa endelevu na zenye ubora, ambapo aliwataka wananchi kuondokana na dhana kuwa kuchangia huduma hizo ni kuibiwa.

Wazee wa Jukwaa la GT EMT Mzee Mwanakijiji Mchambuzi Pasco Nguruvi3 AshaDii na wanasheria kama Lisu na wengine hii imakaaje?

Mipaka ya Kushabikia vyama vya Siasa iko wapi?

1. Je ni Mtu anapohudhuria Mikutano ya Vyama
2. Anapovaa Sare ya Chama
3. Anapokuwa mwanachama
4. Anapopigia kura chama cha siasa?
 
ni mjinga tu huyo na haijui mipaka yake ya utawala yeye amekuwa nani atoe kauli hiyo kuwa naibu katibu mkuu wa chama anaafikiri amekuwa raisi na msemaji mkuu wa nchi?

Anajifurahisha tu huyo hana lolote upeo wake wa kufikiri ni mdogo sana tena sana kwa hiyo anataka kutuambia kuwa watumishi wa umma hawana haki ya kupiga kura?

Na kama wanahaki watapiga kura kwa kutumia chama gani? Sababu kwa kusema hivyo hata yeye mwenyewe hana ruhusa kushabikia vyama coz tayari ni mtumishi wa uma lol mjinga ni mjinga tu hata iweje.
 
Watumishi wa umma hawatakiwi kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa!
 
Anaingilia majukumu ya chief secretary ambae kisheria ndo mkuu wa utumishi, kama ndio viongozi wenyewe hawa akina Nchemba naona mbele ni giza tupu. Ana hoja dhaifu pia anapenda kutumia mabavu badala ya arguement!
 
" A silent fool is termed wise ." sipati ulinganifu kati ya Degree mbili za Mwigulu tena extinction na thinking capacity yake. Awaambie wananchi wakati ni mtumishi pale BOT alikuwa mwanachama wa chama kipi ? Mulugo wakati ni mwalimu / mtumishi alikuwa na kadi ya chama gani ? Tibaigana alikuwa mwanachama wa chama gani ? Ninacho ona hapa ni CCM kuogopa kivuli chake. Watanzania wanasubiria Maisha bora waliyo ahidiwa . Yako wapi? Mbona tunawarudisha watanzania enzi za mkoloni? Rejeeni Katiba Ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 20 (1) ,18 .
 
hii ya mchemba,tusubiri watu kuanza kufukuzwa kazi,maana ukionekana tu kwenye mikutano ya upinzani au kutoa mawazo yanayofanana na wapinzani,kazi huna
 
Watumishi wa umma hawatakiwi kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa!

Mkuu Rejao ni nini Mtumishi wa Uma akifanya ataonekana kwamba Amejiingiza kwenye Siasa
 
Last edited by a moderator:
Mwingilu si bado ni mtumishi wa BOT au alishaacha???

Pia kuna yule mkuu wa mkoa ambae ni mbunge viti maalum

Vipi komba si Capt???
 
Awaambie wananchi wakati ni mtumishi pale BOT alikuwa mwanachama wa chama kipi ? Mulugo wakati ni mwalimu / mtumishi alikuwa na kadi ya chama gani ? Tibaigana alikuwa mwanachama wa chama gani ?

Na mzee Mtei alipokuwa gavana wa benki kuu alikuwa mwanachama wa chama gani?
 
Naibu katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi amesema kwamba CCM haitamvumilia Mfanyakazi yeyote wa Serikali atakaueonekana kushabikia vyama vya Siasa hasa Upinzani.



Wazee wa Jukwaa la GT EMT Mzee Mwanakijiji Mchambuzi Pasco Nguruvi3 AshaDii na wanasheria kama Lisu na wengine hii imakaaje?

Mipaka ya Kushabikia vyama vya Siasa iko wapi?

1. Je ni Mtu anapohudhuria Mikutano ya Vyama
2. Anapovaa Sare ya Chama
3. Anapokuwa mwanachama
4. Anapopigia kura chama cha siasa?

mpumbavu mkubwa huyo tena mshenzi hana adabu hata kidogo jana ameniudhi sana alivyomtukana dr slaa.
 
Back
Top Bottom