Mwangaza
Senior Member
- Feb 26, 2008
- 198
- 64
COPIED FROM FB, by Mtanzania Halisi:
Nukuu ya Samson Mwigamba: -
Kwa sasa napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba safari yangu ya siku 8 iliyoanzia chumba cha mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kuishia Gereza la Mahabusu la Keko ilikuwa ya mafanikio makubwa.
Fanikio la kwanza ni kwamba safari hiyo IMESABABISHA MAKALA ILE ISOMWE NA ASKARI WENGI ZAIDI NA RAIA WENGI ZAIDI. Wakati naandika makala ile nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine askari wengi wa nchi hii hawasomi makala kama hizi kutokana na asili ya kazi yao. Lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine hata raia wa kawaida ni wachache watakaosoma na hivyo ujumbe wangu kuwa umewafikia watu wachache.
Fanikio la pili la safari yangu hiyo ni kwamba imeniwezesha kuishi japo kwa siku kadhaa maisha ya nusu jehanamu iitwayo mahabusu hapa Tanzania. SASA SIOGOPI TENA KWENDA HUKO WALA SIOGOPI TENA KUFUNGWA.
Na fanikio la tatu, nimefanikiwa kujua yale ambayo sikuyajua. Yako mengi yaliyonipeleka huko na ambayo ndiyo niliyoyataka na nitayaandikia ripoti kamili na kuifikisha kunakohusika. Lakini najua wengi mnataka kujua ilikuwaje huko hivyo nitawasimulia kwa kifupi ilikuwaje.
SOURCE: Wameniweka kizuizini lakini mawazo yangu yako huru
MyTake: Kama ilivyodesturi ya Polisi kutekeleza maagizo bila kutathimini madhala yake, Kumshitaki Samson Mwigala ni sawa na "Kumpiga chura teke"