Mwezi kupatwa mfifio kesho usiku Ijumaa Juni 05, 2020 - penumbral lunar eclipse

Je unasisimuliwa na Astronomia (elimu ya nyota) kiasi cha kujitolea muda wa kufuatilia vitu angani?

  • Ndio, ninapenda kiasi

    Votes: 0 0.0%
  • Nidio, ninapenda lakini sipati muda wa kufuatilia

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    7
  • Poll closed .

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Kesho Ijumaa usiku Mwezi utapatwa kififio siku ya tarehe 6 Juni sawa na ile iliyotokea mwanzoni wa mwaka huu Januari 10.

Kiasi cha kufifia kwa mwanga wa Mwezi hakutakuwa kubwa safari hii kwa hiyo ifikapo saa 4:25 usiku Ijumaa hii, kama anga itwakuwa wazi bila mawingu tutaona tofauti kati ya nusu ya kusini ya Mwezi itakayopungua mwanga ikilingnishwa na nusu ya kaskazini ambayo haitafunikwa na kivuli chepesi. Tutathitaji kuangalia kwa uangalifu kwa vile Mwezi hautakuwa mweusi.

Kupatwa kwa Mwezi hutokea siku za Mwezi Mpevu kwa hiyo Juni 5 pia Mwezi utkuwa mpevu na Jua-Ardhi-Mwezi zikiwa katika mstari mnyoofu na Mwezi mpevu utachomoza upeo mara tu Jua linazama upeo wa magharibi.

Siku ya Ijumaa uanze kuangalia Mwezi kabla ya saa 2 usiku ili uweze kulinganisha na ule uliopungua mwanga saa 4:23 ambapo nusu ya upande wa kusini utakuwa umefifia kulingana na nusu ya kaskazini. Anga ikiwa wazi tutaweza kuona tofauti kati ya nusu hizo.

Wakati unaangalia Mwezi angani uelewe kuwa unasogea pole pole angani kutoka upande wa magharibi kuelekea mashariki.

Unaweza kuangalia kupatwa kwa Mwezi moja kwa moja kwa macho bila madhara yoyote kwa vile mbalamwezi ambayo ni mwanga ulioakisiwa na Mwezi ni mdogo sana na wakati wa kupatwa hupungua zaidi.

Kwa siku 15 baada ya Kupatwa kwa Mwezi wa Juni 5, mpangiio wa Ardhi, Mwezi na Jua utaendelea kuwa wa mstari mnyoofu na kwa vile Mwezi utakukwa umeshasogea katika obiti yake na kuwa kati ya Dunia na Jua na kuweza kuzuia mwanga wa Jua itasababisha Kupatwa kwa Jua siku ya tarehe 21 Juni 2020.

Siyo hiyo tu - hali ya kuwa mstari mnyoofu itaendelea kwa siku 15 zingine hadi Julai 5 na kusababisha tena Kupatwa kwa Mwezi siku ya Julai 5, 2020. Ndiyo yalivyo maajabu ya angani.


05 June mchoro kwa kupatwa Mwezi mfifio.png
Sehemu za Dunia kutakoonekana Kupatwa kwa Mwezi Juni 05 2020.png

PENUMBRAL LUNAR ECLIPSE ON FRIDAY, JUNE 05, 2020

There will be a penumbral lunar eclipse on Friday 5th January similar to the penumbral eclipse of January 10 this year.

This time it will be less deep so if the sky is clear we can see only the southern half of the Moon getting slightly darker at 10:25 pm this Friday night. However you will need to observe it closely since it will not become black.

Lunar eclipses occur during Full Moon so June 5th is a Full Moon with Sun-Earth-Moon making a straight line and the Full Moon will be rising from the East horizon exactly while the Sun sets in the West.

To see the difference in the brightness of the eclipsed Moon you should first observe the brightness of the Moon before 8 pm so that you can compare the shading on the Moon with that at 10:23pm when the southern half will be slightly dimmer than the much brighter northern half. We should be able to notice the difference if the sky keeps clear.

When looking at the Moon in the sky, the Moon is shifting very slowly from West going towards East.

Lunar eclipses can be observed safely directly with your eyes since moonlight which is reflected by the Moon is very weak and there is even less light due to the eclipse.

The straight line alignment of Earth, Moon and Sun will be maintained for the next 15 days and the Moon will have moved half way in its orbit and will be between the Earth and Sun, which will result in the annular solar eclipse of 21 June 2020.

In fact this straight line alignment will continue even more until July 5th when after another half orbit the Moon will produce another penumbral lunar eclipse will take place. This shows the amazing wonders of Astronomy.

05 June eclipse diagram.png
 
... vipi tafasiri za kiimani za haya matukio?
Imani inajengwa na namna unvyokabili mambo yanayokupata. Zamani imani ya kupatwa ilitokana na kutoelewa jinsi tukio linavyotokea. Lakini siku hizi tunaelewa zaidi jinsi Jua na Mwezi zinapatwa kwa hiyo sasa inachukuliwa kama alama na ishara ya uwezo wa Mwenyezi
 
Kupatwa kwa jua si kiama
Kweli, kesho itapita bila kiama, na Juni 21 itapita pia baada ya kupatwa Jua, na July 5 pia itapita bila kuona kiama. Kupatwa haileti kiama, labda isemwe siku ya kiama vitu vyote vitapatwa.
 
Back
Top Bottom