Mwenza wa maisha (mume) anahitajika!

Kuna fursa ya ku testiana? Tuone kama tuna match! Otherwise, I'v got everything!
 
Hongera nasreem kwa ujasiri wako ,wewe ni kioo cha jamii naamini utapata tu mume mzuri ,kumbuka wako wengi nyuma yako umewawakilisha hapa hawana uthubutu wa kujaribu .big mom
 
Nahisi kuna kamtihani hapo kwa candidate wako atakayekuoa,maana akisha kula vizuri akiota kitambi utampiga chini?
 
Habari zenu wanajamii.
Jamani maisha ni safari ndefu na inahitaji uvumilivu na ujasiri. Nimetumia ujasiri wangu kwa kujitokeza katika jukwaa hili ili kuweza kupata mwenza ambae atakuwa mume kama Muumba akibariki. Kwa aliye na nia ya dhati haswa naomba tuwasiliane kwa private message.

Sifa zangu
Umri: Miaka 30
Umbo:Ni wa kawaida sana, na kwa wale wanopenda makalio makubwa, mimi sina jamani, ni bora kuwa mkweli!
Urefu: Centimeter158
Rangi: Maji ya maharage
Elimu: Degree mbili
Kazi: Muajiriwa wa serikali
Dini:Islam

Sifa za Mtarajiwa
Umbo: asiwe na kitambi kwa kweli
Urefu: itakuwa vyema kama akinizidi maana isije leta zahma
Rangi: yeyote
Elimu: Degree
Kazi: Ni muhim maana maisha ni magumu sana
Dini: Islam, ila uwe hujaoa!

Najua kunawatakoleta mzaha, ni kawaida sana kwenye jamii. Nipo tayari kwa maswali mtakayoyauliza. Karibuni!

Kwangu mimi hapo ndo umekosa kigezo muhimu sana,otherwise uwe tayari kusalitiwa tu....!!!!
 
hapa mie siwaelewi hawa jamaa , kila mtu akijitokeza anatafuta mtu, anataja elimu ya degree tu ivi jamai tupo wa kweli ?
 
takwimu za hapa zinaonyesha waziwazi, sasa napata shida sana wanaosema kwenye watu watatu, basi wawili ni waislam!.
huyu mdada anakutana na wenye kukidhi vigezo, tatizo kigezo cha dini kinawashinda
 
JF Senior Expert Member sijakuelewa kabisa unapohoji kuwa miaka 30 no fiancee ni issue.Wengine tuna miaka zaidi ya hiyo pia hatuna fiancee na hatujakata tamaa.Wewe unakaa dunia ipi hasa?
Siku hizi kwa taarifa yako wanawake wengi wanachelewa kuolewa kwa sababu mbalimbali.Masomo n.k au tu bado muda aliowapangia Mungu haujafika.Tena nisisahau siku hizi wanaume waoaji hasa na wanaojua maana ya kuoa ni wachache sana.
 
"Umbo: asiwe na kitambi kwa kweli"

itakuwa shida kidogo kwa kijana mwenye umri wa zaidi ya 30 halafu asiwe na kitambi. kama siyo cha beer basi ni cha mahanjumati na mashatashata. au umesahau kitambi ni status!
 
ishu ya dini bana inafanya nikukose. Can't u think otherwise kuhusu hiyo ishu ya dini?
Hizo degree mbili ni za nini, I mean specialization i.e sociology, education, economics...

Unajua Cognitivist, dini kwa upande wangu ni jambo muhimu sana, natamani niwe huru pamoja na familia yetu (na huyu mwenza) katika kuabudu. Hii ni kwa mtazamo wangu tu!
Kuhusu specialization yangu, kwa kweli hizo tarifa zinapendeza kuzitoa kwa yule ambae tutakuwa tumekubaliana. Nakuomba unisamehe kwa hilo!
 
Nasreem, mimi nimefurahishwa na namna unavyojibu maswali, nimevutiwa na nina sifa zote kasoro nimeoa. Ila ningeomba tuwe marafiki tu.. kwani nimevutiwa kuwa na rafiki kama wewe.Kama huna tatizo na hili ni PM.

Ahsante sana Ndukidi, na hakuna taab kuwa na rafiki, nitakutumia PM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom