sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
tuleteeni na gar la riz1 hapa na picha za magar na mijumba ya mafithad vigogo hapa 2one , nan kamzid mwenzie? Cdm vs. Thihiem
Tafadhali mkuu, tumia akili kidogo basi.tuleteeni na gar la riz1 hapa na picha za magar na mijumba ya mafithad vigogo hapa 2one , nan kamzid mwenzie? Cdm vs. Thihiem
Ngongo:
Hii misemo ya Kiswahili:
Kipenda roho hula Nyama mbichi. na
Ukipenda Chongo utaiita Kengeza.
Kwavile jamaa wameipenda CDM basi isijadiliwe wala Isikosolewe!
Hata pesa kama zatokana na Wanachama kuna kila sababu zitumike vizuri, hasa ukizingatia Umaskini na Udhaifu wa Wachangiaji wenyewe.
Ni juzi tu CDM walidai wafuasi wao hawana nauli za daladala. Na kuwataka waunde Maandamano toka watokako kwenda Jangwani.
Kwa hiyo mfano tunaouona hauna tofauti na Ufahari unaopigiwa kelele wa CCM na Serekali yake. Hata Bw Yesu alifundisha kwa Mifano na tena akasema "Utaujua mti kwa Matunda yake"
Kwa hiyo anachotahadharisha Willim ni kuwa " samaki akunjwe angali Mbichi" au Kuna hatari ya kjikuta mmetoa Chui mdogo shimoni na kuingiza Mkubwa!
Haya ndiyo unayoyapenda wewe kama kule Facebook, kusifiwa tu na kuungwa mkono hata kwa upuuzi!! ili kazi yako wewe iwe ni kusema tu pamoja sana, tuko one page na blah blah za kila aina, lakini hoja makini na ngumu unazikimbia.- SALUTE MKUU!
William.
Mkuu Matola, heshma mbele.Haya ndiyo unayoyapenda wewe kama kule Facebook, kusifiwa tu na kuungwa mkono hata kwa upuuzi!! ili kazi yako wewe iwe ni kusema tu pamoja sana, tuko one page na blah blah za kila aina, lakini hoja makini na ngumu unazikimbia.
Kuna picha ya Baba wa Taifa hapo Juu mwaka 1961 yuko ndani ya Roys Roys mbona usemi alipaswa awe ndani ya Bajaj? jitu kubwa zima lakini hovyoo kabisa.
Kama nyumbani kwangu nina uwezo wa kula nyama, niache kula nyama na kula senene kwa sababu jirani yangu hana uwezo wa kula nyama. Sorry watani wangu wa BKB, nimeweka senene as mfano but najua kwenye protein twaweza kutoka ngoma droo. Mbowe ana uwezo wa kununua hayo magari kwa pesa yake mwenyewe na si ya walipa kodi.
Sidhani kama uongozi wa nchi ni sawa na kampuni binafsi ama familia,ukweli ni kwamba taifa la wananchi masikini,lazima viongozi wareflect hilo.Ndo maana ninaamini uongozi wa umma una miiko yake,na bila kuifuata hatuendi popote.Mwananchi kama ndo anamlipa kiongozi,basi ukweli wananchi wengi hawana uwezo wa starehe,kuishi tofauti na jinsi uchumi wa nchi ulivyo ni unafiki, wizi na usaliti kwa wananchi masikini ambao ndo wengi bongo.
- Unajua kuna wakati huwa ninafikiri nilikuonea kuku-delete kule FB, lakini kila ukiandika pumba zako hapa ninapata faraja sana kwamba sikukosea, kwamba huwa unedna kwenye blogu yangu ni maajbu sana kwa mtu ambaye kila wakati unadai sina uwezo mkuwa wa kufikiri! ha! ha! ha! ha!
- Akili yan gu ipo sawa sawa ndio maana niliamua kuondokana na utumwa wa hirai huko Ughaibuni na kuja nyumbani kujumuika na wananchi wenzangu kujenga taifa letu, badala ya kukaa huko na kulia lia kila siku, aliyechanganyikiwa ni yule anyedai mwingine amechanganyikiwa na bado anaenda kwenye blogu ya aliyechanganyikiwa na yeye ni mzima! ha! ha! ha! yale yale ya mwizi kuamini wengine wote ni wezi kama yeye! ha! ha! ha!
- The New Super blogu, nitakwambia siri behind the scene wanao ongoza kwa kuingia kule ni watu kutoka hapa JF, wakifuatiwa na Facebook, sasa tuna average 4100 peoples a day bado hatujaisha ni siku 10 mtupo hewani, so tupo vizuri na wananchi wanatupa feedback ahhhhhhh they love it, tunachanganya kila kitu, siasa, udaku, warembo, mamen, you name it utapata kule, Otheriwse pole sana naona leo nimewashika pazuri sana mkono kwenye kunde na kwenye nyama, ukombozi mnataka na VX8 mnataka, ha! ha! haviendi pamoja!
- Ngoja nikupe darasa kuhusu commonsense, ukiona mtu amevua nguo huvui nguo na kumkimbiza kama unavyofanya hapa unaachana naye, wengi hapa mmelia sana kwamba sina uwezo wa kufikiri! ha! ha! ha! page karibu 10 sasa kwa ajili ya thread iliyoanzishwa na mtu asiye na uwezo mkubwa wa kufikiri? ha! ha! ha! ha! ha!
- Hivi unajua baada ya Jangwani ilifanyika sherehe kubwa sana nyumbani kwa Mwenyekiti? Ulialikwa? Alilipia nani ile sherehe kubwa vile? Sherehe ya nini hasa kufurahia kuja kujionyesha na ma-VX8? Wewe amuka wewe!
William.
ki.
Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?
- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?
- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!
William.
William,
Naona unasumbuliwa na wivu binafsi. Kama Mbowe alifanya sherehe nyumbani kwake baada ya mkutano wa Jangwani wewe
linakuhusu nini? Yaani unataka kutuaminisha kuwa Mbowe hawezi kugharimia private party nyumbani kwake mpaka ichangiwe na mtu? Basi naona una mengi ya kujifunza bado.
Mzee uko dunia ya ngapi?
Unataka ukomunist wa Castro? au vita kama vya Savimbi?
Siasa za kina Castro na Mao nani anazitaka?
Kama hizo ndizo umerithi, pole sana. Ingia darasani tena!
Tunachotaka ni haki na usawa.
Tunataka uwajibikaji!
Kila mtu mwenye uwezo wa kuwa na VX kwa jasho lake awe nalo, sio kupitia uongozi wa kupeana!
Same here, as in "doubtfulness"hivi wazalendo wa nchi hii bila kujali itikadi zao wanakuelewa kweli?? I doubt
Viongozi wa Chadema wengi wanapenda sana maisha ya kifahari juzi nimekutana na msafara wao Kinondoni magari ya kifahari utadhani wasanii wa Marekani. Mwenye gari la bei rahisi milioni 50..pembeni yangu walikuwaepo wazee wawili wakawa wanaulizana hivi kweli hawa ndio wanaotegemea kuwapa maisha bora Watanzania wakishika dola si ndio itakuwa balaa, nilipowasogelea wale wazee wakakaa kimya.
Hapo kwenye red umenifumbua macho!Tafadhali mkuu, tumia akili kidogo basi.
Kulinganisha hivyo nisawa na kusema "Nani fisadi zaidi", wakati issue ni kwamba hatuhitaji ufisadi kabisa.
Kama ufisadi ungekuwa mchezo wa riadha, basi huwezi kusema eti "Huyu anakimbia zaidi", wakati issue ni kwamba hauhitaji kushiriki mchezo huo wa "Riadha"
Kama nchi yetu ni masikini, ni lazima viongozi wareflect hilo, sisi tunaenda kichwakichwa tu.
Kwenye issue hii, kuna hoja mbili kuu hapa...
Kwanza, watu wanazungumzia zaidi bei za magari hayo bila kuzungumzia gharama za maintenence kama vile wese nk.
Lakini hoja ya pili, ni kwamba magari hayo ni more efficient kuwafikia wananchi wengi ambao kwa Tanzania wengi wako in "rural areas", however on the other hand, hilo linatatiza kwasababu magari hao yako associated na "luxury", na gharama kubwa kuya maintain, so viongozi wanaotaka kuwakomboa wananchi, wangeangalia yenye kuweza kufika rural areas kwa gharama ndogo zaidi, na pesa hiyo itakayo kuwa "saved" from matumizi makubwa, iokoe wananchi masikini kwa njia kama kuwapatia dawa zile hospitali zisizo na dawa, kujenga ama kukarabati barabara mbovu, kuwapatia wananchi maji safi, umeme, ama kuwekeza watu wapate kazi nk,ili uchumi nao usonge mbele. Kwa kifupi,ni magari ya kazi yenye kulingana na uwezo wa watanzania.
Kwani mtu kama akiingia madarakani na akawa na uwezo kama ilivyo kwa Mh Mbowe, basi ina maana ataigawia serikali pesa zake?
Starehe ambazo viongozi wetu wa juu tayari wanazo, hata mwanasiasa tajiri akiingia madrakani, bado ni starehe ambazo yeye ataona ni halali yake, kama aliendesha benz kabla hajawa rais, basi usitegemee ataendesha escudo ama vitara akishapata urais.
Lakini hata ambaye si tajiri akiingia madrakani, atataka na yeye aishi maisha kama ya tajiri mkubwa kuliko wote Tanzania, na pengine kushindana na wafanyabishara matajiri nk.Wengine hata wanalipiza na visasi.
Hilo ni kutokana na mentality kwamba kwenye siasa ndo kwenye dili, "everybodody goes in for themselves"
Utumishi wowote, huendana na pale unapopatumikia, so mtumishi wa serikali ya nchi masikini, ni lazima aendane na wale anaowatumikia na serikali ireflect hayo.
Hata ubepari tunaouvamia, mtumishi hawezi kuishi na kulipwa zaidi ya assets zinavyoreflect...Sisi ni kuomba kila siku lakini angalia kufuru ya viongozi.
Bado tuna kazi sana.
Heshima kwenu wanajamvi,
Mkuu W J M kauliza swali zuri sana bahati mbaya hapewi majibu ana ambulia kejeli na viroja.Wanajamvi wenzangu tuitendee haki JF kama huna uwezo wa kujibu hoja kaa pembeni magauzi ya kweli yatafanikiwa ikiwa tutakubali kukosolewa na kujisahihisha.
CDM leo ni chama cha upinzani kesho kinaweza kuwa chama tawala mambo yanayotendwa na viongozi wake leo yanatoa mwanga wakipewa dola watatutendea nini !.
Tunapinga kwa nguvu zetu zetu serekali ya CCM iachane na matumizi ya magari ya kifahari bahati mbaya mbadala wa CCM naye anatumia magari ya kifahari ?.