Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hai mh. Kwayu akataa kuburuzwa mkurugenzi wake

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
PRESS RELEASE
KUTOKA KWA MWENYEKITI, HALMASHAURI YA HAI
5,SEPTEMBA,2012

MSIMAMO WA MWENYEKITI KUHUSU KUAHIRISHWA KWA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 30,AGOSTI,2012.


Habari zimeenezwa kuwa baadhi ya madiwani, hususan wale wa CHADEMA walisusia kikao cha Baraza la Halmashauri cha tarehe 30.8.2012 na hivyo kusababisha kikao kuahirishwa. Ukweli ni kuwa mimi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai nilikifuta kikao hicho na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai awaarifu madiwani wote juu ya jambo hili. Aidha Mkurugenzi alishauriwa aandae kikao kingine kwa tarehe 5 au 6 Septemba 2012 kwa barua mbili za tarehe 27 na 29 Agosti 2012. Mkurugenzi aliendelea kukaidi agizo na ushauri huo.

Nilisikitishwa sana na barua ya Mkurugenzi ya 29/8/2012 iliyosisitiza kuwa tarehe ya kikao ibaki tarehe 30/8/2012. Hatima yake ni kikao kilichovunjika baada ya Halmashauri kuingia gharama zisizo za lazima.

Mapema mwezi Agosti Mkurugenzi alikataa kwa nguvu zote kushiriki nami kuandaa kikao cha Baraza. Baada ya kushindwa kumpata ofsini au kwa simu yake, nilimwaandikia SMS tarehe 13 August 2012 kumtaka awasiliane na mimi ili kati ya mambo mengine tupange kikao cha Baraza ambacho kingeliwajummuisha madiwani wote. Hakuniona. Badala yake tarehe 14/8/2012 alisambaza barua ya kuitisha kikao cha pre-baraza tarehe 22.8.2012 na kikao cha Baraza tarehe 23.8.2012. Vikao hivi viliahirishwa kwa simu na Mkurugenzi masaa machache kabla ya kikao. Baadhi ya wajumbe walihudhuria wakaambulia patupu. Sababu kubwa ya kuahirisha ilikuwa ni ili kuruhusu baadhi ya madiwani wetu washiriki katika chaguzi za CCM (jumuiya ya wazazi na UWT). Pamoja na udhaifu wa taarifa hizi niliona ni vema wenzetu kushiriki katika chaguzi hizo.

Mnamo tarehe 22.8.2012 Mkurugenzi alisambaza barua za Wito wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Halmashauri wa tarehe 30/8/2012. Mapema 23.8.2012 nilimwendea Mkurugenzi kumshauri asitishe kikao hicho kwa sababu kuu mbili.

1. Unyeti wa zoezi la kitaifa la Sensa na majukumu waliyokabidhiwa madiwani ya kuhamasisha na kufanikisha sensa ya watu na makazi. Hata wakati wa kusambaza barua hizo madiwani wakishiriki na Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine walikuwa katika kazi nzito ya kuhamasisha na kufundisha wananchi maana na umuhimu wa sensa na kuwasihi washiriki kikamilifu. Barua ya tarehe 14.8.2012 iliwataka madiwani wawe na ratiba ya zoezi hilo. Tarehe ya mkutano iliangukia wiki ya sensa. Kwa mtu mwenye akili na uzalendo wa nchi ataelewa uzito wa zoezi hili kwa taifa zima.

2. Mbunge wa Jimbo hangeliweza kushiriki katika kikao hicho cha mwaka. Kwangu mimi Mkutano wa Baraza wa Halmashauri ni jambo muhimu sana. Unajumuisha shughuli zote zilizofanyika tangu Halmashauri iingie madarakani na unaweka malengo ya vipindi vinavyofuata. Mbunge akiwa mwakilishi wa wananchi wote wa Hai bungeni anastahili aelewe hali ya wilaya kwa ujumla wake na hakuna mahali pengine popote atakapoweza kupata undani huo zaidi ya kwenye Baraza la mwaka la madiwani.

Mkurugenzi alipuuza mambo haya yote mawili. Mimi niliona umuhimu wa mambo haya, na kama Mwenyekiti nilimuagiza Mkurugenzi asitishe kikao hicho na kukihamishia wiki ifuatayo baada ya wiki ya sensa kwa tarehe 5 au 6 Septemba.

Baada ya kikao cha tarehe 30/8/2012 kushindwa kufanyika, nilitazamia Mkuregenzi aitishe kikao hicho kwa tarehe nilizomshauri, yaani tarehe 5 au 6 septemba. Hakufanya hivyo. Nilirudia agizo langu mara mbili, moja kwa barua na lingine kwa SMS. Yeye amejibu kwa SMS kuwa ameshamwaandikia mkuu wa mkoa na hivyo anasubiri maelekezo yake.

Shauri la kupanga na kuairisha mikutano ya baraza na mikutano mingine katika Halmashauri ni jambo la kawaida. Ikiwa mkutano wa tarehe 30 ulishindikana, ushauriano kati ya Mwenyekiti na Mkurugenzi ungeliweza kupanga kikao kingine bila malumbano yeyote. Mkurugenzi analifanya hili jambo dogo kuwa mgogoro katika Halmashauri. Kwake kichuguu ni mlima. Isitoshe yeye anapenda kupanga na kupangua mikutano ya Halmashauri mwenyewe na kumwarifu mwenyekiti kwa simu dakika za mwisho. Huu sio utaratibu, wala kanuni wala busara za kuendesha Halmashauri. Kamwe Mkurugenzi hawezi kuwa mwamuzi wa mwisho wa vikao vya Halmashauri.
Kwa kifupi hakuna mgogoro Hai.
 
Viva mzee kwayu, ukweli tunatambua kuwa DED anasukumwa na magamba afanye kikao ili kuzuia maendeleo ya halmashauri. idadi ya madiwani ccm ni kubwa kuliko chadema wilaya ya hai hivyo mbunge akikosekana wao ni wakati mzuri wa kutumia wingi wao kuharibu kazi njema ya chadema. DED wakati huu kakutana na mtu wa busara, hekima na akili. Viva Kwayu. fanya kwa maendeleo ya wananchi na sio kwa upumbavu wa vyama ambayo DED anataka kutuletea
 
Hongera mzee KWAYU,una sababu za msingi kabisa,zenye mashiko,naomba nitoe mfano kwa viongozi kama huyu DED,NCHINI AUSTRALIA kuna majira ya JOTO na BARIDI,kuna aina ya panya wanapatikana kule kwa kugundua mabadiliko ya tabia nchi kipindi cha joto wamekuwa wakikusanya chakula cha kutosha na kutunza kwenye mahandaki yao wakitegemea watakitumia kipindi cha baridi na kweli wamekuwa wakifanikiwa kujinusulu na njaa kwa kipindi chote hicho cha majira ya baridi kwani huwa hawawezi kutoka nje kutokana na baridi kali ambavyo huambatana na barafu
USHAURI:Mkurugenzi atumie taaruma yake vizuri,asikurupuke wala asifate ushauri wa magamba,aige maisha ya hawa panya,asikubali kutumika,asikubali kuzidiwa akili na hawa panya wa AUSTRALIA.NAWASILISHA-SAUTI KUTOKA KANDA YA ZIWA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom