Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi ajiuzulu. Adai Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya maamuzi ya kijuha!

Tangia siku ile Dr. Slaa alijikopesha mamilioni kutoka chadema, ni utaratibu upi uliofuatwa? Chama kina utaratibu wa kukopeshana?
kwakweli ilinishangaza kama hii ya kuongeza posho inavyonistaajabisha.

Hapo ndio unaweza ukawa shangaa vijana wa bavicha hivi kweli Dr slaa kwanini hakurudisha mkopo kwa riba?
Hivi chadema ni chama cha siasa au ni saccos au tawi la Pride Tanzania?

Kuna vijana wengi wa chadema nao wana sifa za kukopwshwa kama Dr slaa lakini ukiwambia wanafungua diary ya matusi.

Cha kushangaza zaidi hawa chadema kila anaye toa tuhuma wana muita muongo au msaliti lakini kila leo watu wanasema hoja zile zile na bado wana tuhaminisha kuwa hao watu ni waongo.

Hivi chama hakina pesa za kujenga ofisi kakini za kumkooesha Dr zipo,wakiambiwa wana ng'aka.

Nadhani Godbless J Lema anaona matunda aliyopanda sasa chama kina sambaratika na sijui atambebea mbereko gani mzee Mtei?
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu suala la kutokuwa na maendeleo huko Lindi na Kigoma, si majungu kama akili yako inavyokutuma we siafu, suala la kuwa nyuma kimaendeleo huko katika mikoa hiyo uliyoitaja lipo kihistoria zaidi. Tafadhali soma historia ya kweli si ile uliyosoma darasani ya upotoshaji.

Hayati Nyerere pia anahusika sana katika kurudisha nyuma maendeleo ya Mikoa hiyo, ukandamizaji wa dhati kabisa ulifanyika toka huko zamani, mathalan uduni wa miundombinu katika mikoa hiyo tangu Tanganyika ipate uhuru, hakuna aliyejali kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na sababu inafahamika ukiangalia population ya maeneo hayo na imani zao.

Kutoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa hiyo ilikua ni tabu sana, walau sasa hivi kidogo mambo yamebadilika, na ndiyo maana watu wa maeneo hayo mara nyingi wamekua hawakubaliani na CCM kutokana na kuwa CCM iliwasahau sana tena ni kwa makusudi kabisa.

Sasa ndugu siafu, ikiwa kusoma hujui basi nitafute nikufundishe historia ya kweli ili upate kufahamu yaliyopo 'under the carpet' kwa miaka mingi.
 
Nimeanza kukosa imani na hiki Chama, natumai kwa mgawanyo huu mpk ikifika 2015 sidhani kama cdm iliyokuwepo miaka miwili iliyopita ndo itakuwa2015, heshima ya kuitwa chama Pinzani na udadi ya wabunge na Madiwani sijui itakuwaje ifikapo2015
 
Mara anasema lile bomu la Arusha kwenye mkutano liliratibiwa na Dr Slaaa,ha ha ha ha ntachoma moto kiofis chenu hata mtaaan kwangu
 
Sisi tumewaonya CHADEMA mapema sana juu ya huu uamuzi wao wa ajabu sana na sasa hili sagga nilinaendelea hivyo ngoja tuone kama watanufaika vipi hapa ila cha msingi Chadema ni kujirekebisha mapema na kuona au kukaa na Zitto Kabwe

Josh,

Huwezi kuwa na maridhiano na mtovu wa nidhamu.Hatua ya Kamati Kuu ni msimamo thabiti.Huwezi kuogopa kuchukua maamuzi kwa sababu ya kuogopa athari.Ukichukua dola kwa style hiyo utaunda serikali ya ovyo kama / kuliko iliyopo
 
Jeshi la polisi limkamate na kumuhoji na pia aeleze ni kwa namna gani alishiriki mipango mibaya kwa nchi na kwanini akae na taaifa za hatari kwa usalama wa nchi bila kuripoti

Haiwezejani akaa na Siri muda Wote huo. Wasipo Muhoji ntajitokeza Hadharani na Kumpeleka Polisi ili akahojiwe na Afande Pasua.
 
Watanzania sikuzote tunakuwa mabwege na tutaendelea kuwa mabwege sababu kwanza umuelewe alichokiongea uyu mtu alafu ndio utoe comet zako sio unakurupuka unaanza kumkashifu na kumuona mdini alichosema watu watano waliochaguliwa wote wakristo kanakwamba chama akina waislamu ila ajalaumu kusema chadema chama cha kidini lakini mkumbuke mtei nae alishawahi kusema tume ya katiba imejaa waislamu nae sio mdini tuache ushabiki sababu siasa ni maisha ya mtu vile vile kauli za matusi azifai wewe kama kweli unakipenda chama chako comet ya msingi
 
Kumbukeni amesema alitokea NCCR mageuzi; huyu sio mtu wa kumuamini ni mchumia tumbo na ndio maana amejikita kwenye mishahara ya hao walioteuliwa!! Nenda mwana kwenda kwani CHADEMA will come out stronger after you masalia are weeded out.
 
Sisi tumewaonya CHADEMA mapema sana juu ya huu uamuzi wao wa ajabu sana na sasa hili sagga nilinaendelea hivyo ngoja tuone kama watanufaika vipi hapa ila cha msingi Chadema ni kujirekebisha mapema na kuona au kukaa na Zitto Kabwe

ni bora haya yamefanyika mapema ili takataka zijiondoe ,huwezi ukawa na chama chenye viongozi wasio na uelewa kama huyu halafu ukategemea chama kukua na kupata mafanikio ,nashauri hali hii iendelee mpka dakika za mwisho ili wajingajinga wote wajiondoe ili wakaanzishe chama chao au wakajiunge na ccm
 
tukianza kuangalia watu kwa dini zao na upande wa nchi walikotokea hii nchi tutaiteketeza.
Ndio maana binafsi sikuunga mkono mzee mtei aliposema waislamu wengi kwenye tume ya katiba.
Tuwakemee wote wenye mawazo haya.sidhani kama nchi zilizoendelea watu wanajadili dini za watu badala ya uwezo.
Bila kujali itikadi ya vyama kataa huu upuuzi.

jamani wanaotaka kuondoka chadema ondokeni sasa.inaonekana mmefuata watu na sio sera.mtuachie chama chetu.ondokeni!!kuna watu wamefukuzwa cdm wanatembea nchi nzima wanakichafua chama.hawajengi walikohamia.nawaonya:kuna siku mtapigwa mawe.watu hawafurahii matendo yenu mkae mkijua.
 
Siku zote maji na mafuta hujitenga! Hongra zako kwa kujitambua kwamba hufai ktk Chadema kwa kuwa unaendekeza Udini. Nenda huko kwa Wadini wenzako ila Cdm ni ya dini zote.

Tunajua huu ni mwanzo tu wa Wale watu 50 na ambao tayari 5 wamekwisha ondolewa ktk waliotajwa ktk ule Waraka wa kuhujumu uongozi halali wa juu wa chama kuendelea kujiondoa wenyewe kabla ya kuondolewa.
CDM ni ya wakristo, usione maji yanamwagika sasa,unadhani waislam ni majuha, sidhani kama mtashinda uchaguzi kwa kura za wakristo tu!
 
Sisi tumewaonya CHADEMA mapema sana juu ya huu uamuzi wao wa ajabu sana na sasa hili sagga nilinaendelea hivyo ngoja tuone kama watanufaika vipi hapa ila cha msingi Chadema ni kujirekebisha mapema na kuona au kukaa na Zitto Kabwe

Lema jana alitangaza maamuzi ya chama kuwa hawawezi kumvumilia zitto na kumbuka kauli ya Godbless J Lema ni sawa na kauli ya Mzee Mtei.

Lema ndio mwenye chama atafanya lolote zitto afukuzwe.

Na kamanda wa lema bwana Mungi amesema kuwa watahakikisha Mbowe anakuwa mwenye kiti hata kwa mtutu.

Kifupi Bwana Mungi katangaza vita ndani ya chadema kwa wale ambao wanaona mbowe hafai.
 
Last edited by a moderator:
Wakubwa,

Saga la kuwavua uongozi zitto kabwe na kitila mkumbo limeendelea kuweka wingu jeusi ndani CHADEMA baada ya muda mfupi uliopita hapa katika ukumbi wa DDC-LINDI kushudia Mtendaji mtiifu wa makao makuu ya CHADEMA ndugu ALLY OMARY CHITANDA ambaye ni MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI KWA SASA na pia ni katibu wa SEKRETARIETI Kutoa TAMKO kali dhidi ya kamati kuu na ofisi anayoifanyia kazi.

Kumbe huyu ni udini ndio unamsumbua?

Hivi DINI ni sifa ya kuwa kiongozi siku hizi? Kaaazi kweli kweli....
 
Nimeanza kukosa imani na hiki Chama, natumai kwa mgawanyo huu mpk ikifika 2015 sidhani kama cdm iliyokuwepo miaka miwili iliyopita ndo itakuwa2015, heshima ya kuitwa chama Pinzani na udadi ya wabunge na Madiwani sijui itakuwaje ifikapo2015

hiki chama hakina shukurani kwa kuwa waislam walijitolea uhai wao lakini leo malipo yake ni kutupwa jalalani.
zitto kabwe ameponea chupuchupu mara saba.kwa ajili ya chadema, leo anaondolewa kwa matusi ya nguoni hadi mama yake anatukanwa.
sio siri ni udhalilishaji wa hali ya juu kabisa kupata kutokea ktk duru za siasa.
 
Back
Top Bottom