This is embarassing and humiliating. Ule ubabe wote wa kuwa Kinara unakuja kunaswa na mtego mwepesi kama huu?
Jamani nyie kina Seleli, Kilango-Malecela, Kimaro na wengine wote mlioanza kukiuka "miiko" ya Chama anzeni kujisafisha na kutoa tongotongo zote la sivyo mtaumbuka kama Mwakyembe!
Haya tuliokurupuka! Mwenyewe amesema! Au ndiyo ana'spin'?
Hatukukurupuka bwana, tulitumia vyanzo halali vya habari kama ambavyo wewe umetumia hii. Tutasubiri counterpunch ya DAWASCO. Kama ni ukurupukaji itakuwa ni DAWASCO au Mwakyembe, so far JF hakuna aliyekurupuka!
Haya tuliokurupuka! Mwenyewe amesema! Au ndiyo ana'spin'?
Katibu Mkuu wa chama chetu huwa anatuasa kila siku kuwa tukitaka kupambana na ufisadi sawasawa ni lazima sisi wenyewe tujitahidi kuwa wanyoofu! Sasa hili Mwakyembe kajiingiza mwenyewe. Hii ya kamati tayari ilishafanya watu wakasahau yale madudu yake ya kutetea mauaji ya Zanzibar, sasa naona amejirudisha mwenyewe na watu itabidi tukumbuke mengi yake!
I'll tell you what will happen:
DAWASCO watamuomba radhi kama siyo leo hii basi mapema wiki ijayo. Kwa sababu in the original story, mama Mwakyembe alienda kutaka huduma ya maji, sasa kama tayari alikuwa na huduma ya maji kwanini alienda kuomba huduma ya maji.
Sasa unaenda una shida ya maji halafu unaambiwa umeshajiunganishia maji na unatakiwa ulipe shilingi laki sita wakati hauna maji utalipa?
DAWASCO wamejiingiza katika mtego wa Agenda 21.
Mwanakijiji,
Mimi nilivyoelewa hiyo habari ni kwamba huyo mama alienda kuhalalisha huduma ya maji toka DAWASCO labda baada ya kusikia heka heka za kata maji.
Akizungumzia hatua ya Dkt. Mwakyembe ambaye ni mbunge wa Mbeya kukutwa amejiunganishia maji, Ofisa Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Badra Masoud, alisema wiki moja iliyopita mkewe alikwenda katika ofisi za kampuni hiyo kwa lengo la kujaza fomu ya kuomba huduma ya maji NDIPO (Msisitizo wangu) alipoelezwa kuwa wamejiunganishia maji isivyo halali.
Bila kumtaja jina lake, Bi. Masoud alisema walipomkatalia kumpa fomu hizo wakimtaka alipe faini kwanza alikataa.
"Kwa kuwa alikataa ndio maana leo hii (jana) tumekuja kumkatia," alisema Bi. Masoud. Alitaja faini aliyotakiwa kulipa kuwa ni sh. 600,000.
Hata mimi nilielewa hivyo hivyo kwamba alitaka kwenda kuhalalisha huduma hiyo. Hata hivyo baada ya kusoma hayo maneno ya Mwakyembe, nimerudi na kusoma original story na inasema hivi na kuthibitisha kuwa tulikosea kufikiri tulivyofikiri kwa sababu of our own prejudices and biases.
Huoni tulikosea kufikiri alienda kuhalalisha huduma ya maji tulioamini wamejiunganishia kinyemela? Story is very clear.
Mkuu,
Hapo patamu kweli kweli. Nijuavyo mimi mheshimiwa Mwakyembe anaishi hilo
eneo lililotajwa. Sasa hapo kumekuja kitu kingine, kwamba huenda huo uwanja sio wa kwake.
Ni mahakama tu inaweza kuamua maana ni ngumu kwa wengine kujua kama hapo ni kwake au sio kwake hata kama anaishi hapo.
Labda angefanunua zaidi kwa kusema yeye nyumba yake ni namba fulani na haidaiwi na hiyo iliyotajwa ni namba fulani na ni ya mtu mwingine.
Wacha tuendelee kusubiri zaidi.
Anachodai Mheshimiwa kuwa mahali penye deni pana banda tu na ni pa mteja wake ambaye ni marehemu! Sasa mwenzetu unatueleza kuwa Mheshimiwa anaishi sehemu hiyo. Tuseme anaishi kwenye hilo banda? Au ndiyo yale ya vijisenti, kasri kuita banda!!!! Mimi nahisi mheshimiwa ana nyumba anayoishi (pengine kapanga), kiwanja na hicho chenye matatizo. kwa sababu dawasco waliona wameishampata ( si unajua utanzaji wa kumbukumbu wa mashirika yetu) mama alipoenda kuomba kuunganishwa kwenye kiwanja chake wakaingia mkenge! Haya tuvute subira maana mkweli atajulikana tu.
Mwakyembe alijiunganishia maji kinyume cha utaratibu,huo ni wizi na ukosefu wa uadilifu,hakutumwa na RA kufanya hivyo,na siyo wakwanza kukamatwa anafanya hivyo na kutangazwa....msiwe double standard kama mtu amekosea na asemwe.
Msimamo wangu juu ya hili ni kwamba kosa ni kosa tu, ukifanya kosa hakuna haja ya kutafuta mchawi.
Wale wote wanaoongoza mapambano na mafisadi lazima wafanye juhudi kubwa kuhakikisha na wao huko nje wanakuwa wasafi kadri iwezekanavyo kwa mazingira ya TZ. Ni sawa na sisi JF, tutakuwa credible kama yale tunayoyapinga, tutayapinga kwa kila mtu bila kujali chama na kuhaki,kisha sisi wenyewe sio vifisadi wadogo.
Hata kama nia ya ku-report hii taarifa ni ingine, lakini ni aibu sana na ujinga wa hali ya juu kwa mtunga sheria kuvunja sheria. Ni wapi mwisho wa kuvunja sheria ile nchi. Halafu nashangaa watu mnashupalia mambo mengine wakati kuna clear and utter violation of the law hapa.
Mnataka kuleana sio??? hawa wanaojifanya waheshimiwa ndio wanaua nchi kwa kupenda miteremko huku wanavunja vishoka kwenye mashangingi tuliyolipia kodi zetu....Uchafu mtupu!!!
Dr. Mwakyembe na wenzie watengeneze mambo yao kwani watakapobanwa (na tulionya hili tangu Februari) wasije kulalamika kuwa wanaundiwa "mizengwe" au kuna watu wanajaribu kuwatafuta ubaya.
Hata kama nia ya ku-report hii taarifa ni ingine, lakini ni aibu sana na ujinga wa hali ya juu kwa mtunga sheria kuvunja sheria. Ni wapi mwisho wa kuvunja sheria ile nchi. Halafu nashangaa watu mnashupalia mambo mengine wakati kuna clear and utter violation of the law hapa.
Yeye (Mwakyembe) kafanya kazi yake. Nampongeza kwa hilo. Tatizo zi kukatikwa maji. Huyu bwana ambaye Watanzania walianza kujenga imani juu yake kwa kuonekana ni muadilifu kumbe sivyo. Amejiunganishia maji kwa njia za panya na kisha kaminya kulipa bili. Hapa inaonyesha ni jinsi gani Wabongo tunatisha. Yaani kila mtu akipata upenyo kidogo tu anakwiba. Wengine wanaonekana wasafi tu kwa vile hawajapata nafasi ya kufisadi.
Wanaomtetea Mwenyekiti wa Richmond siwaelewi kabisa. Kama habari za kukakiwa maji na sababu zilizotolewa na DAWASCO ni za urongo basi na ajitetee mwenyewe.
..Dr.Mwakyembe yeye ni mwanasheria aliyebobea, mtetezi wa umma, anayepiga vita ufisadi, dhuluma, na uhujumu uchumi. haitegemewi kabisa mtu mwenye sifa asilipe bili zake kwa vyombo vya umma.
Hakuna anayekataa hapa kuwa Dr.Mwakyembe kaenda kinyume na sheria ya kuunganishiwa maji kama ilivyodaiwa
This is embarassing and humiliating. Ule ubabe wote wa kuwa Kinara unakuja kunaswa na mtego mwepesi kama huu?
Nakubali lakini ukweli kuwa reaction yetu ya mwanzo was so one sided and condemning which was unfair. Nadhani next time tujitahidi kuwa more balanced. Binafsi nimeshajifunza hilo. Let me remind you how we reacted:
sasa katika haya yote, ni wapi kuna fairness or any sense of balance? Je haioneshi kuwa sisi tunajiona ndio wenye haki zaidi na hatuna "room" for mistakes or a sense of "wait a minute, lets hear Mwakyembe before we make any judgement"? doesn't this show our own sense of twisted arrogance and self-importance? I know I was wrong.
Mwanakijiji,
JF sio gazeti au radio. Naamini muundo wetu wa sasa ni bora zaidi kuliko tukianza kujifanya waandishi wa habari wa kusomea.
Hii ya kwetu ni citizen journalism.
Kuna wakati tutakosea lakini pia kuna mara nyingi tutapatia. Ni muhimu pale tunapokosea kukubali tumekosea hata kama anayesemwa na fisadi Chenge.
Tukitaka tupate uhakika wa 100% kabla ya kuandika, JF itapoteza lengo lake
la kukusanya, kuchambua na kuiwakilisha habari kwa haraka iwezekanavyo.
tatizo haliko kwenye kuripoti habari, nadhani habari zinakuja sawasawa tu na hilo linafaa.. la maana ni sisi kupima reactions zetu na kukubali kuwa kuna wakati tuna overeact with very little facts na reactions zetu zinaongozwa na our own prejudices and biases to the point that we present them as authoritative. Inapohusu character ya mtu, we have to be measured. Tukubaliane kuwa reaction yetu kuhusu Mwakyembe was unfair, biased, and indeed unfounded. Na huo ndio uungwana.
Nadhani hata kichwa cha habari kibadilishwe, aidha kwa kuongeza alama ya kuuliza au kwa kukibadilisha kabisa ili kireflect upande wa pili wa hoja za Mwakyembe pia kuliko kilivyo sasa ambapo kinaonekana kuwa ni factual which is not.
Kwanini hatutaki kujihukumu wenyewe kwa makosa yetu na tunataka kuwalaumu wengine. Why are we so harsh on others but lenient on ourselves. We messed up big time and we have to own up to that. Huko ndiko kumkoma nyani giledi siyo nyani wa wengine tu hata wa kwetu.
I own up to my own mistakes. I over reacted and I'll try do do better next. Wengine muamue wenyewe lakini ukweli unabakia pale pale we overreacted without any basis.