Mbunge Kishimba: Viongozi Tumieni Maji ya Miradi Mnayozindua Badala ya Maji Ya Chupa Ili Wananchi Wawe na Imani Nayo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Mbunge wa Kahama Jummane Kishimba amekemea tabia ya Viongozi kuja na maji ya dukani kuzindua miradi ya maji ya Wananchi akisema huo ni ubaguzi.

Bwana Kishimba amesema Ili Wananchi Wawe na Imani na usalama wa Maji yanayozinduliwa kwenye miradi inatakiwa Viongozi wawe Wanakunywa maji hayo hadharani badala ya maji ya dukani.
---
MBUNGE wa Kahama, Jumanne Kishimba amewataka viongozi wanapokuwa katika hafla ya kuzindua miradi ya maji wahakikishe mezani wanakuwa na maji kutoka kwenye chanzo wanachozindua na sio kutumia maji yanayouzwa madukani.

Amesema, kufanya hivyo kutawafanya wananchi kuyaamini maji yanayozunduliwa kuwa ni salama na safi kwa matumizi kuliko wanavyofanya hivi sasa kuwa na maji ya dukani mezani huku wananchi wakitumia maji ambayo viongozi wao hawajayatumia.

Kishimba ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa mradi wa maji wa kata ya Isagehe uliogharimu kiasi cha Sh.milioni 946.197 na unatarajia kuwanufaisha wakazi zaidi ya 15,000 na mpaka sasa jumla ya wananchi 59 wamepata huduma hiyo majumbani.

“Mheshimiwa Waziri wetu nimepenyezewa jambo hapa na wananchi kuwa kwanini viongozi wanaozindua miradi ya maji juu ya meza zilizopo mbele yao huwa na maji ya kununua, kwanini wasiwe na maji au kutumia maji yanayotoka kwenye chanzo kinachozunduliwa”Anahoji Kisimba.

Waziri wa Maji Juma Aweso akizundua mradi huo amesema, siku zote anapozindua miradi ya maji vijijini huwa lazima ayatumie kwanza kwa kunywa ili kuwaaminisha wananchi kuwa ni safi na salama kwa matumizi na kumuondoa hofu mbunge kuwa maji yaliyopo mezani ni kwa ajili ya picha tu.

My Take
Kishimba ana akili sana ,naunga mkono hoja vinginevyo inaonekana hayo sio maji safi na salama ndio maana wanakwepa.
 
Kishimba anaakili ya kufikili mbali zaidi. Kiujumla maji yanasambazwa nchini ni vema yakawa yanathibitishe na viongozi ili kuwapa imani wananchi kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.
 
MBUNGE wa Kahama, Jumanne Kishimba amewataka viongozi wanapokuwa katika hafla ya kuzindua miradi ya maji wahakikishe mezani wanakuwa na maji kutoka kwenye chanzo wanachozindua na sio kutumia maji yanayouzwa madukani.
Huyu jamaa ana hoja ya msingi sana, ili kama kufa tufe wote
 
Kama waziri kasema hayo maji ni safi na salama basi Kishimba yuko sahihi kumlazimisha ayanywe. Nadhani maji safi na salama huwa yanapatikana Moshi na Sumbawanga. Yaani unaweza kuchota bombani na kuyanywa.
 
Waziri ndo atakuwa tbs au tfda
 
Mbunge wa Kahama Jummane Kishimba amekemea tabia ya Viongozi kuja na maji ya dukani kuzindua miradi ya maji ya Wananchi akisema huo ni ubaguzi.

Bwana Kishimba amesema Ili Wananchi Wawe na Imani na usalama wa Maji yanayozinduliwa kwenye miradi inatakiwa Viongozi wawe Wanakunywa maji hayo hadharani badala ya maji ya dukani.
---
MBUNGE wa Kahama, Jumanne Kishimba amewataka viongozi wanapokuwa katika hafla ya kuzindua miradi ya maji wahakikishe mezani wanakuwa na maji kutoka kwenye chanzo wanachozindua na sio kutumia maji yanayouzwa madukani.

Amesema, kufanya hivyo kutawafanya wananchi kuyaamini maji yanayozunduliwa kuwa ni salama na safi kwa matumizi kuliko wanavyofanya hivi sasa kuwa na maji ya dukani mezani huku wananchi wakitumia maji ambayo viongozi wao hawajayatumia.

Kishimba ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa mradi wa maji wa kata ya Isagehe uliogharimu kiasi cha Sh.milioni 946.197 na unatarajia kuwanufaisha wakazi zaidi ya 15,000 na mpaka sasa jumla ya wananchi 59 wamepata huduma hiyo majumbani.

“Mheshimiwa Waziri wetu nimepenyezewa jambo hapa na wananchi kuwa kwanini viongozi wanaozindua miradi ya maji juu ya meza zilizopo mbele yao huwa na maji ya kununua, kwanini wasiwe na maji au kutumia maji yanayotoka kwenye chanzo kinachozunduliwa”Anahoji Kisimba.

Waziri wa Maji Juma Aweso akizundua mradi huo amesema, siku zote anapozindua miradi ya maji vijijini huwa lazima ayatumie kwanza kwa kunywa ili kuwaaminisha wananchi kuwa ni safi na salama kwa matumizi na kumuondoa hofu mbunge kuwa maji yaliyopo mezani ni kwa ajili ya picha tu.

My Take
Kishimba ana akili sana ,naunga mkono hoja vinginevyo inaonekana hayo sio maji safi na salama ndio maana wanakwepa.
pumba tupu, cjui unawaza nini
 
ukiwa Tajiri raha sana, unakuwa na ujasiri wa kuongea mawazo binafsi, kama huyu jamaa!
Ukiwa mbunge mwenye njaa huwezi kutoa challenge kama hizi
Big up
Kishimba
 
Back
Top Bottom