Mwenyekiti Kamati ya Richmond akatiwa maji

...tabu ya wabongo ndio hiyo watu wakisema ukweli mnadai ni siasa sasa wasipolipa maji hiyo DAWASCO itadumu kweli?? M nadhani huu tukitoka kwenye maji ifatie wasiolipa bill za umeme angalau Tanesco nayo inaweza kuzinduka, then EPA, na kwingineko acheni unafiki hakuna politiki hapa ni kazi tu wasipodai kwa njia hiyo mashirika yanakufa nyie ndio wa kwanza kutangaza lawama kwamba wa-tz hawajui kuendesha mashirika yao. Mbona Net group solution walipokata umeme kwenye wizara na sehemu nyingine nyeti walilipa bill zao.... Mnataka kuleana sio??? hawa wanaojifanya waheshimiwa ndio wanaua nchi kwa kupenda miteremko huku wanavunja vishoka kwenye mashangingi tuliyolipia kodi zetu....Uchafu mtupu!!!
 
Hata kama nia ya ku-report hii taarifa ni ingine, lakini ni aibu sana na ujinga wa hali ya juu kwa mtunga sheria kuvunja sheria. Ni wapi mwisho wa kuvunja sheria ile nchi. Halafu nashangaa watu mnashupalia mambo mengine wakati kuna clear and utter violation of the law hapa.

Kitila,

Tatizo la watu wengi hapa duniani ni double standards. Nafikiri ifike mahali tuchukie makosa hata kama yanafanywa na baba, mama au watoto zetu.

Pia mtu ukikosea hakuna haja ya kuanza kutafuta mchawi. Duniani hapa always kutakuwa na motives za watu mbalimbali kufanya wanayoyafanya.
 
Mtanzania na Kitila hapa nakubaliana na nyinyi kwa asilimia 100. Sheria ni sheria na hukata kama msumeno. Bila kujali nani amevunja sheria ni lazima wote tujifunze kufuata sheria hizo.

Hata hivyo linapokuja suala la kuwawajibishwa waliovunja sheria hatuna budi kuangalia kosa lenyewe, mazingira ya kosa na asili ya kosa lenyewe na adhabu yake.

Sasa, pale inapothibitika kuwa kuna mtu (bila kujali mtu huyo ni nani) amejiunganishia maji kinyemela na ameshindwa kuijulisha DAWASCO au kama ni umeme Tanesco, na mashirika hayo yakamfuata na kudai aandikishe na kulipia maji au umeme huyo basi mtu huyo lazima afanye hivyo pamoja na adhabu yake. Anapokataa hata kama ni mtu maarufu kiasi gani basi hatua zinapochukuliwa zichukuliwe.

Lakini kuna vingine ambavyo ni lazima tufikirie hasa inapokuja suala la taasisi nyeti kama Jeshi, Hospitali n.k Ndio maana binafsi niliona ukosefu mkubwa wa kukatia maji Jeshi kwa sababu ya bili ya maji.

Hata hivyo, ni lazima tuangalie ukweli mwingine pia ambao upo na ni sehemu ya maisha ya kisiasa na utumishi. Wapo watu watakaoongozwa na ajenda zao na hivyo ni jukumu la wahusika kusafisha njia zao.

Dr. Mwakyembe na wenzie watengeneze mambo yao kwani watakapobanwa (na tulionya hili tangu Februari) wasije kulalamika kuwa wanaundiwa "mizengwe" au kuna watu wanajaribu kuwatafuta ubaya.
 
Lakini hebu tuangalie habari hii hapa ilivyoanza:

KAMPUNI ya Huduma ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) imemkatia maji aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza Mkataba wa Richmond na kusababisha Waziri Mkuu na mawaziri wengine kujiuzulu, Dkt.Harrison Mwakyembe, baada ya kubainika amejiunganishia maji isivyo halali.

Kilichonishangaza ni kuwa wanapotaja vigogo wengine wote hakuna anayesemwa yeye alifanya nini zaidi ya kutajwa nyadhifa zao au walizowahi kuwa nazo.

Kwanini kwenye kumtaja Mwakyembe badala ya kusema aliyekuwa "Mwenyekiti Kamati iliyochunguza Mkataba wa Richmond na Mbunge wa Kyela".. na badala yake kuchomekea "na kusababisha Waziri Mkuu na Mawaziri wengine kujiuzulu".. what is the relevance of that except ...
 
Kiongozi,
hii tabia ya kuona watu au taasisi fulani ni bora kuliko nyingine ndio inatupoteza wa-tz kama we jeshi au kiongozi na wadhifa wako unajua maji ni muhimu kwako na kuna mtu au taasisi inayokufanya uyapate hayo maji kwa nini usilipe bill zako. ina maana unyeti wa taasisi yako uharibu kazi ya taasisi nyingine?? Kama we ni nyeti tafuta vyanzo vyako vya maji uweke uone kama kuna atakaekuja kukubughudhi.

kama hao watu walijiunganishia maji kinyume cha utaratibu walipe na faini zote bila kujali kuwa ni mheshimiwa nani. Mnatuharibia kazi hata sisi tuna wake na watoto wanategemea ku-survive kwa kazi hii ya kusambaza maji sio kujifanya viongozi au taasisi nyeti lipeni bill zenu..nyie mnapenda kwenu kuchanue kwa wenzenu kusinyae.... Mambo ya kizamani hayo...yaone kwanza
 
Mzee Mwanakijiji,

..nadhani suala la Dr.Mwakyembe kuwa headline hapo ni suala la kibiashara tu. sasa kama yeye ni headline lazima mwandishi ahalalishe hilo kwa kuandika aliyoyafanya hapo zamani kidogo--ripoti ya richmond etc etc.

..katika taarifa inayomtaja Dr.Mwakyembe wako pia vigogo na wengine "mafisadi" kama Ole Naiko.

..Dr.Mwakyembe alifanya kazi nzuri kama mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya richmond. lakini hilo halimfanyi awe juu ya sheria kwamba aache hata kulipa bili kwa vyombo vya wananchi/umma.

..hili suala la mafisadi nadhani limetuelemea baadhi yetu hapa jambo forums. nadhani imepelekea mpaka ku-impair our judgments on issue like civic responsibilities and equality under the law.
 
mimi nimepigasana principle ya kuanika hawa watu wa maji...kama hawajalipa, kateni maji..tatizo ni huduma ya maji, nini itakufanya ulipe?..the fact kama uko kwenye magazeti au the fact kama huna maji. Huduma ya maji ni mkataba kati ya wateja na Dawasa. sisi haituhusu...and i agree kama wana sheria ya kuanika wasiolipa maji basi waanike mafisadi.

Shame watu wana politicize bill za maji...naona ile report iliwagusa sana, sasa hata pumba wataandika tu ilimradi wale waliowaumbua waaibike...

tatizo la haka kamama ni kaandishi habari fulani.......sasa kamepata kazi DAWASCO...........kakikatia watu maji kanatuma habari magazetini......."kwa kutumwa"........wee kamama.........ugomvi wa kisiasa usiuingilie......kaa chonjo...........endelea kufanya kazi yako ya kukata maji kwa wale wasiolipa......Godd work though!!! keep it up!!
Usitake kumponda mama wa watu bure. Yeye kafanya kazi yake. Nampongeza kwa hilo. Tatizo zi kukatikwa maji. Huyu bwana ambaye Watanzania walianza kujenga imani juu yake kwa kuonekana ni muadilifu kumbe sivyo. Amejiunganishia maji kwa njia za panya na kisha kaminya kulipa bili. Hapa inaonyesha ni jinsi gani Wabongo tunatisha. Yaani kila mtu akipata upenyo kidogo tu anakwiba. Wengine wanaonekana wasafi tu kwa vile hawajapata nafasi ya kufisadi.

Wanaomtetea Mwenyekiti wa Richmond siwaelewi kabisa. Kama habari za kukakiwa maji na sababu zilizotolewa na DAWASCO ni za urongo basi na ajitetee mwenyewe.

 
Mzee Mwanakijiji,

..nadhani suala la Dr.Mwakyembe kuwa headline hapo ni suala la kibiashara tu. sasa kama yeye ni headline lazima mwandishi ahalalishe hilo kwa kuandika aliyoyafanya hapo zamani kidogo--ripoti ya richmond etc etc.

Agreed
..katika taarifa inayomtaja Dr.Mwakyembe wako pia vigogo na wengine "mafisadi" kama Ole Naiko.

kwanini hawakusema Ole Naiko ndiye yule aliyesema kuna njama dhidi ya wamasai na inaweza kusababisha genocide?


..Dr.Mwakyembe alifanya kazi nzuri kama mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya richmond. lakini hilo halimfanyi awe juu ya sheria kwamba aache hata kulipa bili kwa vyombo vya wananchi/umma.

Hilo halina mjadala kwangu. Sheria ni Msumeno.

..hili suala la mafisadi nadhani limetuelemea baadhi yetu hapa jambo forums. nadhani imepelekea mpaka ku-impair our judgments on issue like civic responsibilities and equality under the law.

yeah, lakini lazima tuangalie tunapopigana vita ni nani yuko upande wetu. Hata adui anayekusaidia vitani wakati mwingine hupewa afueni. It is not double standard. Yaani unataka kuniambia tumtendee Mwakyembe kwa kosa la nyumba yake sawa na kumtendea Mkapa na Kiwira yake? Kwa idealists yes! kwa mimi ambaye ni realist nasema hapana. Sasa hiyo watu watafsiri vyovyote vile lakini siwezi nikiwa na dhamira safi kumtendea Selelii kwa kushindwa kulipa tiketi ya gari kama kumtendea Balali na BoT, dhamira yangu inanikataza. Ila akifanya kitu ambacho kina uzito unaostahili, sitamuonea aibu mtu yeyote.
 
Mwanakijiji,

..kwasababu Ole-Naiko tumemuweka ktk kundi la mafisadi, basi inategemewa kwamba atakuwa na tabia za hovyo-hovyo kama hizo za kutolipa bili ya maji.

..Dr.Mwakyembe yeye ni mwanasheria aliyebobea, mtetezi wa umma, anayepiga vita ufisadi, dhuluma, na uhujumu uchumi. haitegemewi kabisa mtu mwenye sifa asilipe bili zake kwa vyombo vya umma.

..It is all about kuuza magazeti. Nadhani huko kwenu Ulaya ktk masuala ya TV wanaita ratings.

..sasa kwenye masuala ya kuwa realists vs idealist, nakubaliana na 100%. ndiyo maana wakati mwingine kwenye nchi za wenzetu kuna mambo ya plea-deal ili kuweza kukamata vinara wa uhalifu.
 
mimi nina shaka kama kweli Mwakyembe aliunganisha maji kinyume inawezekana kuwa siasa ya wana Fisadi imeingia kati. Maana DAWASCO wakati fulani ilikuwa chini ya Fisadi fulani.
 
Hakuna anayekataa hapa kuwa Dr.Mwakyembe kaenda kinyume na sheria ya kuunganishiwa maji kama ilivyodaiwa..........na hata katika post zangu zote nimesifu JUHUDI za Badra hilo halina ubishi...........na nilisisitiza pia zoezi linalofanywa na DAWASCO ni muhimu kwa shirika hilo ili liweze kutoa huduma bora........hilo halina mjadala

hilo la siasa kuonyesha kuwa Badra in some way anatumika na mtandao.........guys you have to work it out to connect the dots
 
Lakini hebu tuangalie habari hii hapa ilivyoanza:



Kilichonishangaza ni kuwa wanapotaja vigogo wengine wote hakuna anayesemwa yeye alifanya nini zaidi ya kutajwa nyadhifa zao au walizowahi kuwa nazo.

Kwanini kwenye kumtaja Mwakyembe badala ya kusema aliyekuwa "Mwenyekiti Kamati iliyochunguza Mkataba wa Richmond na Mbunge wa Kyela".. na badala yake kuchomekea "na kusababisha Waziri Mkuu na Mawaziri wengine kujiuzulu".. what is the relevance of that except ...

Mwanakijiji,

Hiyo ndiyo "Kunkoma Nyani Kiladi" na si "Kumkoma Nyani Giladi"!
 
Dk. Mwakyembe naye halipi ankara ya maji (Tanzania Daima)




na Hellen Ngoromera



ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kuchunguza Mkataba wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, anatuhumiwa kulihujumu Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (Dawasco) kutokana na kujiunganishia maji kwa njia ya wizi.

Kutokana na tuhuma hizo, Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM), anayemiliki nyumba hiyo namba 102 iliyopo Kata ya Kunduchi Mtaa wa Kilongawima, ametozwa faini ya sh 796,272 na Dawasco.

Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya kuwang’olea mabomba wadaiwa sugu katika maeneo ya Boko, ambayo iliandaliwa na shirika hilo. Katika operesheni hiyo wateja 11 waling’olewa mabomba yao.

Kwa mujibu wa Dawasco, iwapo Dk. Mwakyembe hatolipa fedha hizo za faini, watamshtaki.

Wengine waliong’olewa mabomba ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel ole Naiko anayedaiwa sh 791,379.60 katika nyumba yake iliyopo Bahari Beach, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Peniel Lyimo (sh 678,295), aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Edgar Maokola Majogo (sh 673,573) na Vincent Mrisho (sh 613,752).

Pamoja na hao, wadaiwa wengine sugu ni Kanisa la Tanzania Christian (TCC) lililoko Boko ambalo linadaiwa sh milioni 1.2, Abubakar Somo, sh milioni 2.4, Stamford Masulube sh milioni 1.9, Miraji Msuya sh milioni moja, Dominic Pallangyo sh 982,003 na Roger Magwaza anayedaiwa sh milioni 1.9.

Meneja Uhusiano wa Dawasco, Badra Masoud, alisema pamoja na operesheni hiyo ya kuwakatia maji wadaiwa sugu kuendelea, lakini wanasikitishwa na kitendo cha viongozi wengi wa nchi kupuuzia kulipia huduma hiyo.

“Bado tunaendelea na operesheni hii, hata hivyo tunasikitishwa na kitendo cha viongozi wetu kutoitikia wito wetu wa kulipia maji, usipolipa hatutajali wewe ni nani, hatutaki kusubiri mzungu aje ndio afanye kazi hii, acheni tufanye kazi,” alisema Badra.

Naye Meneja wa Dawasco eneo la Boko, Ramadhani Mtindasi, alisema wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali ikiwemo mafundi wao kutishiwa kwa silaha.

“Vikwazo ni vingi, wateja wetu hawataki kutulipa hivyo kutufanya tufanye kazi katika mazingira magumu, tunawashauri watulipe ili tuwahudumie.

“Eneo langu lina matatizo mengi, naweza kuwatuma wafanyakazi wangu mara nyingi kufuatilia malipo bila mafanikio, wakati mwingine nalazimika kwenda mwenyewe,” alisema Mtindasi.

Aliwaomba wateja wa Dawasco kuwa na ushirikiano kwa kulipia ankara zao ili kujiepusha na usumbufu unaoweza kuupata.
 
This is embarassing and humiliating. Ule ubabe wote wa kuwa Kinara unakuja kunaswa na mtego mwepesi kama huu?

Jamani nyie kina Seleli, Kilango-Malecela, Kimaro na wengine wote mlioanza kukiuka "miiko" ya Chama anzeni kujisafisha na kutoa tongotongo zote la sivyo mtaumbuka kama Mwakyembe!
 
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kuchunguza Mkataba wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, anatuhumiwa kulihujumu Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (Dawasco) kutokana na kujiunganishia maji kwa njia ya wizi.

Kutokana na tuhuma hizo, Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM), anayemiliki nyumba hiyo namba 102 iliyopo Kata ya Kunduchi Mtaa wa Kilongawima, ametozwa faini ya sh 796,272 na Dawasco..

Key words about his image, Kulihujumu na Wizi! Je kalipa hiyo faini? je hakuna Sheria Dawasco au EWURA wanaweza tumia wakamsweka yeye na wengine ndani? maana wamehujumu!
 
This is embarassing and humiliating. Ule ubabe wote wa kuwa Kinara unakuja kunaswa na mtego mwepesi kama huu?

Jamani nyie kina Seleli, Kilango-Malecela, Kimaro na wengine wote mlioanza kukiuka "miiko" ya Chama anzeni kujisafisha na kutoa tongotongo zote la sivyo mtaumbuka kama Mwakyembe!

Rev. Kishoka,

Ushauri muhimu sana huo. Ukiamua kuwa mtetezi wa Wanyonge na mwedesha vita juu ya mafisadi ni muhimu kujiandaa kuwa msafi hasa. Makosa madogo madogo kama haya yanaweza kukuchafua wakati faida ya ya kuyatenda ni ndogo sana.

Watu kama akina Mwakyembe au Anna Kilango lazima wategemee kwamba watafuatwa sana, hivyo ni muhimu kuwa waangalifu na kuhakikisha wanatimiza yale wanayohubiri.
 
Rev. Kishoka,

Ushauri muhimu sana huo. Ukiamua kuwa mtetezi wa Wanyonge na mwedesha vita juu ya mafisadi ni muhimu kujiandaa kuwa msafi hasa. Makosa madogo madogo kama haya yanaweza kukuchafua wakati faida ya ya kuyatenda ni ndogo sana.

Watu kama akina Mwakyembe au Anna Kilango lazima wategemee kwamba watafuatwa sana, hivyo ni muhimu kuwa waangalifu na kuhakikisha wanatimiza yale wanayohubiri.


Lakini watayasikia au watakuwa na mioyo migumu kama wale waliokubuhu wenye jeuri ya chama ya "vijisenti"?
 
Tunajua sasa hivi kuna Kundi maalum linalipwa kwaajili ya Fitina za kuchafuliana Majina, ila wananchi tunajua Mbivu na Mbichi. Wewe kama ulikuwa na matatizo si kwa ulafi wenu. Dk Mwakyembe kanyaga twende haturudi Nyuma.
 
Tunajua sasa hivi kuna Kundi maalum linalipwa kwaajili ya Fitina za kuchafuliana Majina, ila wananchi tunajua Mbivu na Mbichi. Wewe kama ulikuwa na matatizo si kwa ulafi wenu. Dk Mwakyembe kanyaga twende haturudi Nyuma.

Kanyaga twende baada ya kulipa faini na kulipa bili za maji na umeme kila mwezi pia. Je umeme pia aliunganishiwa na kishoka, na je mita yake inakwenda sawa au spidi imepunguzwa, may be anatumia luku. Kwa upande mwingine naona kama hii issue ni ya mkewe so Mama Mwakyembe watch your step. You reflect the image of your husband.
 
Dk. Mwakyembe: Sijaiba maji na sidaiwi na Dawasco

2008-04-25 09:48:28
Na Mwandishi Wetu


Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harisson Mwakyembe, amekanusha tuhuma za kutumia maji ya Kampuni ya Majisafi na Majitaka (DAWASCO) bila kulipa na kujiunganishia maji bila kibali.

Akihojiwa na Nipashe jana kutoka kwenye jimbo lake la uchaguzi Kyela, Dk. Mwakyembe alisema kwamba nyumba iliyotajwa na maofisa wa Dawasco siyo yake bali ya mteja wake.

Alisema kuwa nyumba inayotajwa ni banda la uwani la mfanyakazi lililojengwa zaid ya miaka 10 iliyopita,na kwamba kiwanja hicho bado hakiendelezwa.

``Nyumba hiyo ya Kunduchi ni banda la uwani na kiwanja ni cha mteja wangu ambaye sasa ni marehemu anayeitwa A.T.X.De Souza ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni ya Zapata Holdings``, alisema Bw.Mwakiyembe.

Katika gazeti hili jana tulimkariri meneja wa uhusiano wa Dawasco,Bi Badru Masoud akidai kuwa kampuni yake inamdai Dk.Mwakyembe sh 700,000 na kwamba amejiingizia maji nyumbani kwake bila kibali.

Dk.Mwakyembe alikanusha vikali madai hayo ya Dawasco na kuwataka waende mahakamani kama ni ya kweli.

``Mimi nakusudia kuwafikisha mahakamani kwa kuchafua jina langu,`` alisema.

SOURCE: Nipashe

Haya tuliokurupuka! Mwenyewe amesema! Au ndiyo ana'spin'?
 
Back
Top Bottom