Mwenye ujuzi wa kuongea na wafu, nataka nikamsalime mama angu

chakula cha watoto

JF-Expert Member
Apr 25, 2023
462
974
Hodi humu! Nimekuja kuomba msaada kama huku Kuna mjuzi anisaidie kupata dawa ya kuweza kunisaidia kuongea na wafu, marehemu mama angu amefariki mwezi ulopita na mimi sikuwepo nilikuwa nje kikazi nikakuta washamzika, nataka niende kaburini kuongea nae kwa Mara ya mwisho hata kwa dakika tatu tu.

Kama humu hayupo basi mnielekeze hata kwa wataalam waganga wa kienyeji jamani.

Asanteni
 
fursa january hii mkuu utatapeliwa amka saa tsa usiku au alfajiri muombee sana mama mkuu fanya kama ibada maana mida ya usiku ndo muda mzuri wa kuongea na muumba wako na hakika hata mama atapata faraja huko aliko muombee tu kwa imani yako
Nahitaji kuzungumza nae mdomo Kwa mdomo akiwa kaburini mm nikiwa nimesimama kando ya kaburi la mama angu
 
Sijui kama upo serious nitakupa mafunzo ni rahisi lakini yanaogopesha. Utafanya astra projection ni mafunzo ya roho kuacha mwili kwa muda.

Ni mafunzo hatari kama umepitia jkt au jwtz kidogo unaweza kumudu kuongea na wafu....ukiwa serious nitafute.

Hii ni kama vita na hakuna vita ndogo muhimu. Kushambulia adui kwa silaha nzito kumzamisha mapema. Kuna faida na hasara zake.... Usicheke tulia uone kesho kuna muda utasinzia lakini sio kulala
 
Na ukimfwata fwata sana huko makaburini au kwa waganga atakuingia mwilini halafu uone shughuli yake.

Mwache aende na safari yake, unachoweza kufanya ni kumtamkia maneno yafuatayo: "MAMA NASHUKURU KWA UPENDO WAKO, ULINILEA NA KUNITUNZA KWA KADIRI YA ULIVYOWEZA, NAKUSAMEHE PALE ULIPOKOSEA, NA MIMI NISAMEHE NILIPOKUKOSEA, NAKUTAKIA SAFARI NJEMA, TUTAKUTANA WAKATI UTAKAPOWADIA. KWAHERI MAMA, NAKUPENDA SANA NAKUOMBA UENDELEE NA SAFARI NYINGINE YA MAISHA HUKO ULIPO.

Hayo yanatosha. Na umuache, vinginevyo yatakukuta makubwa.
 
Hodi humu! Nimekuja kuomba msaada kama huku Kuna mjuzi anisaidie kupata dawa yakuweza kunisaidia kuongea na wafu, marehemu mama angu amefariki mwezi ulopita na mimi sikuwepo nilikuwa nje kikazi nikakuta washamzika, nataka niende kaburini kuongea nae Kwa Mara ya mwisho hata kwa dakika tatu tuu

Kama humu hayupo basi mnielekeze hata kwa wataalam waganga wa kienyeji jamani. Asanteni

Njia rahisi ni wewe pia kufa...
 
Achana na mawazo ya kipumbavu ya waganga sijui wachungaji.

Mimi mama yangu alifariki miaka 7 iliyopita, mara nyingi hua ananitembelea tunaongea kwenye ndoto na siku hiyo nikiamka siku yangu inakua nzuri sana.

Mama yangu endelea kupumzika kwa amani. Jua kijana wako ulieniacha hapa Duniani sitakuangusha, nitaendelea kupigana siku zote za maisha yangu, nimehakikisha yote uliyoniambia nifanye nimefanya na endelea kunitakia afya njema nifanye zaidi.
 
Sijui kama upo serious nitakupa mafunzo ni rahisi lakini yanaogopesha. Utafanya astra projection ni mafunzo ya roho kuacha mwili kwa muda.

Ni mafunzo hatari kama umepitia jkt au jwtz kidogo unaweza kumudu kuongea na wafu....ukiwa serious nitafute.

Hii ni kama vita na hakuna vita ndogo muhimu. Kushambulia adui kwa silaha nzito kumzamisha mapema. Kuna faida na hasara zake.... Usicheke tulia uone kesho kuna muda utasinzia lakini sio kulala
Ngoja nikutafutie pm mkuu tuongee, nipo tayari Kwa lolote
 
Na ukimfwata fwata sana huko makaburini au kwa waganga atakuingia mwilini halafu uone shughuli yake.

Mwache aende na safari yake, unachoweza kufanya ni kumtamkia maneno yafuatayo: "MAMA NASHUKURU KWA UPENDO WAKO, ULINILEA NA KUNITUNZA KWA KADIRI YA ULIVYOWEZA, NAKUSAMEHE PALE ULIPOKOSEA, NA MIMI NISAMEHE NILIPOKUKOSEA, NAKUTAKIA SAFARI NJEMA, TUTAKUTANA WAKATI UTAKAPOWADIA. KWAHERI MAMA, NAKUPENDA SANA NAKUOMBA UENDELEE NA SAFARI NYINGINE YA MAISHA HUKO ULIPO.

Hayo yanatosha. Na umuache, vinginevyo yatakukuta makubwa.
Mkuu nataka kuongea nae Over!
 
Achana na mawazo ya kipumbavu ya waganga sijui wachungaji.

Mimi mama yangu alifariki miaka 7 iliyopita, mara nyingi hua ananitembelea tunaongea kwenye ndoto na simu hiyo nikiamka siku yangu inakua nzuri sana.

Mama yangu endelea kupumzika kwa amani.
Mkuu ulifanyaje Naomba muongozo, Kuna Rafik angu pia huwa anaongea na marehemu mama ake kila baada ya miaka mitatu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom