- Thread starter
- #101
Hivi jamani kumbe kuna baadhi ya watu wanafikiri kwa kutumia makalio eh? Kauli ya Pinda si ya kuungwa mkono kwa namna yoyote ile!
Ni kweli, kwa wapenda fujo na vurugu kama wewe ni lazima uwe na msimamo huo!
Hivi jamani kumbe kuna baadhi ya watu wanafikiri kwa kutumia makalio eh? Kauli ya Pinda si ya kuungwa mkono kwa namna yoyote ile!
Lyagwa,
Umeandika mambo mengi sana tena ya msingi, ukweli ni kwamba nimesoma na nimeelewa mawazo yako kuhusiana na kauli ya Pinda.
Mawazo yako hayana tofauti na yale ya mhe Pinda, ila tu tatizo lilikuwa upotoshaji uliofanywa humu jukwaani, sumu imeshaenezwa humu na ni jukumu langu mimi na yeyote yule mpenda ukweli kuhakikisha sumu hiyo inaondolewa.
Mhe Pinda hakuwa ana halalisha mauaji kama wengi humu wanavyo lazima watu waamini. Mhe Pinda alikuwa akitoa baraka kwa jeshi la polisi liwadhibiti wale tu wakaidi wa maelekezo ya vyombo vya dola.
Kama wewe unaitambua na kuheshimu sheria, basi sheria hiyo hiyo ndiyo ina-regulate tabia ya mwanaadamu, na kama sisi wananchi tukiitii bila shuruti, sidhani kama kungekuwa na vipigo ama kitu chochote kwa polisi dhidi ya raia.
Ukiona hali ipo hivi, ujue tu kuna kundi la watu linataka kuharibu utawala wa rais Kikwete ili uonekane ni bure na hauna maana. Niamini mkuu, hii michezo ipo na ina ratibiwa na vyama vya siasa, lakini kwa bahati mbaya wanao humia ni raia na viongozi wa vyama hivyo wanabaki wanapeta tu!
RAIA, ADUI YETU SIO POLISI, SIO SERIKALI, BALI NI WANASIASA UCHWARA NDIO WENYE KUTUGOMBANISHA NA SERIKALI.
Halafu wewe TAYADI ni mdini, sasa mambo ya maislamu na wakristo yamekujaje hapa?
Piga tu wakifa tutazika.Ni kweli, kwa wapenda fujo na vurugu kama wewe ni lazima uwe na msimamo huo!
Wana-JF!
Ingawa kumekuwa na upotoshaji wa aina yake humu jamvini na kwengineko, kuhusu kauli ya mhe. Pinda, ila ukweli utabaki palepale kuwa mhe. Pinda ametoa kauli sahihi kwa wakati sahihi.
Kauli ya mhe. Pinda imepewa tafsiri ya uongo, kuwa imevunja katiba, hali iliyo pelekea wengi wenu kustaajabu kuwa ina kuwaje mwanasheria mkongwe kama mhe. Pinda kufanya hivyo, ila ukweli wa kauli yake mhe. Pinda ni huu hapa;
Mhe. Pinda alivyosema polisi wapige tu, hakuwa ana maanisha kuwa polisi wapige tu raia hovyo hovyo, lah hasha, bali alimaanisha polisi wadhibiti kwa maana ya kuwapiga raia wenye kukaidi maagizo ya dola.
Wote humu jamvini tunajua ni wajibu wa polisi kulinda raia na mali zao, lakini kwa vurugu za hivi karibuni, usalama wa raia umekuwa hatarini, kutokana na fujo za vyama vya siasa, kwa hali kama hiyo, serikali ni lazima ingetoa kauli, kauli yenyewe ndio hiyo ya mhe. Pinda.
Kauli ya mhe. Pinda imekuwa faraja kwa wapenda amani na utulivu wa hapa nchini, lakini imekuwa ni mwiba kwa wapenda fujo na maandamano yasiyo na tija yoyote kwa taifa.
Mhe. Pinda asante, TAIFA LIPO SALAMA SASA.