Pile F
Senior Member
- Aug 15, 2020
- 121
- 170
Wasalaam wanajamvi... Poleni na majukumu na Mwenyezi awawekee wepesi kila wakati mema yazidi kuongezeka kwa kila mmoja wetu
JE MNAAMINI KUWA KUNA UWEZEKANO HALISI WA KUONDOSHA SILAHA ULIMWENGUNI?
Uwezekano kama huo upo bila ya kujali kwamba tangu mwanzoni kabisa mwa historia yao, binadamu walikuwa wakiendesha vita, wakiunda na kukamilisha silaha za aina mbalimbali, huku serikali zao zikitegemea utumiaji wa mabavu kama chombo cha kudhaminia hali ya kuishi kwa usalama na kupuuza kabisa miito yoyoye ile ya mara kwa mara juu ya uondoshaji wa silaha.
Naam, hivyo ndivyo hali ya mambo hayo ilivyokuwa mpaka sasa, lakini haipasi wala haiwezi kuachiwa kuendelea mbele tena, kwani zama hizi ndizo zama za kupatikana kwa silaha kali sana za KINYUKLIA, jambo ambalo limeyafanya matarajio yoyote yale juu ya utumiaji mabavu kama njia ya kutanzua matatizo ya kimataifa kuwa ni maruirui matupu