Mwanza: Wafuasi CHADEMA waliokamatwa msibani kupandishwa kizimbani

Bavicha bwana ! Watu 500 kwenda kuhani msiba is it possible? Walijiorganize vp?
Kwani msiba huwa unakuwa na kiwango cha watu kuhudhuria. Sasa kama ni mwanachama nwenzao kuna ubaya gani kuhimizana kwenda kwenye msiba wa mwenzao? Hata CCM nao si wanaweza kufanya hivyo? Kosa liko wapi?
 
Mwanza. Wafuasi zaidi ya 10 wa CHADEMA waliokamatwa wakiwa nyumbani kwa mwanachama mwenzao kuhani msiba wanatarajiwa kupandishwa kizimbani muda mfupi ujao.

Watu hao, leo Machi 14, 2018 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza na kuwekwa katika mahabusu mahakamani hapo kusubiri kukamilika kwa taratibu za kimahakama ili wasomewe mashtaka dhidi yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi watu hao walikamatwa eneo la Mabatini Machi 13, 2018 baada ya kutokea kutoelewana kati yao na askari polisi.

Amesema askari hao walikuwa wakifuatilia nyendo za wafuasi hao tangu walipokuwa wakikusanyika kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Mwanza kwenda nyumbani kwa wanachama mwenzao kwa kile kinachodaiwa ni kuhani msiba.

Katika tukio hilo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu zaidi ya 500 waliokuwa kwenye eneo hilo.


Chanzo
: Mwananchi


Siku ya jana, wanachama hao wa CHADEMA walikamatwa na Jeshi la Polisi Mwanza Zaidi soma => Viongozi na wafuasi 20 CHADEMA washikiliwa na polisi
kuhani msiba ni kosa! au kuna tatizo jingine zaidi ya kuhani msiba?
 
Pole pole huwa anafanya nini? Hamkumbuki majuzi tu hapa walikuwa na bongeeeeeeee la mkutano wakajaza kirumba na wakapewa ulizi,
Hii double standard mkija baadae kufanyiwa msilie kama mugabe
 
Daaaah jamani watanzania tumwombee RAISI wetu huenda mambo yakawa kama tunavyotaka
 
Back
Top Bottom