Mwanza: Pinda aagiza waislam kuendelea kuchinja...

Si muda mrefu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amemaliza kikao chake na Masheikh pamoja na Maaskofu hapa Mwanza katika ukumbi wa BoT kuhusu nani achinje kitoweo.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu nani hasa mwenye uhalali wa kuchinja wanyama kati ya Wakiristo na Waislam, Waziri Mkuu, Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja yaendelee hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.

Ameagiza pia kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kamati hiyo iundwe na kufanyakazi zake na kukamilisha haraka sana!.

Zaidi soma -> Pinda ‘aelemewa' mgogoro wa nani achinje nyama | Fikra Pevu

​Mtoto wa mkulima waziri mkuu MIZENGO PINDA ameishiwa cha kuwambia Watanzania.Anataka tuishi kwa mazoea hata kama mazoea hayo hayana tija kwa wakati huu.Tumekupata vizuri mheshimiwa.
 
NYERERE KAFANYA MENGI YA KUUHUJUMU UISLAMU. ILA HILI LA KUCHINJA KALIACHA. HIVI HAMTUMII TU AKILI ZENU??? Ukipendelewa usidai haki.
 
Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?

..wewe ni MAAMUMA! Ni makubaliano tu na wala sio sheria kwamba muislam ndo awachinjie wengine. Mimi kwangu nachinja vizuri tena ndio nazidisha kitimoto ili kupunguza wazee wa kudoea maana mmezoea kuondoka na shingo, vichwa na miguu kwa kisingizio cha haki ya kuchinja! Mkienda Ulaya mnavyokulaga huwa mnachinja nyie?! Fanyeni kazi msizoee vya bure. Wafugaji Tanzania wamejaa bara hasa kanda ya ziwa na Arusha leo hii kuchinja mchinje nyie mliojaa Pwani mliozoea kula samaki, CHINJENI SAMAKI nyama tunachinja wenyewe watafutaji, mmekalia UVIVU TU yakheeeeee nendeni Uarabuni mkageuzwe!!

..wewe MAAMUNA unajua maana ya neno DINI? Dini ni neno lililotokana na lugha ya kiarabu na maana yake ni NJIA na BIBLIA inasema wazi kwamba YESU NDIYE NJIA YA PEKEE ikimaanisha kuwa YESU ndiye DINI PEKEE! Tafadhali soma Injili ya Yohana 14:6 imeandikwa YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
 
suala la mnyama kuchinjwa na pagani wa kiislamu ni mwisho, wakristo kama wanaakili wale kitimoto, kuku na samaki ngombe waachie waislamu, wajinga hao vichwani huwa hawana kitu
 
Shida ya waislamu ni moja tu,ni Elimu dunu, mtu mwenye elimu idogo utamwoa kwenye mambo madogo.
Wakati wenzenu wanakazana kupeleka watoto shule nyie ndo kwanza mnabishaa nani achinje
Kwanza ukichunguza hao wanogangana kuchinja hata nusu kilo hawana uwezo nayo
Jamani hamwezi kupingana na watu wa Mungu, hata kachinje na samaki kaa ikiwezekana lakini kila goti litapigwa kwa yule mwenye jina lipitalo ajina yote Jehova .

Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?
 
Kitu ambacho uislamu unabidi uangalie sasa ni jinsi dunia inavyobadilika na watu wanavyobadilika. TV, internet na vyombo vingine vya habari vinaleta "modernisation" ambayo inatoka kwenye nchi zilizoendelea na bila kuficha itaifanya Uislamu uchakachuliwe vibaya sana. Leo hii kiti moto kinaliwa na waislamu wengi kuliko huko nyuma. Nina rafiki zangu watatu hivi huwa wanapiga kiti moto vibaya sana siku za weekend. Wao husema, Uislamu dini, Kiti moto nyama!!!

Hili swala la kuchinja ni mazoea na upendo tu wa Wakristu na hii ni kwa sababu dini yao inahimiza upendo. Si swala la sheria wala nini. Leo hii Wakristu wakiamua wasile nyama iliyochinjwa na mwislamu, si tu waislamu watakuwa wamenyimwa kipato bali watakuwa wamejitenga au wametengwa!!! Busara inabidi itumike na si kulazimisha.
 
Mi hata sishangai kwani ni kitabu gani cha MUNGU kati ya TORATI, ZABURI, INJILI na QURAN ambacho kimeandika Mkristo achinje ? Na wapi (katika vitabu tajwa hapa juu ) wameandika kuwa UKRISTO ni dini ?

Ushauri wa bure. Hiyo Avatar unayoitumia unaidhalilisha na kujidhalilisha. Weka ya Osama Bin Laden Itakufaa sana kwa fikra zako.
 
Mkuu Nyerere ukristo hauongozwi na kichwa chako, toa andiko linalomtaja ALLAH kuwa ni pepo nipate kukuamini... Sio unajaza pumba zako wakati ALLAH humjui.

Na hivi ndivyo nimjuavyo Allah;

1 Yohana 4


1 Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni. 2 Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.

3 Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!

4 Lakini ninyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu zaidi kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu. 5 Wao husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani wao ni wa ulimwengu.

6 Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.

7 Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.

8
Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo. 9 Na Mungu alionyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake. 10 Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kutuondolea dhambi zetu.

11
Wapenzi wangu, ikiwa Mungu alitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu. 13 Tunajua kwamba tunaishi katika umoja na Mungu, naye Mungu anaishi katika umoja nasi, kwani yeye ametupa Roho wake. 14 Sisi tumeona na kuwaambia wengine kwamba Baba alimtuma Mwanae awe Mwokozi wa ulimwengu.


15 Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu.

16 Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye. 17 Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri Siku ile ya Hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo. 18 Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza uoga wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga huhusikana na adhabu.

19 Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.

21 Basi, hii ndiyo amri aliyotupa Kristo: Anayempenda Mungu anapaswa pia kumpenda ndugu yake.

Ndugu, sasa umeamini?
 
Vitabu vyoote vimeagiza MUISLAM achinjee kwani yeye ndiye mwenye kibali kutoka kwa MUNGU na pia wamefundishwa wakichinja wasemeje..!

Soma Agano la kale utapata majibu
Sio maandiko yenu yanayochapishiwa Dodoma hayoo !

sawa lakini tukiwaleta na nguruwe ntachinja au mliambiwa mtakachochinja lazima mlee??
hivi mabucha na nyama zote mlizowahi kula mna uhakika gani kama zimechinjwa na mwislam??
kama hamuwezi kushuhudia kila mnyama anayechinjwa kama amechinjwa na mwislam basi basi mshakula vibudu sana hasa hapa dsm.
waislam waliosoma na kuelimika wanajua haya hawa waislam wa madrasa ndio wanachafua wenzao.
Imani yako ndio itakayokuponya.
 
Hivi ninyi kama mnajifanya mnamwogopa sana Mwenyezi Mungu na kufuata taratibu zote, kwa nini mnakuwa wepesi wa fujo na kuuwa?

Kama kweli wakristo wao hawafuati taratibu za kuchinja na kwako kinakuwa haramu kwa nini msihimizane msile kilichochinjwa na Mkristo badala ya kuhimizana kufanya fujo na mauaji. Hakuna sehemu inayomlazimisha Mkristo kula kilichochinjwa na Mwislamu bali busara tu inayotumika. Sasa hawa waislamu wasitumie mabavu.


Ni kweli kabisa kutumia mabavu hakukubaliki. lakini kulishwa kibudu kwa kisingizio cha kukosa maandiko yanayolazimisha wakristo kuchinjiwa na waislamu ndo hakukubaliki kabisa........
 
Serekali haina dini..kama hawataki kula hizo nyama nawasile,badala ya kuomba mambo ya msingi kama kusomesha watoto wao,wao hukaa na kuzungumzia mambo ya kipumbavu eti nani achinje nyama..pumbavu zenu sana basi chinjeni na kitimoto(nguruwe),msitake vitamu tu kuku na ngombe

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hivi ndugu unatumia ubongo wako na kuufikirisha kweli au ni ulimbukeni wa kushabikia udini? Hivi siku zote hizi nakula nyama unafikiri nahitaji hiyo yenye udhu au ibada ya mtu mwingine? Kwa mimi binafsi hakuna wa kuniamulia kuwa nyumbani mwako ule nini lakini nilichozungumza au kujadili ni kuwa hoja ya nani achinje ni kuwa na mawazo mgando kwa kuwa hujaanza leo kula nyama, namna gani unakula na inatoka wapi ni juu yako. Hivi hujiulizi kuna waislamu wangapi wanaoita nyama zinazoliwa na wakristo haramu lakini na wao wanakula? ebu fanya utafiti kujua waislamu wangapi wanashiriki kula kiti moto ndio ulete hoja yako isiyo na mashiko. Hata hivyo hapa hatutafuti eti dini gani au dhehebu gani lipo juu kuliko jingine, nao huo ni ujinga lakini tunachojadili nini mustakabali wa Taifa letu katika kuondoa mbegu hii ya udini, siku zote wakristo ulishaowahi kuona wamekataa kula nyama iliyochinjwa na waislamu? Tatizo wenzetu waislamu wachache hawajifunzi kuwa na uvumilivu kwani masuala ya imani yanahitaji kuvumiliana, kupendana na kuheshimiana; hakuna mtu ambaye anaweza kusimama na kudai kuwa dini yangu imechaguliwa na mwenyezi Mungu na kujihesabia haki, huyo ameshapata thawabu yake lakini sisi sote tunaamini katika Mungu ila kama una wasiwasi na Mungu unayemwabudu hapo ndio utaanza kujipigania wewe na nafsi yako
Na hoja inayoongelewa hapa si ya kuchinja wewe kwa ajili ya kitoweo chako.... Elewa!!!! Wewe ndo unamawazo mgando. Kilicholeta mzozo ni kwa mtu asiye na udhu kuchinja kisha na nyama hiyo kuuzwa katika public. Kuna uhakika gani nyama hiyo ikanunuliwa na wakristo tu? Kusema kuwa hata kama unachinja kitoweo kwa ajili yako na familia yako hakuna atakayepiga kelele... Hata kama utaamua kula kinyesi chako mwenyewe hakuna atakayeshughulika na wewe maana kama unafanya bila kuonekana na mtu. Lakini ukikamatwa unakula kishesi chako mwenyewe hadharani unakamatwa!!!! Ni kosa.... Ninyi wakristo shida yenu hampendi kuona waislamu wanakuwa juu yenu, maana mwislamu akichinja DUNIA nzima na madhehebu yote wanakula lakini madhehebu yakichinja mwislamu hawezi kula maana madhehebu mengine yakichinja haihesabiki kama ni kuchinja bali ni kuua. Na ukila nyama yake unakuwa umekula najsi. Kwa hiyo hampendi na mnaona uchungu. Maandiko yapo mengi sana yanayothibitisha hilo ila kwa kuwa ukristo wa sasa unarahisisha mambo hata ukipewa maandiko hayo utayakataa.
 
Hivi ndugu unatumia ubongo wako na kuufikirisha kweli au ni ulimbukeni wa kushabikia udini? Hivi siku zote hizi nakula nyama unafikiri nahitaji hiyo yenye udhu au ibada ya mtu mwingine? Kwa mimi binafsi hakuna wa kuniamulia kuwa nyumbani mwako ule nini lakini nilichozungumza au kujadili ni kuwa hoja ya nani achinje ni kuwa na mawazo mgando kwa kuwa hujaanza leo kula nyama, namna gani unakula na inatoka wapi ni juu yako. Hivi hujiulizi kuna waislamu wangapi wanaoita nyama zinazoliwa na wakristo haramu lakini na wao wanakula? ebu fanya utafiti kujua waislamu wangapi wanashiriki kula kiti moto ndio ulete hoja yako isiyo na mashiko. Hata hivyo hapa hatutafuti eti dini gani au dhehebu gani lipo juu kuliko jingine, nao huo ni ujinga lakini tunachojadili nini mustakabali wa Taifa letu katika kuondoa mbegu hii ya udini, siku zote wakristo ulishaowahi kuona wamekataa kula nyama iliyochinjwa na waislamu? Tatizo wenzetu waislamu wachache hawajifunzi kuwa na uvumilivu kwani masuala ya imani yanahitaji kuvumiliana, kupendana na kuheshimiana; hakuna mtu ambaye anaweza kusimama na kudai kuwa dini yangu imechaguliwa na mwenyezi Mungu na kujihesabia haki, huyo ameshapata thawabu yake lakini sisi sote tunaamini katika Mungu ila kama una wasiwasi na Mungu unayemwabudu hapo ndio utaanza kujipigania wewe na nafsi yako


ndio maana tunasema ni vema waanzishe mabucha yao!
 
Kama Pinda amahalalisha waisilamu wachije, basi wasikatae kutuchinjia "Kiti Moto aka Mkuu wa meza"
 
Back
Top Bottom