MWANZA: Mbowe, Patrobas, Mwakajoka na wanachama kadhaa wa CHADEMA wakamatwa na Polisi

Hata uingereza na marekani kampeni zikianza ndio kuna mikutano, uchaguzi ukiisha watu wanakuwa bize kujenga nchi. We hata miezi 6 haijaisha mamikutano na maandamano kutwa kucha yasiyo na tija! Bungeni wanatukana ovyo, hawatii kanuni za bunge yaani ni ujinga mtupu!

CCM wangekuwa na hata nusu ya UHURU uliopo hizo nchi sidhani kama Tulia angefanya upumbavu ule pale Bungeni
 
Jana,Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho walikamatwa na jeshi la polisi huko Mwanza. Kosa lililoripotiwa ni 'kuwasalimu' watu wa vijiweni. Wakati huohuo,Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe anasakwa na jeshi la polisi.

Kosa linalotajwa kwa Zitto ni kutaka 'kuichambua bajeti ya Serikali ya 2016/2017' .Wachambuzi wa kisiasa wanayaona matukio hayo kama juhudi za makusudi za 'kuwadhibiti' wanasiasa wa upinzani. Zitto amesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge huko Dodoma.

Mikutano yote ya kisiasa (ikiwemo makongamano na kusalimiana kimakundi) kumepigwa marufuku! Ndiyo mambo ya demokrasia? Tenga muda leo uyasome magazeti ya Mwananchi na Mtanzania ya leo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Mzee wangu huko CCM mmekosa kabisa watu wenye busara na hekima??Hivi ndiyo serikali mlitaka iwe hivyo?Ukiona watanzania wanamuona JKN kwenye miembe ujue wamechoshwa na hila za utawala wa mabavu wa CCM.
 
Back
Top Bottom