Mwandishi wa habari akamatwa na TAKUKURU Arusha

Antar bin Shaddad

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
202
101
Leo mjini Arusha majira ya saa 10 za jioni mwandishi wa habari wa kujitegemea Joseph Ngilisho amekamatwa na maafisa wa takukuru kwa tuhuma za kupokea rusha ya shilingi milioni 2 kutoka kwa afisa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hoteli ya African Tulip.

Awali kabla ya kutiwa mbaroni mwandishi huyo aliandika habari katika gazeti la Dira wiki iliyopita kuwa jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki linavuja na limejengwa chini ya kiwango madai ambayo kimsingi yalikuwa ya uongo na baada ya kuandika habari hiyo akawa anampigia simu mhandisi wa jumuiya Dr. Kleruu akimtisha ampe fedha la sivyo ataendelea kuwaandika na ndipo maafisa wa jumuiya wakaripoti Takukuru na mtego wa kumnsa ukaandaliwa hadi jioni ya leo alikuwa bado mahabusu.
 
Takukula nao...hawaoni rushwa kubwa kubwa wanaona hizi za waganga njaa...hiv wanajua thamani halisi za mabomba ya jk ya gas anayotaka kuwachakachua wana mtwara?
 
Wanajulikana hao kwa vibahasha haswa kutoka kwa kile chama cha mabwepande kinawahonga sana wawachafue wenzao,kama vipi amuhonge na huyo takokuru atamuachilia tu....
 
Du hawa waandishi makanjanja mbona wengi tu yaani wao ni kuzusha na kutuacha tukigombana
 
Takukula nao...hawaoni rushwa kubwa kubwa wanaona hizi za waganga njaa...hiv wanajua thamani halisi za mabomba ya jk ya gas anayotaka kuwachakachua wana mtwara?

Nahisi na wewe ni mmojawapo wa hawa WAANDISHI UCHWARA waganganjaa!!!! Badala ya kukemea unaona safi.
 
Nisingependelea kuona anaendelea kuwa rumande, atendewe haki ya kupelekwa mahakamani kama alivyopelekwa mchina na kuhukumiwa akalipa faini ya laki 7 na kuachiwa hivyo na huyu hana kosa tofauti na hilo wakajanjanja wengi, leo anaonekana uchwara kwasababu ameomba fedha ya kujikimu lakini kama issue alioandika ingefuatiliwa inawezekana kuna ukweli ndani yake tisipinge haraka japo anakosa lake lakini sheria zisipindishwe hapo.
 
waandishi wa habari wengi hupenda kuwablacmail watu ili wapate mkate wa kila siku. huwa hawalipwi mishahara hao.
 
Back
Top Bottom