Mwandishi wa habari akamatwa na TAKUKURU Arusha

Kibanga, hiyo ni ajali kazini ila mimi nasimamia zile bahasha halali!.
P.
Nakubaliana na hoja yako ya "ajali kazini" kwasababu kiukweli tasnia ya habari imeoza kwa hilo ingawa mnajiona watakatifu sana na mko mstari wa mbele kuhukumu na kuandika ya wengine. Kukiwa na mwamko wa namna hii mbona watalizwa wengi? Hii ndio staili yao ya maisha wakishajua issue yako iwe kweli au uwongo ni simu na vitisho zitafuata utadhani umemuajiri. Safi sana TAKUKURU wanaoita ni posho ya kujikimu sawa tumewaelewa kwasababu siku zote bata hanyi, huharisha...Mwenye haki ya kunya ni kuku tu.
 
Du hawa waandishi makanjanja mbona wengi tu yaani wao ni kuzusha na kutuacha tukigombana
ndo maana nawachukia, tofauti yao na polisi ni ndogo sana, wao kazi yao kama walivyo polisi ni kupindisha ukweli. I hate them.
 
Hebu watu baki tufanye uchunguzi kwanza si ajabu habari yake ilikuwa ya kweli akatengenezewa ajali kama ndugu yake Jerry pale Kibaha.Kwani hao takohuru ooh sorry TAKOKURU wako kazini kweli?Mbona kama ni bahasha kwa wana habari makanjanja zinatolewa nje nje??Aah waache maskhara bwana.
 
Huu ni mfano halisi wa waandishi wetu, unaandika taarifa siyo kwa kuelimisha bali kukomoa kwa vile tu hauna maslahi nayo. Sasa unalipwa zaidi ya ulivyokusudia. Hivi kama jengo linavuja ni lazima uandike? kwani wenyewe hawaoni kuwa linavuja? na je traarifa hiyo iliandikwa ili imufaishe nani hasa. Maana kama alikuwa na uwezo wa kuongea na mhandisi kuhusu tatizo hilo aliona ugumu gani kumweleza na yakaisha biala kuandika?
 
Kibanga, hiyo ni ajali kazini ila mimi nasimamia zile bahasha halali!.
P.

yaani nilipoona hii thread nikawa najiuliza siyo Pasco au rafiki zake baada ya kuona jina siyo nikategemea kuona mchango wako..nikwambie tu pasco kwa namna unavyopenda kutumika na kupokea rushwa iko siku wata kuzunguka hutoa amini macho yako..vipi wale marafiki zako walokamatwa Monduli bado wananyea debe au ni rushwa juu ya rushwa..
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni kama takrima bunge lilifuta nakutungiwa sheria sasa ni rushwa
Mkuu Mende, zile bahasha za waandishi sio takrima!, ni za logistic support ili kuwezesha hivyo ni bahasha za "uwezeshaji" na hapa naomba nisisitize na ku underline kuwa "hata ikulu inatoa bahasha hizo" na ikitokea kazi ya TAKUKURU inayowahusisha waandishi kupewa "logistic support", "hata TAKUKURU wanatoa bahasha!"

Nakiri kuwa "the dividing line kati ya bahasha za rushwa na za uwezeshaji ni very thin!" ili kujiridhisha which is which, nisome hapa Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...
Pasco.
 
yaani nilipoona hii thread nikawa najiuliza siyo Pasco au rafiki zake baada ya kuona jina siyo nikategemea kuona mchango wako..nikwambie tu pasco kwa namna unavyopenda kutumika na kupokea rushwa iko siku wata kuzunguka hutoa amini macho yako..vipi wale marafiki zako walokamatwa Monduli bado wananyea debe au ni rushwa juu ya rushwa..
Mkuu Crashwise, wakati nilipokuwa mwandishi wa newsroom, bahasha nimezipokea sana!, mpaka sasa mimi ni mwandishi mshauri elekezi na mwezeshaji, ambapo kazi yangu sio tena kupokea bahasha bali kuzigawa!.
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...
Pasco.
 
ndo maana nawachukia, tofauti yao na polisi ni ndogo sana, wao kazi yao kama walivyo polisi ni kupindisha ukweli. I hate them.
Mkuu Ngwendu, hilo tumelizoea, hata humu jf, tunao sio tuu ma haters kibao, tunao mpaka "prophets of the doom" kibao tuu!. Kuna watu wana chuki for a reason na iko justifiable, ila kuna watu wa chuki for no reason at all!. Naomba nikupe ushauri wa bure, chuki ikizidi hugeuga ugonjwa that "eats you from inside!"
Pasco.
 
Mkuu Mende, zile bahasha za waandishi sio takrima!, ni za logistic support ili kuwezesha hivyo ni bahasha za "uwezeshaji" na hapa naomba nisisitize na ku underline kuwa "hata ikulu inatoa bahasha hizo" na ikitokea kazi ya TAKUKURU inayowahusisha waandishi kupewa "logistic support", "hata TAKUKURU wanatoa bahasha!"

Nakiri kuwa "the dividing line kati ya bahasha za rushwa na za uwezeshaji ni very thin!" ili kujiridhisha which is which, nisome hapa Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...
Pasco.

.......

Hizi bahasha hizi zinashusha credibility ya uandishi wa habari, wewe unalipwa mshahara kwa kazi uliyo tuma kwenda kuifanya kwa nini tena upokee hiyo ya uwezeshaji?
 
Nahisi na wewe ni mmojawapo wa hawa WAANDISHI UCHWARA waganganjaa!!!! Badala ya kukemea unaona safi.

Mkuu me ni muuza vocha mtaa wa kati hapo stand kaka..nani asiyejua kwamba kuna rushwa kubwa zipo na hawa takukula wanaziona wanafunga macho...unaongeleaje rushwa bandarin paka makyembe azishtukie wao wap? Uhitaji degree au master. Kutambua hili unless wew ni mbumbumbu...
 
kwahiyo wangemwachia, hapo vipi.

.........

Swala si kumwachia mkuu..tunataka kusikia na mafisadi wakubwa ambao ndio wenye madhara makubwa kwenye uchumi wetu wakikamatwa kwa hali na kasi ya hawa tunaowaita dagaa..
 
Hizi bahasha hizi zinashusha credibility ya uandishi wa habari, wewe unalipwa mshahara kwa kazi uliyo tuma kwenda kuifanya kwa nini tena upokee hiyo ya uwezeshaji?
Mkuu Mende, lets be realistic, wewe si ni unafanya kazi na unalipwa mshahara?, hivi ukisafiri kikazi, unautegemea mshahara wako?.

Hivi ukihudhuria mkutano wa kazini, unalipwa pesa zozote?, na ukihudhuria warsha, semina au makongamano huko jee hali ikoje?.

News is free and will always be free! yaani habari ni bure na siku zote zitakuwa bure!. Hata hizo bahasha za uwezeshaji sio kila habari, lazima iandamane na bahasha, habari zinazoandamana na bahasha ni zile tuu zinazohitaji uwezeshaji, au zile ambazo zimeishatengewa bahasha za uwezeshaji mfano warsha, semina, mikutano na makongamano ambapo washiriki wote hulipwa na waandishi wakiwemo!.

Jee unajua kuwa posho ya wabunge ni Sh. 200,000 kwa siku kwa kigezo kuwa gharama za maisha ya Dodoma zimepanda sana. Katika usawa wa binadamu, kama mhe. mbunge ni binadamu na mwandishi ni binadamu, kama anatakiwa kula vizuri na kulala vizuri, pia mwandishi anatakiwa kupewa haki zile zile!. Jee unajua waandishi wanalipwa posho ya shilingi ngapi kwa siku wawapo bungeni?.

Hili suala la bahasha za halali kwa waandishi, nitalitetea mpaka mwisho wangu!.

Tena mshukuru sitting alowances za vikao vya bodi nyingi ni siri, mngesikia baadhi ya wajumbe wa bodi fedha wanazolipwa kama posho tuu za kuhudhuria kikao kimoja ni zaidi ya mshahara wa mtu wa mwaka mzima!, msingethubutu hata kuzipigia kelele hivyo vijipunje kwenye bahasha za waandishi!.
Kuhusu hilo, nisome hapa Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...

Pasco.
 
Wakuu naomba nitofautiane na wenzangu kwenye baadhi ya maeneo.Kosa lake ni kuchukua rushwa,lakini mimi niko ndani ya jengo hilo na linavuja vibaya mno.Huyo Cleruu aliyetajwa ni Estate Officer wa Jumuiya.Wakandarasi wamemjengea hotel kubwa maeneo ya sakina kama ahsante.Kama hamwamini njooni kipindi cha mvua mtajionea wenyewe.
 
Back
Top Bottom