Mwanaume, Una miaka 26? Ingia kwenye ndoa, acha uoga

Ndoa sio jambo linalotegemea umri, ni jambo la utayari. Kama utasukumwa na umri ila ndani yako hakuna utayari utakuwa umepoteza muda.

Kwenye ndoa hatutafuti tu watoto kwamba umri wa miaka 29 unatakiwa uwe na watoto wawili blah blah..

Ndoa ni maisha wapo ambao wanao hao watoto, Mali n.k ila bado wanazikimbia ndoa zao. Pia kuzaa kwasasa sio kama zamani kwamba unazaa tu watoto nyumbani kuna mashamba watalima.

Sasa hivi ukizaa ujue umejiongezea jukumu kubwa sana ambalo linahitaji pesa yako, uangalizi wako, muda wako n.k.

Vijana wapewe elimu ha mahusiano na ndoa kisha waachwe wafanye maamuzi
Target yangu ni Vijana WA kiume wawe strong
 
Mume mpende mke wako na mke muheshimu mume wako,hii kauli haimaanishi wanaume hawahitaji upendo au wanawake hawahitaji kuheshimiwa Bali mume anazingatia sana kuheshimiwa yani hadhi na mamlaka yy ni kichwa Cha familia,halafu mwanamke anazingatia sana upendo yani urafiki na mambo kama hayo.Narudi kwenye hoja yako,hivi mtoa mada,kwa ulimwengu huu tulipofikia unahisi ili mwanaume apewe hiyo heshima anayostahili kwenye ndoa anahitaji mambo gani? Na ili amwonyeshe huyo mwanamke mapenzi anahtaj awe anamfanyia mambo gani? Hata hivyo kuoa ni jambo jema kwa watakaoamua lakini pia kuoa sio lazima(Kutokana na maandiko ya Biblia) ,hivyo acha Kila mtu afanye jambo lake kwa wakati wake na mustakabali wake.
 
Kuna msemo WA kataa ndoa ni msemo WA kioga kwa wAnaume Sababu kuu ya kataa ndoa ni.

Éti Wanawake ni wapenda hela, wajeuri hawajatulia.n.k.

Unakuta a man ni 29yrs anaogopa kuoa mwanamke mwenye elimu,pesa au mzuri kisa Eti atamsumbua

Bro kaza kiume ingia kwenye ndoa mpe mwanamke wako vigezo na masharit ya ndoa halafu stay real focus n'a maisha

Mwambie mwamke wako akupende asikupende Ila kukuheshimu ni lazima

Mwambie hakuna second chance akikucheat anarudi nyumban kwao stay strong .

tongoza mara moja kama hakutaki achan nae wanawake ni mwengi sana.

miaka 30 ni Muda WA kutafuta mtoto WA pili Mwanaume
Chief inashangaza huyotunaetaka kumuoa ni nani?kwan
 
Kuna kipindi nipo kitaa,hali ni tete,sijui pa kuanzia,giza totoro,nakutana na jamaa kafanyiwa kila kitu na wazazi wake,nyumba kapewa aishi bure,hajui kodi hua Tsh ngapi,gari kanunuliwa,mpk kuoa kasaidiwa baadhi ya mambo

Eti akawa ananisisitiza mimi nioe 🙆😊😄😄
Nilikua namuona ni mwehu sijui alitaka nije kuishi maisha gani na huyo mwanamke 🙆🙆

Jamani Maisha hatufanani
Pole
 
Back
Top Bottom