Mwanaume hutakiwi kufuata Dini ya mwanamke, Mwanamke ndio afuate yako

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
334
Anguko kubwa la mwanaume ni kuamua kubadilisha dini na kumfuata mwanamke. Mwanaume hutakiwi kubadilisha dini na kumfuata mwanamke bali yeye anatakiwa kubadilisha dini na kukufuata wewe.

Mwanamke anapoolewa na mwanaume, automatic huondoka katika jamii yake na kwenda katika jamii ya mwanaume. Kama alikuwa anaitwa Esta John na ameolewa na Pius Massawe, sasa ataanza kuitwa Esta Massawe na si John tena.

Anaondoka nyumbani kwao, anazaa watoto kwa ajili ya ukoo wa mwanaume na si wa mwanamke. Kwenye kitu muhimu sana unachotakiwa kujua, ni kwamba mwanamke anatakiwa kukufuata wewe.

Wakati Abraham amemuoa Sarai, mwanamke huyo alitoka kwenye familia iliyo na miungu yao, walikuwa na njia zao za kuabudu ila baada ya Abraham kutokewa na malaika kuambiwa ni kwa namna gani alitakiwa kuabudu, ni Mungu gani alitakiwa kumwabudu, sasa naye Sarai akatakiwa kumfuata.

Sarai hakumwamini Mungu wa Abraham, alitambulishwa kitu kipya kabisa. Alishazoea ibada za kwao huko, za miungu yao, hata Malaika alipomwambia Abraham kwamba Sarai atazaa akiwa na miaka 90, mwanamke huyo akacheka. Alicheka kwa kuwa hakumwamini Mungu mpya ambaye mume wake alimtambulisha, kila kitu kwake kilikuwa kigeni.

Sarai akaachana na miungu ya huko, sasa akaanza kumuabudu Mungu wa Abraham ambaye alimwamini mno. Kwenye kila jambo, Sarai alipokwenda vibaya, aliambiwa amekosewa, Mungu alitaka hiki na kile, hakutaka hili na lile.

Udhaifu wa kwanza wa mwanaume ni kubadili dini kisa mwanamke. Uanaume wako unaanza kuuuza hapo. Nguvu ya uanaume wako inaanza kupotea hapo. Mungu amempa nguvu kubwa mwanaume ila kuna mambo ukiyafanya kisa mwanamke, nguvu yako inapotea.

Unauacha uanaume wako kisa mapenzi, Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kisa njaa, yaani alishindwa kuhimili mambo hayo, akauza haki yake kwa ujumla.

Tupende, tuoe na tufanye kila kitu, ila usijaribu hata siku moja kuuza nguvu zako kama mwanaume. Kama hujaelewa, soma tena na tena.
 
Nimeelewa

41c4145a07cf291ef1a25f6cbf396710.jpg
 
Ndo maana nimeachana na dini, wanawake wanafanywa kama bidhaa yaani🚮

Hii misemo 'mwanamke hana dini' 'mwanamke hana kwao' siipendi kabisa

Sasa sijui nitaoaje oaje, au nitabaki kama mkristo hewa tu
 
Ushauri ninao wapa vijana ni kwamba.....
Nivyema ukaoa mwanamke anae kufaa, kijana oa mwanamke anae kusikiliza na anae kutii.
Ikiwa utafuata ushauri huu, hakika hautokaa upatane na shida nyingi zinazo kuteseni.
Na ukisha oa mwanamke, then usisahau kuishi nae kwa akili.
 
Ushauri ninao wapa vijana ni kwamba.....
Nivyema ukaoa mwanamke anae kufaa, kijana oa mwanamke anae kusikiliza na anae kutii.
Ikiwa utafuata ushauri huu, hakika hautokaa upatane na shida nyingi zinazo kuteseni.
Na ukisha oa mwanamke, then usisahau kuishi nae kwa akili.
Mbali na hayo yote Oa mnae abudu pamoja kama nyie ni watu wa Imani
 
Ndo maana nimeachana na dini, wanawake wanafanywa kama bidhaa yaani🚮

Hii misemo 'mwanamke hana dini' 'mwanamke hana kwao' siipendi kabisa

Sasa sijui nitaoaje oaje, au nitabaki kama mkristo hewa tu
Ukiwa kama binadamu huru still una option ya kufanya.

Ukifikia hatua ya kuoa tafuta mwanamke atheist muanzishe familia maisha yaende haina haja ya kuumiza kichwa.
 
Back
Top Bottom