Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Ukiona hivi ujue kuna wambea wamemtonya werema kuwa soon kikwete amepanga kutangaza kuwafuta nafasi zao
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Hivi ikitokea amekataa, itakuaje sasa? Au mara zote ni lazima rais akubali?
 
maigizo hayo. Amepigwa chini.hiyo kujiuzulu ni tafsida kutaka kujifariji tu na kuuhadaa umma kuwa serikali dhaifu kuna uwajibikaji na utawala boro kumbe amna lolote
 
Kuna nyimbo flani wameimba sijui ni wakenya au watu gani, chorus inaenda "who is the chicken now? kwakwakwakwaaka X 2"
Natamani watoe remix waimbe 'who is the tumbili now? werewerwereeee"
Nitachangia production.

KUJIUZULU HAKUTOSHI!!! BRING BACK OUR MONEY FOOLS!!!
 
Mimi nimeshasema. Kikwete anazidi kuunda matatizo makubwa zaidi kwa taifa. Eti anamsifia kwamb utumishi wake uliongozwa na uaminifu sijui na uadilifu. Inahitaji ujasiri wa kifisadi kutamka maneno haya hadharani bila hay akwa mhusika wa kashifa iliyo dhahiri.

Asije kumpa kazi nyingine ama kumfanya balozi kwa sababu anazidi kuhatarisha usalama wa nchi. Hawezi kuimarisha mtandao wa majizi kana kwamba nchi hii ni yake. Ninaamini maneno yaliyozagaa kwamba Accounts za escrow, zilizokuwa Stanbic, ni za kikwete, mkewe na familia yao ndiyo maana anaishia kujiuma uma na kufanya unafiki ili kuwapoza mafisadi wenzake, wasimuumbue. They are team mates!.

Tunahitaji watu wote waliohusika kwa kashifa ya escrow wawajibishwa kisheria na warudishe fedha zote. Hadith za kijinga n kuwafaya watanzania wote ni wajinga hazikubaliki.

Tulijua nia ya kikwete na lowasa kwenda ikulu haikuwa kuwatumikia wananchi. Ilikuwa ni kukidhi tamaa zao za anasa na mtamanio binafsi lakini hatukujua zitakuwa na syndicate ya wizi mkubwa kiasi hiki. Kikwete ni mwizi na ni kiongozi mkuu wa mafisadi. Anastahili kuwajibishwa kwa kushindwa kazi na kuhujumu uchumi wa nchi huku akijenga misingi ya machafuko nchini.

Huo ni mtandao mkubwa hao ni kama wale waarabu wa kile kisiwa kidogo wanajuana kwa vilemba vyao
 
Pesa zilikuwa BOT aliyesema zitoke zilipwe ni Werema na sasa kaachia ngazi, Mhongo akitoka lazima Gavana,Waziri wa Fedha,Waziri wa Viwanda na Biashara nao wang'oke kwani walifanya kazi sambamba iweje Mhongo ashinikizwe peke yake? Kisa ana Ugonvi na Mengi juu ya Udalali wa Vitalu vya Gesi, huku Mkono akiwa na Uchungu wa kunyang'anywa kazi zote za kisheria Wizara ya Nishati, Mhongo ni Shinikizo Binafsi la Mengi na Mkono kwa Manufaa yao, Tunaomba Kafulila na Zito nao wajiuzulu kwa kuwa walipewa pesa na Mengi ili wapaze sauti kwa Manufaa ya kuwafurahisha kisha kuwaaminisha wananchi ili wawaonee huruma mengi na mkono ambao pia si walipaji kodi ipasavyo, wao pia wakichunguzwa na FBI wana Madhambi lukuki, Nchi hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole, Watumishi wengi wa Umma wanaishi Kinyume na Vipato vyao Harisi, wakiletwa FBI hapa wawachunguze wote wenye Mali hakuna ambaye atapona.

Naona unamtetea profesa maandazi
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

dr Slaa, prof Lipumba, Mbowe, Mbatia - kesho ikipita kimya bila mmoja wenu au collectively kutoa karipio kali dhidi ya kauli hii ya profeza Jakaya, mtatukoma!!
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Safi sana Kama kweli tu2 Werema kajiuzulu bado tu2 muhongo na tu2 tibaijuka
 
0

MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI, JAJI WEREMA AJIUZULU
by GLOBAL
28 minutes ago


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema (pichani) leo amejiuzulu nafasi yake na tayari amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete asema amepokea barua yake na kumshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha katika kipindi cha utumishi wake.
Sababu ya kujiuzulu ni kwamba ushauri alioutoa kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka vizuri.
 
BBC wametangaza kupitia Star TV saa 3 kuwa Kaandika barua ya kujiuzulu kwa kuwa ushauri wake kuhusu ESCROW haukueleweka na umeleta hali mbaya ya hewa na JK amamkubalia!
 
Hivi karibu kumekuwa na watu wanazusha taarifa za uwongo. Neangalia ITV mwanzo mpaka
Mwisho sijasikia taarifa ya TATAA MURA kujiuzuru. Naomba ufafanuzi wadau!
ITV hii hii ya Tanzania au? Utakua umeangalia ITV ya Uingereza lakini hii ya Mengi hii habari ndiyo ilikua ya kwanza.
 
Wahisani wanataka kuona hatua stahiki zinachukuliwa dhidi ya wahusika....sasa mtu kajiuzuru kwa hiari yake hyo sivyo tutakavyo...afikishwe mahakamani akajibu tuhuma za kusababisha upotevu wa mabilion ya pesa za umma...
 
Back
Top Bottom