Mwanamke kuwa kiongozi wa Thailand

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Kiongozi wa upinzani wa Thailand, Yingluck Shinawatra ameshinda katika uchaguzi mkuu, miaka mitano baada ya kaka yake, Thaksin, kupinduliwa na jeshi.
110703150948_yingluck_shinawatra_304x171_bbc_nocredit.jpg


Matokeo yanaonesha kuwa chama cha Bi Yingluck, Puea, kimepata viti vya kutosha bungeni -- na hivo kumuwezesha kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo.
Waziri Mkuu wa sasa, Abhisit Vejjajiva, amekubali kushindwa.
Wakati wa kampeni vyama vote viwili vilitaka uhasama wa kisiasa ulioleta ghasia nchini humo kwa miaka kadha, umalizike.
Na Thaksin Shinawatra alisema wapigaji kura wa Thailand wamechagua mabadiliko na upatanishi katika taifa.
Akihojiwa na BBC kwa simu kutoka Dubai, ambako anaishi uhamishoni, Bwana Thaksin alisema, hatarudi haraka Thailand: anataka kuchangia katika suluhu siyo matatizo.
Alisema ana hakika kuwa dada yake ana uwezo wa kuongoza nchi
 
thats guuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuud!!!!!!!!!!

mungu ampe busara na hekima katika uongozi wake ameeeeeeeee.

i like t
 
Ni mabadiliko ya siasa za Thai, hata hivyo bado nashindwa kung'amua jinsi nchi itakavyoendeshwa na dada wa kiongozi aliyepinduliwa. Nadhani ni busara kwa Thaksin kutorejea haraka nchini mwake ili kuepusha ghasia zinazoweza kufuatia jeshi la nchi hiyo kumfurusha aliyekuwa PM miaka kadhaa iliyopita..punde tu baada ya ziara ya kiserikali iliyofanywa na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa nchini humo.
 
Back
Top Bottom