Mwanamke anayejituma au mtafutaji......

yaani house wife ana-deserve tena more than 100% maana huyo muda wote yupo home kuangalia familia, hiyo ndo kazi yake, na hana mshahara. na baba atakaye mtelekeza huyo mama sidhani kama atasamehewa.
sasa mwenzangu na mie unafanya kazi, una mshahara, unataka kila kitu kifanywe na baba................. nauliza tena na tena, wamama wa hivyo hela zao wanaona zinastahili kufanyia nini? kama chakula, mavazi, malazi, saluni ...... kila kitu kitoke kwa mume?

Kujenga kwao na kusaidia wadogo zake ada ya shule
 
hahahaha sweetlo gfsonwin.....ngoja sijui nikusubiri urudi home ama vipi......tunachosema hapa nadhani ni kupishana kiswajili tu, majukumu yote yanachukuliwa sawa tu ndani ya familia, kama anaenda saluni mfano na mi nipo around na hela karibu, anachukua mwenyewe kwen wallet kiasi atakacho....kama sijui ni nguo, zinahitaji hela...sio ishu, I mean I don't fee kuwa nafanya vile kama WAJIBU WANGU KAMA MUME (obligated) ila tunatambua kuwa tu wawili na kila kitu tunashare. hakuna specific activities. sasa kama hiyo kwa wengine inakufanya less romantic sijui but nadhani inawork kwa upande wangu na most cases kama hakuna matatizo mengine!
umeona enh!hiyo safi kikweli kuchukua hela ya kiranja mkuu kuna raha yake bana!we acha tu!hata 10000 tu!
 
kuna thread moja hapa inasema mume hana hela anakopa kwa jamaa rafiki wa mke wakati mke ana hela za kumwaga, hapohapo jamaa anakopa kwa mke anapewa. kwa sasa najiuliza, labda mume alikuwa anataka kufanyia kitu ambacho mkewe hakijui, otherwise kwa nini asingecheck na mke kujua kama ana hela ili wafanyie hicho kitu. au alimwomba mke akasema kuwa hana? kama aliamua kumyima mumewe hela wakati anajua kwa-haki ya Mungu kuwa mumewe hana hela alikuwa na maana gani? halafu anampa mtu ambaye si mumewe....................... ndoa nyingine!

hahaha FP niliposoma ile sredi nilijuwa kuna matatizo kwen hiyo ndoa. Hata kama hakuna basi wana operate kwenye model ya cha mume cha wote cha mke cha mke. sasa kasheshe ukute alikuwa anakopa hiyo laki ili akampe mkewe elf 50 ya saluni ili aonekane anamjali mkewe! hahahahaha
 
Last edited by a moderator:
wanaume! wanaume! wanaume Ee mola wape moyo wa kujali familia, kila mwanaume anaejali familia huwa anabarikiwa sana na kupata mafanikio makubwa.
 
inategemea na walivyoanza toka mwanzo kama hazikuwepo basi jua hazipo ila kama ilikuwa desturi zitaendelea kuwepo
 
come again?

Mr. Kaizer nina maana kuwa unawezakuta mwanaume ana hela lakini hajali familia yake sio mke bali hata watoto wake pia. na hii husababisha stress kwa mke wake majonzi ya watoto na hupelekea kukosa baraka, simaanishi kuwa ni wote ila baadhi yao. do u copy me?
 
oooh now yes Ms mdida. wanaume wa ivo sio wanaume ni wa jinsia ya kiume tu...hizo hela zinakuwa za kufanyia nini?
 
Last edited by a moderator:
Siku zote nasema na nitazidi kusema kuwa Mwanamke ndio hu determine nyumba, familia na ndoa itakuwa inaendeshwa kwa namna ipi. Katika jamii zetu za Kiafrika kiutamaduni imejengeka kuwa mwanaume anatakiwa a provide kwa ajili ya familia yake.. (ni kitu ambacho kinaendelea hadi sasa thou kikienda kikipungua kwa kasi tokana na sababu mbali mbali).

Ndio maana ni bora toka mwanzo mkaweka mazoea ili yajijenge. Sio wanaume wote wanapenda kufanya majukumu yao in the line of 'family responsibility'. Ni wachache (God Bless their souls) ambao HUJITUMA kwa dhati kuwa ni wajibu wake kujali familia no matter mkewe ana kipato ama Lah. Wengine hufanya sabababu ni obligation... Mke ukilegeza kamba ukajifanya unaweza bila yeye, then imekula kwako...

Hivo unapokuta mume mvivu, mtegevu, mpenda kujirusha hasa kimagenge na nadra na familia, asiyokuwa na focus hasa katika maendeleo, asiyefanya bila kusukumwa ndio mumeo na wewe wajituma. Unaweza kuta unasimamia familia yenu na mwisho wa siku anakopa hadi hela kwako akichacha (na hali ha provide).

Mie naamini katika kugawana majukumu (hasa kama mwanamke na wewe wajishughulisha); sababu at the end of the day he is human too... Kuna wakati anachoka nae anahitaji support. Hapo ni bora kabisa mkagawana majukumu tokana na kipato chenu, mjue kabisa tuna joing account ambayo hiatakiwi kugusa (ni kwa ajili tu ya family emergencies) nje ya wajibu kama chakula, bills, na the like. Hio inasaidia hata kuwepo na amani ndani ya nyumba... Sasa hivi ugomvi wa wanandoa wengi upo 'economically based', hivo hio sector ikisimamiwa vema inaweza kuwa msaada sana kwa wana ndoa...

Ashukuriwe Mungu wife huwa haingii JF. Maana asije kujifunza ku-argue kama akina AshaDii.
 
Last edited by a moderator:
Kujenga kwao na kusaidia wadogo zake ada ya shule
haya ni mawazo ya wamama ambao wapo mguu ndani mguu nje kwenye ndoa zao. kama upo pale kustay huwezi waza hivyo (sikusemi wewe jodoki , nawasema wale wanaofanya hivyo)
 
Last edited by a moderator:
hahaha FP niliposoma ile sredi nilijuwa kuna matatizo kwen hiyo ndoa. Hata kama hakuna basi wana operate kwenye model ya cha mume cha wote cha mke cha mke. sasa kasheshe ukute alikuwa anakopa hiyo laki ili akampe mkewe elf 50 ya saluni ili aonekane anamjali mkewe! hahahahaha
si ndo hapo! labda hakumwambia mkewe kuwa ameishiwa.................. na kama anajua mke ni material basi anajua nikitangaza kufilisika tu basi sina mke.
kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia mkewe alikuwa mfanya kazi, tena ana masters lakini akaamua hataki tena kazi sababu mshahara sio mzuri, mume akawa anamshauri asiache kazi mpaka apate nyingine. wameenda kama miaka 2 kila siku mke anaimba kuacha kazi, mume anashauri asiache, siku moja mke akamwambia kuanzia wiki ijayo naacha kazi, kama unaona mzigo kukaa na mke asiye na kazi nirudishe kwetu wazazi wangu watanitunza..................... unalo!
 
Madam, unalosema ni kweli kabisa kwani MUNGU alisema mwanume utakula kwa jasho na mwanamke utazaa kwa uchungu. alimaanisha ni kazi ya mwanaume kuiwezesha familia kwa kila kitu.

lakin kwa maisha ya sasa sivyo, mwanamke nae anatafta kipato, mnarudi nyumbani pamoja mnamtegemea hsgirl kutimiza majukumu yote ya ndani, ambaye analipwa na father house. sasa wewe mwanamke unataka mume akupe eti pocke money, hela ya salun, mavazi nk huku wew majukumu ya ndani umemuachia hsgirl.!!!!!!

kuna mtu aliwasi sema, yeye kama mke wake akitaka ampe kila kitu wakati nae anafanya kazi, basi akifika nyumani hata kama wamerudi paamoja, ampe chakula, maji ya kuoga, watoto wameoga na kila kitu bila kujali ataweza vipi wakati wamerudi pamoja saa hiyo.

Jamani hamjaambiwa mtoe kila mara lakini mara moja moja kwa kweli inatoa changamoto. Hizo nguo na salun expenses at the end anaefaidika ni baba wa nyumba, mavazi si lazima yale ya kitchen party kuna yale ya wawili usiku nayo yanaleta mshawasha kwenye uhusiano, kwanini hamuangalii hili on +ve side.
 
Angalau wewe una sound realistic zaidi! Mara kwa mara huwa namkumbusha make wangu kuwa ajaribu kuishi maisha ambayo leo au kesho 'nikiitwa mbele za haki' asitetereke sana!

Ñi kweli,kuna leo na kesho hivyo tuhakikishe tunasave na kushare majukumu,

Mimi nimejifuta kabisa FB maana nilikuwa kwenye group linaloweka nguo mpya kila kukicha linamaliza vijisenti vyangu, nikaona ya nini nichop my money on new stuff kila kukicha nimeridhika na nilizo nazo nanunua nguo mpya nikipata zali la nje tu au harusi ya close relative
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Injinia Nsiande nimepeda saaana mtazamo wako

nimemsoma kamusi an am like "he! hili linawezekana kweli" na by the way anaishije na ndugu zake watatu nyumbani? siku hizi hayo mambo yapo kweli? wanafanya nini?

Ila binafsi, labda pengine tupo huru sana, kwetu siye we share kila kitu hakuna mwenye 'chake' per se....na kila jukumu kila mmoja ana feel responsible nalo...so si ndio usawa huu wajameni?

Safí saña! Hello Twin !
 
Last edited by a moderator:
school fees za ckuiz ni milion milion tu, rent ya nyumba, na gari lake ni muwekee mafuta?, hela ya saluni?, msosi home sasa hela yake mwanamke inafanya kazi gani?
 
haya ni mawazo ya wamama ambao wapo mguu ndani mguu nje kwenye ndoa zao. kama upo pale kustay huwezi waza hivyo (sikusemi wewe jodoki , nawasema wale wanaofanya hivyo)

Ni kweli kabisa wenye mawazo ya mguu ndani mguu nje ndio huwa hivyo, kikubwa ni mshikamano katika kuhakikisha kila mmoja ana mchango katika maendeleo ya familia though mwanaume inabidi ajitambue yeye ni kichwa cha familia hata kama amebahatika kupata mke mwenye kuchacharika, madam x ameleta thread nzuri sana ya kukumbusha hata kama mwanamama ana kipato si mbaya once in blue moon kumnunulia kitu.
 
school fees za ckuiz ni milion milion tu, rent ya nyumba, na gari lake ni muwekee mafuta?, hela ya saluni?, msosi home sasa hela yake mwanamke inafanya kazi gani?
si wamesema huko ni ya serengeti boys? ha haaaaaaaaa usiue mtu
 
si ndo hapo! labda hakumwambia mkewe kuwa ameishiwa.................. na kama anajua mke ni material basi anajua nikitangaza kufilisika tu basi sina mke.
kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia mkewe alikuwa mfanya kazi, tena ana masters lakini akaamua hataki tena kazi sababu mshahara sio mzuri, mume akawa anamshauri asiache kazi mpaka apate nyingine. wameenda kama miaka 2 kila siku mke anaimba kuacha kazi, mume anashauri asiache, siku moja mke akamwambia kuanzia wiki ijayo naacha kazi, kama unaona mzigo kukaa na mke asiye na kazi nirudishe kwetu wazazi wangu watanitunza..................... unalo!

mi ningemrudisha tu.
 
Back
Top Bottom