Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
Weekend hii nilimpitia mshikaji wangu mmoja pamoja na rafiki yake wa kike ili twende kwenye party. Nilipofika nilikuta mtafaruku fulani kuhusu nguo gani avae shemeji. Mshikaji alimng'ang'ania shemeji avae nguo ndefu wakati shemeji alin'ga'ngania anataka avae nguo fupi. Huyo mshikaji akawa anamwambia unataka kumfurahisha nani huko na dada akajibu "naipenda tu nguo hii na nikivaa nahisi kupendeza. Kwa hiyo nafurahia mwenywe wala simfurahishi mtu kama unavyodhani". Mshikaji wangu alisisitiza kwamba yeye ndo alitakiwa afurahishwe.
Baada ya kuwasihi kwa muda walielewana, shemeji akatinga kivazi kirefu na tukaenda zetu kula raha.
Tukio hili linikumbusha rafiki yangu mmoja ambaye mke wake aligombana na mama mkwe wake kwa kumzuia kuvaa nguo fupi. Mke alisisitiza kuwa kwa kuwa mume wake anaridhika yeye haoni tatizo.
Hivi, mwanamke anapojipigilia pamba akapendeza lengo linakuwa ni kuifurahisha nafsi yake, au kumfurahisha ampendaye, kuwafurahisha walimwengu au kuwaonyeshea wanawake wenzake?