Mwanamke akipendeza anamfurahisha nani?

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Weekend hii nilimpitia mshikaji wangu mmoja pamoja na rafiki yake wa kike ili twende kwenye party. Nilipofika nilikuta mtafaruku fulani kuhusu nguo gani avae shemeji. Mshikaji alimng'ang'ania shemeji avae nguo ndefu wakati shemeji alin'ga'ngania anataka avae nguo fupi. Huyo mshikaji akawa anamwambia unataka kumfurahisha nani huko na dada akajibu "naipenda tu nguo hii na nikivaa nahisi kupendeza. Kwa hiyo nafurahia mwenywe wala simfurahishi mtu kama unavyodhani". Mshikaji wangu alisisitiza kwamba yeye ndo alitakiwa afurahishwe.

Baada ya kuwasihi kwa muda walielewana, shemeji akatinga kivazi kirefu na tukaenda zetu kula raha.

Tukio hili linikumbusha rafiki yangu mmoja ambaye mke wake aligombana na mama mkwe wake kwa kumzuia kuvaa nguo fupi. Mke alisisitiza kuwa kwa kuwa mume wake anaridhika yeye haoni tatizo.

Hivi, mwanamke anapojipigilia pamba akapendeza lengo linakuwa ni kuifurahisha nafsi yake, au kumfurahisha ampendaye, kuwafurahisha walimwengu au kuwaonyeshea wanawake wenzake?
 
The lady is right!
Kupendeza siyo kwa ajili ya kufurahisha wengine bali ni kwa ajili ya mvaaji mwenyewe. Ukipendeza unakuwa na confidence about yourself!
Mweleze rafikio kuwa kama mara zote amekuwa akiamini ati huyo mdada anampendezea yeye anajidanganya.Akifurahi kupendeza huko basi hiyo ni ziada tu hahahahah.
 
nafsi yake, kumfurahisha ampendaye, kuwafurahisha walimwengu au kuwaonyeshea wanawake wenzake/wanaume pia
 
Wanawake ni mapambo ya Dunia - Hupendeza kwa kila KIUMBE!

Yaelekea mshikaji wako hajui tofauti ya kupendeza, kuvutia na kutamanisha! Na ukiweza mpeleke pale Magomeni - panaitwa Traventine - siku ya Taarabu ajionee tofauti ya mavazi ya kike!

hao walikuwa na kigine wanagombania , we hukkijua tu. sio nguo, kama nguo ilitumika basi kiikuwa chambo tu.

kimsingi mwnamke akipendeza lazima imfurahishe mume pi. ikitokea akafurahi mwanamke pekee bila mume kufurahi, pana walakini hapo na hizo confidence anazozungumzia wos si lolote kama hukuzipata kwa mume wako. i mean kama huna confidence kwa mume wako, huwezi kuzipata kwenye pamba...............
 
napenda nivae vile nitakavyo amua ..aaha haya mambo ya kuchaguliana uanweza vaa oversize
 
unatakiwa kama umeolewa au unaumpendaye kwa dhati ndo umfurahishe kama alivyoamua kuvaa alopenda mpnz wake hapo safi
 
Anaye vaa baibui anamfurahisha nani?
icon10.gif
 
hao walikuwa na kigine wanagombania , we hukkijua tu. sio nguo, kama nguo ilitumika basi kiikuwa chambo tu.

kimsingi mwnamke akipendeza lazima imfurahishe mume pi. ikitokea akafurahi mwanamke pekee bila mume kufurahi, pana walakini hapo na hizo confidence anazozungumzia wos si lolote kama hukuzipata kwa mume wako. i mean kama huna confidence kwa mume wako, huwezi kuzipata kwenye pamba...............
Hili nalo wazo kama kuna mawazo chanya kwa huyo mume! Kuna wengine hawapendi mke/mpenzi aonekana mtanashati kwa watu.. na hivyo hujitahidi sana kuficha wasipendeze kwa hofu ya kitu fulani.

Hujasikia wanaume wengine wakikataza wake zao kutengezea nywele, kuvaa mitindo fulani n.k? Sasa huku ndio kukosa confidence kwa mkatazaji maana hajiamini kuwa ni yeye tu!
Ila mwisho wa siku pamoja na kupendeza lazima staha/heshima nayo iwepo na siyo kuvaa mivalio yenye kukutia aibu wewe na wale walio karibu nawe.
 
mwanamke ni UA zuri lipambalo dunia hii, mimi hupenda sana kuvaa Tshirt na Jeans na raba nikiwa home hapo kwa kweli nakuwa na confidence ya hali ya juu, lkn wife hapendi kabisa raba anataka nivae sandals., hii hainipi mie confidence kwa hali ninayotaka lkn hapa nakuwa nimemfurahisha yeye. Mimi naona kama uko naye, mwache avae vile anavyoona yeye inampa raha ilimradi asiwe nusu uchi, lkn km ni kimini cha kimtindo mwache ajivinjari, labda kama umri wetu ni mkubwa lakini kama ni vijana, sioni kibaya sana hapo.SO sidhani kuvaa kuna wajibika kumpendezesha fulani ila ni wewe kuvaa vile ambavyo inakupa confidence na raha ndano ya roho.
 
unatakiwa kama umeolewa au unaumpendaye kwa dhati ndo umfurahishe kama alivyoamua kuvaa alopenda mpnz wake hapo safi

Wanawake hawaeleweki kabisa. Yeye anataka avae anavyopenda ili aifurahishe nafasi yake lakini wewe (mume au boy friend) uvae anatavyotaka yeye ili umrahishe na usimtie aibu akikutana na wezake!!:confused::confused:

Wengine tumeamu kukubali yaishe. Kama nguo hainitii aibu avae tu na mimi navaa anavyotaka ili aifurahishe roho yake. Hakuna sababu ya kugombana bure kwani zaidi ya hapo ni kuingia ulingoni na kutest vichwa kama kondoo.
 
mimi navaaa nguo inayonifanaya nijiskie comfortable, confident na decent!!!

nataka niritdhike mwenyewe na nilichovaa na si vinginevyo.
 
Wanawake hawaeleweki kabisa. Yeye anataka avae anavyopenda ili aifurahishe nafasi yake lakini wewe (mume au boy friend) uvae anatavyotaka yeye ili umrahishe na usimtie aibu akikutana na wezake!!:confused::confused:

Wengine tumeamu kukubali yaishe. Kama nguo hainitii aibu avae tu na mimi navaa anavyotaka ili aifurahishe roho yake. Hakuna sababu ya kugombana bure kwani zaidi ya hapo ni kuingila ulingoni na kutest vichwa kama kondoo.

hahaaaaa sasa kama ulikuwa unavaa zile suruali za vitambaa zenye selebresheni kwa pale mbele na turn-up za ajabu ajabu akuache tu....................

hahaaaaaaaaaaaaaaa DC umenifurahisha kwa kukubali yaishe
 
Anaifuraisha nafsi yake na walimwengu, huyo jamaa yake aache wivu, wana wa nchi tuahitaji kuona uumbaji ili kama vipi tubeep!!
 
mimi navaaa nguo inayonifanaya nijiskie comfortable, confident na decent!!!

nataka niritdhike mwenyewe na nilichovaa na si vinginevyo.

Mbona bado naona ka element ka-umimi (selfness)? Kwani imebadilika lini kutoka kwenye hii kanuni ya ndoa,

Marriage >>>1+1=1 na kuwa 1+1=2?

Sasa huoni ukinilazimisha kuwa wewe uko comfortable wakati mimi nimekereka akili inaweza kuweweseka tukaishia kuchapana makonde au kuvunja safari? Kwa nini tusitumie kanuni ya JK kwama "kula na wewe uliwe" badala yake unataka mwenzio ndiye aliwe tu?
 
kumbe hii ni kwa wanandoa tu....DC mi sikujua bana!!

i will consider my hubby ntakapofunga ndoa......

for now najikonsider mwenyewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom